Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-08 17:50:08    
Duru jipya la mazungumzo ya pande 6 lastahili kuwa na matarajio

cri

Duru jipya la mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea litafanyika tarehe 9 hapa Beijing. Je, pande mbalimbali zimefanya juhudi gani ili kusukuma mbele maendeleo ya mazungumzo hayo? Je duru jipya la mazungumzo hayo litapata maendeleo makubwa au la? Mwandishi wetu wa habari Bibi Pan Xiaoying alisema:

Ili kuandaa duru la 5 la mazungumzo ya pande 6, China imedumisha mawasiliano barabara na pande nyingine 5, balozi wa China anayeshughulikia mambo ya peninsula ya Korea Bwana Li Bing alifanya ziara nchini Korea ya kaskazini, Marekani na Korea ya kusini. Jambo linalostahili kutajwa ni kuwa, rais Hu Jintao wa China aliitembelea Korea ya kaskazini mwishoni mwa mwezi Oktoba, ambapo alibadilishana maoni na kiongozi wa Korea ya kaskazini Kim Jong il kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea, na wameona kwa kauli moja kuwa, matokeo yenye juhudi yalipatikana katika duru la 4 la mazungumzo ya pande 6, na pande zote husika zitatekeleza taarifa ya pamoja na kuendelea na juhudi ili kutimiza lengo la kuifanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na nyuklia. Aidha, China na upande wa Japan na upande wa Russia pia zimedumisha mawasiliano, China imeweka hali nzuri kwa ajili ya kufanyika kwa duru la 5 la mazungumzo ya pande 6 bila vikwazo.

Suala la nyuklia la peninsula ya Korea linahusiana moja kwa moja na uhusiano kati ya Korea ya kaskazini na Korea ya kusini pamoja na amani ya peninsula nzima ya Korea. Hivyo Korea ya kusini pia imefanya juhudi kubwa za usuluhishi na usawazishaji kuhusu suala hilo. Mwandishi wetu wa habari aliyeko Korea ya kusini alisema:

Baada ya kumalizika kwa duru la 4 la mazungumzo ya pande 6, rais wa Korea ya kusini alipoongea kwa simu na viongozi wa nchi zinazohusika alisema kuwa, Korea ya kusini itashirikiana na nchi mbalimbali katika kufanya juhudi za kulitatua mapema iwezekanavyo suala la nyuklia la peninsula ya Korea. Kiongozi wa ujumbe wa Korea ya kusini pia alifanya ziara nchini China na Marekani.

Mwandishi wetu wa habari aliyeko Japan alisema:

Kabla ya kuanzishwa kwa duru jipya la mazungumzo ya pande 6, mawasiliano kati ya Korea ya kaskazini na Japan pia yameweka hali nzuri kwa mazungumzo hayo.

Na mwandishi wetu wa habari aliyeko Russia alisema:

Wanadiplomasia wa Russia wanakaribisha duru la 5 la mazungumzo ya pande 6, wanatumai kuwa mazungumzo hayo yatapata njia halisi ya kutekeleza taarifa ya pamoja.

Lakini Korea ya kaskazini na Marekani ambazo ni wahusika muhimu wa suala la nyuklia la peninsula hiyo, bado hazina moyo wa kuaminiana kuhusu masuala kadhaa muhimu, kila upande unashikilia maoni yake pekee. Ingawa pande hizo mbili zimefanya mawasiliano mara kadhaa katika mwezi mmoja na zaidi uliopita, lakini migongano kati yao bado haijapungua. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Korea ya kaskazini aliona kuwa, serikali ya Marekani inaitilia shinikizo Korea ya kaskazini na kujaribu kuifanya Korea ya kaskazini ikubali ombi la Marekani la kuitaka iache kwanza mpango wa nyuklia. Lakini Marekani inaona kuwa, matakwa husika ya Korea ya kaskazini ni masharti kwa mazungumzo ya pande 6, na hii ni kinyume na taarifa ya pamoja.

Migongano hiyo na hali ya kutoaminiana kati ya Korea ya kaskazini na Marekani huenda itaathiri moja kwa moja duru la 5 la mazungumzo ya pande 6, na duru jipya la mazungumzo hayo huenda litakutana na taabu kubwa zaidi. Vyombo vya habari vinatumia kuwa pande husika zitaongeza maelewano na uaminifu, pia kuonesha hali unyumbufu ili kusukuma mbele kwa pamoja mchakato wa mazungumzo ya pande 6.