Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-09 18:39:09    
Mapishi ya kamba-mwakaje kuwa kama jiwe linalong'aa

cri

Mahitaji

Kamba-mwakaje gramu 200, kiasi kidogo cha vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi iliyokatwa vipande kidogokidogo, ute wa yai, wanga, chumvi, M.S.G.

Njia

1. osha kamba-mwakaje na uwakaushe. Waweke kwenye bakuli moja, tia chumvi, M.S.G, korogakoroga. Tia mvinyo wa kupikia, tia wanga na ute wa yai korogakoroga. Mimina mafuta kidogo.

2. tia mafuta kwenye sufuria pasha moto mpaka yawe na joto la nyuzi 20, tia kamba-mwakaje, koroga kwa haraka mpaka wagawaike halafu wapakue.

3. tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi, mimina maji kidogo, tia kamba-mwakaje ndani ya sufuria , tia chumvi, M.S.G koroga koroga, mimina maji ya wanga, na kisha upashe moto tena. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.