Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-07 16:20:32    
Majeshi ya muungano ya Marekani na Iraq yashambulia vikosi vya "al-Qaeda"

cri

Tarehe 6 ni siku ya pili tokea jeshi la Marekani nchini Iraq na vikosi vya usalama vya Iraq vianze operesheni ya "Pazia la Chuma cha Pua" kwenye sehemu ya mpakani kati ya Iraq na Syria. Askari wa Marekani na Iraq walipambana vikali na vikosi vyenye silaha vya Iraq, na raia wengi walikimbia makazi yao.

Tarehe 5 jeshi la Marekani nchini Iraq na vikosi vya usalama vya Iraq vilifanya operesheni ya kijeshi inayoitwa "Pazia la Chuma cha Pua" kwenye sehemu ya Husaybah, magharibi mwa Iraq karibu na mpaka wa Syria. Jeshi la Marekani linaona kuwa sehemu hiyo ni njia muhimu ya "al-Qaeda" kwenda kwenye bonde la mto Euphrates, likikata njia ya magaidi wa nchi za nje, fedha na zana za kivita ili kuharibu mfumo wa ugaidi wa "al-Qaeda" katika sehemu hiyo ili kurudisha usalama na utulivu kwenye sehemu ya mpaka kati ya Iraq na Syria na kuboresha hali ya usalama kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 15 Desemba. Lengo lingine la operesheni hiyo ni kuishinikiza Syria. Jeshi la Marekani tarehe 5 lilishutumu serikali ya Syria kwa kutowajibika ipasavyo katika usalama wa mpakani, na kuona kuwa "al-Qaeda" iliingiza watu wenye silaha, fedha na silaha nchini Iraq kutoka kwenye mpaka wa Syria.

Inasemekana kwamba, Husaybah ni mji uliopo magahribi mwa mkoa wa Al-Anbar, kilomita 320 kutoka Baghdad, mji huo una jumla ya watu 30,000 na wakazi 4,000, kati ya watu hao wengi zaidi ya wa madhehebu ya Suni. Askari 3,500 wa jeshi la Marekani na Iraq walishiriki katika operesheni hiyo, kati yao, askari wa Marekani 3,500 na askari wa Iraq 1,000, hii ni mara ya kwanza kwa vikosi vya Iraq kushiriki kwa wingi kwenye operesheni inayoongozwa na Marekani.

Habari kutoka gazeti la New York Times zinasema kuwa askari wa Marekani tarehe 5 walifanya msako wakisaidiwa na vifaru katika mji wa Husaybah. Kutokana na upinzani mkubwa wa watu wenye silaha, askari wa Marekani walishindwa kudhibiti sehemu yoyote ya mji huo. Habari kutoka mtandao wa internet wa CNN zinasema kuwa tarehe 5 askari wa Marekani walipambana kwa dakika 20 na watu wenye silaha karibu na msikiti mmoja mjini humo, na katika mapambano kwenye sehemu ya kusini magharibi ya mji huo askari wa Marekani waliwaua watu wenye silaha kumi kadhaa. Jeshi la Marekani tarehe 6 lilitangaza kuwa jeshi hilo lilifanya mashambulizi angani kwa mara zisizopungua 9 kwenye sehemu zinazoshukiwa kufichwa watu wenye silaha na kulipua gari moja linaloshukiwa kuwa na baruti. Hivi sasa bado hakuna ripoti kuhusu askari wa Marekani waliokufa au kujeruhiwa.

Kutokana na operesheni hiyo, wakazi wengi walikimbia makazi yao. Watu walioshuhudia walisema, baadhi ya wakati waliondoka Husaybah kwa miguu huku wakiwa wakishika vijiti vyenye vitambaa vyeupe, kwa sababu jeshi la Marekani liliwahi kuonya kuwa watu walioondoka kwa gari pengine watafyatuliwa risasi. Mwalimu Ahmed Mukhlef mwenye umri wa miaka 35 alisema, asubuhi tarehe 6 aliposikia milio ya bunduki aliacha nyumba na gari na kukimbilia mji mwingine ulio karibu akiwa pamoja na mkewe na watoto wake.

Jeshi la Marekani tarehe 6 lilisema kuwa askari wanne wa Marekani walikufa na watatu walijeruhiwa katika mapambano ya siku hiyo. Isitoshe, msafara wa askari wa Marekani ulishambuliwa na makombora, raia mmoja wa Iraq aliuawa na watatu wa Iraq kujeruhiwa. Katika siku hiyo "sehemu ya kijani" iliyolindwa sana na askari wa Marekani pia ilishambuliwa kwa mizinga, raia wawili waliuawa.