Hadi tarehe 8 bei ya mafuta katika soko la Marekani imeshuka hadi chini ya dola za Kimarekani 60 kwa pipa, bei hiyo imepungua kwa asilimia 16 ikilinganishwa na bei ya mwishoni mwa mwezi Agosti. Wachambuzi wanaona kuwa bei ya mafuta duniani inaathiriwa na sababu nyingi, hivi sasa mwelekeo wa kuendelea kushuka chini kwa bei ya mafuta bado haujaweza kubainika.
Tokea mwezi Oktoba bei ya mafuta katika soko la Marekani ilikuwa ikiyumbayumba kwenye dola za Kimarekani 60 kwa kila pipa, lakini tarehe 7 Novemba, bei ikashuka hadi kufikia dola za Kimarekani 58.6 kwa pipa, bei hiyo ni ndogo kabisa tokea tarehe 26 mwezi Julai. Wachambuzi wanaona kuwa sababu moja kwa moja ya kusababisha kushuka kwa bei ni kuwa, mwaka huu hali ya hewa haitakuwa baridi katika majira ya baridi kama ilivyokuwa zamani nchini Marekani. Hivi sasa, Marekani imeingia katika kipindi cha kupasha moto kwa mafuta zaidi ya wiki moja, lakini kutokana na vuguvugu la halijoto, watu hawajaanza kuleta joto kwa mafuta. Sababu ya pili ni kuwa, wizara ya madini ya Marekani tarehe 7 ilitangaza kuwa, kutokana na kuathiriwa na kimbunga cha "Katrina" na "Rita", 51.54% ya visima vya mafuta na 44.82% vya gesi kwenye ghuba ya Mexico havijafufua uzalishaji, lakini takwimu hizo pia zimeonesha kuwa uzailshaji wa mafuta katika sehemu hiyo umekuwa ukirudishwa, hali mbaya ya upatikanaji mafuta katika soko la Marekani inatazamiwa kutengamaa. Tatu, wadau wanaona kuwa ripoti itakayotolewa na wizara ya nishati ya Marekani kuhusu akiba ya mafuta nchini Marekani itaonesha kuwa akiba ya mafuta na gesi itaongezeka.
Ingawa sababu hizo zitasaidia bei ya mafuta kushuka, lakini pia kuna mambo mengine ambayo yatasababisha bei ya mafuta kupanda, kwa hiyo bei ya mafuta duniani bado haiwezi kubainika kuwa itaendelea kushuka.
Kwanza, mabadiliko ya hali ya hewa hayana sheria. Ingawa mwaka huu hali ya hewa inaelekea kuwa joto katika majira ya baridi nchini Marekani, lakini mabadiliko ya hali ya hewa ni mengi, katika majira ya baridi yenye miezi minne, ni vigumu kubashiri hali ya hewa itabadilika vipi, ingawa mabadiliko ya hali ya hewa yataathiri bei ya mafuta kwa muda mfupi.
Pili, tokea mwaka jana, mambo ya vita, hali ya hewa, siasa na magendo ya mafuta yalisababisha bei ya mafuta kupanda na kutokea upungufu wa mafuta, na OPEC ilishindwa kudhibiti bei, bei ya mafuta ikawa inashindwa kutulia na kuathiriwa na tukio japokuwa dogo.
Tatu, nchi zinazotumia mafuta mengi, hasa Marekani, hazikuwajibika ipaswavyo. Marekani ni chanzo muhimu cha kusababisha mabadiliko ya bei ya mafuta duniani, matumizi yake yanachukua robo ya mafuta katika biashara ya mafuta duniani, lakini rais Bushi wa Marekani anafurahia bei kubwa ya mafuta. Vyombo vya habari vya Misri vilitangaza moja kwa moja kuwa Marekani ni chanzo muhimu cha kusababisha ongezeko la bei ya mafuta. Kwa sababu bei kubwa ya mafuta inaweza kuziletea faida kubwa nchi za ghuba zinazozalisha mafuta na kuziwezesha nchi hizo kuisaidia Marekani kwa fedha zinazotumika katika vita vya Iraq. Pamoja na hayo, bei kubwa ya mafuta itakwamisha uchumi wa nchi zinazoshindana na Marekani zikiwa ni pamoja na Japan, China na nchi za Umoja wa Ulaya ili Marekani iendelee kuwa na nguvu duniani.
Kutokana na hali ambayo bei ya mafuta ilikuwa kubwa bila kushuka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, tunaweza kusema kuwa ingawa bei ya mafuta inaamuliwa na hali ya mahitaji na kiasi cha uzalishaji, lakini hali nyingine pia inaamua bei ya mafuta.
|