Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-11 19:30:30    
Biotekinolojia ya chakula ya China yafaa sana kwa nchi za Afrika

cri

Kuanzia tarehe 20 Oktoba hadi tarehe 28 Novemba, semina ya kuwaandaa wanafunzi kutoka nchi zinazoendelea hasa kutoka nchi za Afrika kuhusu biotekinolojia ya chakula yanafanyika hapa Beijing. Semina hiyo iliendeshwa kwa pamoja na wizara ya biashara ya China na taasisi ya utafiti wa chakula na umuaji wa chakula cha China.

Wiki iliyopita tuliwaletea maelezo kuhusu jinsi wanafunzi kutoka Kenya, Tanzania na Uganda wanaoshiriki semina hiyo wanavyoiona China kwa macho yao wenyewe. Leo tunaendelea kuwaletea mazungumzo ya wanafunzi wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki.

Bwana Fredrick Mohamed Kiilu kutoka wilaya ya Machakos, mkoa wa mashariki nchini Kenya ni mfanyabiashara mdogo, ana kiwanda kidogo cha kutengeneza vinywaji na bidhaa nyingine za matunda. Alisema kuwa, biotekinolojia aliyojifunza hapa China itamnufaisha yeye na wanaviwanda wadogo wadogo wengine wa Kenya. Anatumai kuwa, licha ya biotekinolojia ya chakula, zana za China pia zitaweza kupatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu huko Kenya. Akisema:

Bi. Sarah Lifa ni ofisa mtafiti wa maendeleo wa chakula na biotekinolojia kutoka shirika la utafiti na maendeleo ya viwanda ya Tanzania. Alisema kuwa, China ni nchi inayoendelea sana katika elimu ya biotekinolojia, inatumia ujuzi huu kukidhi haja ya chakula ya idadi kubwa ya watu. Aliona kuwa, biotekinolojia ya chakula ya China inafaa sana kwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Baada ya kurudi nchini Tanzania, atatumia elimu aliyopata hapa China kuendeleza viwanda vya vyakula vya Tanzania. Akisema:

Bw. N. C. Macharia ni ofisa anayeshughulikia mambo ya viwanda ya wizara ya biashara na viwanda ya Kenya, baadhi ya kazi yake ni kutoa ushauri kwa wafanyabiashara na wawekezaji wadogo wadogo. Aliona kuwa, biotekinolojia aliyopata hapa China itaweza kuwaletea faida kubwa wawekezaji wadogo wadogo katika kusindika malighafi za kilimo ili kuongeza thamani ya mazao ya awali ya kilimo ya nchini kwao. Akisema:

Bi. Jane Wanjiru Wambugu anatoka wilaya ya nyeri ya mkoa wa kati wa Kenya, kazi yake ni kuwafundisha akina mama kilimo bora na kupata mapato zaidi kwa kufanya biashara ndogo inayotegemea kilimo. Alisema kuwa, tekinolojia anayojifunza hapa China inafaa sana kwa kilimo cha huko nyumbani kwake, hivyo baada ya kurudi nchini Kenya, atawafundisha akina mama kuendesha miradi kadhaa ya kutumia tekinolojia ya chakula ya China. Akisema: