Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-14 17:54:58    
Mkutano wa 13 wa Umoja wa Asia ya Kusini umepata mafanikio

cri

Mkutano wa 13 wa viongozi wa serikali wa Umoja wa Asia ya Kusini, ambao ulifanyika kwa siku 2, ulifungwa tarehe 13 huko Dhaka, mji mkuu wa Bangladeshi. Mkutano huo umepata mafanikio makubwa.

"Azimio la Dhaka" lenye vifungu 53 lililopitishwa kwenye mkutano huo linaeleza msimamo wa nchi za Asia ya Kusini kuhusu ushirikiano wa kikanda, kutokomeza umaskini, maendeleo ya uchumi mapambano dhidi ya ugaidi na kuimarisha ushirikiano wa kisiasa. Azimio hilo linasema kuwa viongozi walioshiriki kwenye mkutano wanaona kuwa umaskini ni changamoto kubwa inayoikabili sehemu ya Asia ya Kusini, na kutangaza kuwa kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2015, itakuwa ni miaka 10 ya kupunguza umaskini ya Umoja wa Asia ya Kusini, azimio pia linazitaka nchi zote za umoja huo kuhusisha mpango wa maendeleo ya nchi zao na lengo la kutokomeza umaskini la Umoja wa Asia. Mkutano huo umeamua kuanzisha shirika la utoaji msaada la kutokomeza umaskini, ili kulifanya shirika hilo litoe huduma kama shirika la utaoji msaada kwa maendeleo ya nchi za umoja huo katika ujenzi wa jamii, miundo mbinu na maendeleo ya uchumi. Mkutano huo pia umeamua kuitisha mkutano wa mawaziri wa fedha wa umoja huo kabla ya mwezi Desemba nchini Pakistan, ili kujadili kuanzishwa kwa shirika la utoaji msaada kwa ajili ya kutokomeza umaskini la umoja huo.

Licha ya kutokomeza hali ya umaskini, kuhimiza utandawazi wa uchumi wa kikanda pia ni moja ya mambo makubwa ya umoja huo katika miaka 10 ijayo."Azimio la Dhaka" linazitaka nchi wanachama zimalize majadiliano kuhusu suala la eneo la biashara huria la umoja huo na kutunga utaratibu husika kabla ya mwishoni mwa mwaka huu, ili kuhakikisha kuwa mkataba wa biashara huria wa Umoja wa Asia ya Kusini unafanya kazi kuanzia tarehe 1 Januari mwaka 2006. Azimio linazitaka nchi wanachama ziendelee kuimarisha mchakato wa utandawazi wa uchumi zianzishe biashara ya huduma, kupanua uwekezaji wa vitega uchumi, kuondoa ushuru wa forodha na vikwazo vya kibiashara miongoni mwa nchi wanachama za umoja huo, ili kutimiza lengo la kuanzishwa kwa eneo la biashara huria la Asia ya Kusini katika mwaka 2010 na kufanya maandalizi kwa ajili ya kuanzishwa kwa umoja wa uchumi wa Asia ya Kusini katika mwaka 2020. Wakati wa mkutano huo nchi wanachama wa umoja huo zilisaini mikataba 3 kuhusu kuimarisha ushirikiano wa forodha, kuanzisha baraza la hukumu la Umoja wa Asia ya Kusini na kuepusha utozaji ushuru mara mbili, na kuamua kufikia makubaliano mapema iwezekanavyo kuhusu masuala mengine, kuondoa ushuru wa forodha na vikwazo vya kibiashara kati ya nchi wanachama za umoja huo. Ili kuhimiza maingiliano ya watu na shughuli za kiuchumi za umoja huo, mkutano umeamua kulegeza masharti ya utoaji visa na kufanya watu wengi zaidi wakiwemo waandishi wa habari waweze kuingia na kutoka kwa urahisi zaidi katika nchi za Umoja wa Asia ya Kusini.

Aidha mkutano huo umeamua kukubali Afghanistan kuwa nchi mwanachama rasmi wa umoja huo na kuzipa China na Japan hadhi za wachunguzi. Baada ya kukamilisha shughuli za kujiunga, Afghanistan itakuwa nchi mwanachama rasmi wa Umoja wa Asia ya Kusini. Baraza la mawaziri la Umoja wa Asia ya Kusini litaitisha mkutano mwezi Julai mwaka 2006 kujadili kihalisi hadhi ya wachunguzi wa umoja huo.

Katika kipindi cha mkutano huo viongozi wa nchi mbili za India na Pakistan walionesha uvumilivu mkubwa kuhusu suala la Kashimir. Waziri mkuu wa India Bw. Manmohan Singh na waziri mkuu Shaukat Aziz walikuwa na mazungumzo mara mbili, moja kati ya hayo yalifanyika kwa nusu saa, viongozi hao wawili wamefurahia maendeleo ya mazungumzo ya amani kati ya nchi hizo mbili. Baada ya mazungumzo yao Bw. Aziz alisema kuwa, pande mbili zilifanya mazungumzo katika hali ya uaminifu na yenye mafanikio, aliongeza kuwa mazungumzo yao yalihusu masuala yote yanayohusu pande hizo mbili likiwemo suala la Kashimir. Alisema kuwa uhusiano kati ya India na Pakistan ni kama kujenga jengo moja kubwa, ujenzi wake unatakiwa kufanyika hatua kwa hatua, alisema kuwa mazungumzo ya viongozi wa nchi hizo mbili yalikuwa moja ya hatua hizo.