Hivi sasa Bara la Asia limekuwa sehemu ya matumizi makubwa ya mafuta duniani, wastani wa ongezeko la matumizi ya mafuta ya kila siku umezidi ule wa dunia nzima. Namna ya kuhakikisha nishati zinatolewa kwa miaka mfululizo katika hali yenye utulivu na usalama inafuatiliwa na nchi mbalimbali za sehemu hiyo. Na kwenye mkutano wa kwanza wa Baraza la uchumi wa Ulaya na Asia uliofanyika hivi karibuni huko Xian, China, nchi mbalimbali husika zimefikia maoni ya pamoja kuhusu suala hilo.
Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kuanzishwa kwa ushirikiano wa nishati kwenye sehemu za Ulaya na Asia, nchi mbalimbali za sehemu hizo zinadai siku hadi siku kuanzishwa kwa utaratibu wenye ufanisi wa ushirikiano wa nishati katika sehemu hiyo. Naibu waziri wa mafuta wa Iran Bwana Hosseinian ameona kuwa, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kikanda wa nishati ni njia yenye ufanisi ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya nishati. Akisema:
Hivi leo tunakabiliwa na changamoto mbalimbali za nishati, kama tukifanya ushirikiano wa kimataifa na kikanda na kufikia maoni ya pamoja, ndipo tutakapoweza kufanikiwa katika kukabiliana na changamoto hizo.
Sehemu za Ulaya na Asia zina maliasili nyingi na soko kubwa la matumizi. Hivi sasa nchi mbalimbali za Ulaya na Asia zinafanya juhudi kutafuta ushirikiano wa nishati wa ngazi mbalimbali na kwa njia mbalimbali. Katibu mkuu wa Baraza la Boao la Asia Bwana Long Yongtu alisema:
Mashirika ya nchi mbalimbali yakishiriki kwa juhudi kwenye ushirikiano wa nishati wa sehemu hizo, hii itakuwa hatua halisi muhimu. Hivyo tunapaswa kuharakisha zaidi ushirikiano kati ya mashirika ya sehemu hizo; aidha serikali za nchi mbalimbali za sehemu hizo pia zinatakiwa kutoa uungaji mkono.
Kundi la mafuta na kemikali la China ni kampuni kubwa ya nishati na kemikali katika sehemu ya Asia, kampuni hiyo imeanzisha miradi mbalimbali ya ushirikiano wa nishati katika sehemu za Ulaya na Asia. Naibu meneja mkuu wa kundi hilo Bwana Mu Shuling alisema kuwa, Kundi la mafuta na kemikali la China linapenda kuendelea kufanya ushirikiano huo katika sehemu za Ulaya na Asia. Alisema:
Kundi la mafuta na kemikali la China lina nguvu bora za kinadharia na kiteknolojia katika sekta ya uchimbaji na uendelezaji wa mafuta, tunapenda kutafuta ushirikiano mpya na nchi mbalimbali chini ya kanuni za kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja.
Uzbekistan ni nchi muhimu ya uzalishaji na uuzaji wa nishati, meneja mkuu wa kampuni ya mafuta na gesi ya nchi hiyo Bwana Majitov ana matumaini ya furaha juu ya mustakbali wa ushirikiano wa nishati kati ya mashirika ya nchi mbalimbali. Alisema, anatumai kuwa ushirikiano huo kati ya nchi mbalimbali ya sehemu za daraja la bara la Ulaya na Asia utahimiza uzalishaji na uuzaji wa bidhaa za mafuta na gesi za Uzbekistan.
Mtaalamu wa nishati wa China Bwana Jiang Runyu anaona kuwa nchi za sehemu hizo zinaweza kusaidiana katika sekta ya nishati, hivyo ushirikiano kati ya nchi za sehemu hizo utaweza kuanzishwa na kupanuliwa. Amezitaka nchi mbalimbali zinazohusika ziharakishe ushirikiano, kuanzisha utaratibu wa lazima wa ushirikiano ili kuanzisha ushirikiano wa kunufaishana.
|