Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-15 10:13:18    
Ma Yun, bingwa wa Internet

cri

Bw. Ma Yun

Internet imepata maendeleo makubwa tangu ilipoanzishwa nchini China katikati ya miaka ya 90 ya karne iliyopita, na watu wengi mashuhuri walijitokeza ghafla kutokana na kufanikiwa katika kuanzisha tovuti kwenye mtandao huo. Katika kipindi cha nchi yetu cha leo, nitawafahamisha, bingwa mwingine wa sekta ya mtandao nchini China, ambaye hivi sasa anaendesha mtandao wa kwanza kwa ukubwa duniani wa shughuli za biashara za elektroniki unaojulikana kwa jina la Alibaba. Miaka 9 iliyopita Bw. Ma Yun alikuwa hafahamiki, lakini baada ya miaka 9 jina lake linafahamika kwa watu wengi.

Miaka 9 iliyopita, Bw. Ma Yun alilazimika kutafuta wateja wake kutoka kampuni moja hadi nyingi, kwani watu wa China walikuwa bado hawajafahamu Internet ni nini, wakati ule watu wengi walidhani kuwa Bw. Ma Yun ni mdanganyifu. Baada ya miaka 9, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mwezi Agosti mwaka huu hapa Beijing, Bw. Ma Yun alitangaza kuwa kampuni ya Alibaba anayoingoza imenunua mali yote ya tawi la Kampuni ya Yahoo nchini China. Aidha, Kampuni ya Yahoo imewekeza dola za kimarekani bilioni moja. Huu ni ununuzi mkubwa kabisa katika historia ya Internet. Alipozungumzia ununuzi huo Bw. Ma Yun alisema kwa majivuno,

"Mara tu baada ya kushuka kutoka ndege nchini Marekani tarehe 26 mwezi Julai mwaka 2005, niliwaambia mawakili kuwa kumbuka, hii ni Alibaba kununua tawi la Yahoo nchini China, siyo kampuni ya ubia au Kampuni ya Yahoo kununua Alibaba. Endapo kukosa msingi huo, basi hakuna haja ya kuwa na mazungumzo tena."

Ununuzi huo wa Alibaba, si kama tu umepata uwekezaji wa dola bilioni 1, bali umeleta zawadi nyingi zikiwa ni pamoja na haki ya matumizi yasiyo na kikomo cha muda ya tovuti, utafutaji wa habari, upelekaji wa ujumbe, matangazo ya biashara na nembo ya Yahoo nchini China. Walakini gharama inayogharamiwa na Kampuni ya Alibaba ni 40% ya hisa zake, 35% ya haki ya upigaji kura na kiti kimoja kwenye bodi ya wakurugenzi.

Kampuni ya Yahoo ni moja ya kampuni kubwa inayoongoza katika shughuli za mawasiliano ya kompyuta, sasa imenunua kampuni 25 duniani na haijawahi kuuza mali yake. Je Ma Yun alifanya nini hadi kufanya kampuni ya Yahoo kuuza tawi lake nchini China?

"Mimi sina kichwa kingine cha ziada kuliko watu, mimi ni mwembamba na sina sura nzuri, lakini ninaona kuwa akili ya mwanaume ni kinyume cha uzuri wa sura yake."

Hayo ni maneno anayosema Bw. Ma Yun mara kwa mara. Watu waliowahi kumwona Ma Yun wanajua kuwa anaonekana kama mtu wa kawaida kabisa na ni vigumu kwa watu kumhusisha na bingwa wa sekta ya Internet. Ma Yun alizaliwa mwaka 1964 katika mji wa Hangzhou, mkoa wa Zhejiang ulioko sehemu ya mashariki ya China. Mara ya kwanza aliposhiriki kwenye mtihani mkuu wa kuingia chuo kikuu alipata 21 kwenye somo la hisabati, na alishiriki mtihani mkuu huo kwa miaka mitatu, hatimaye alichukuliwa na shule moja ya Kiingereza. Baada ya kuhitimu masomo Ma Yun alikuwa mwalimu katika chuo cha elektroniki cha Hangzhou. Ma Yun hana elimu ya teknolojia wala mali nyingi, sababu ya kufanikiwa kwa Ma Yun ni kujiamini na moyo thabiti wa kuchapa kazi.

Mwaka 1996, Ma Yun alitambulisha tovuti yake kutoka kwenye kampuni moja hadi kampuni nyingine. Kutokana na kukosa wateja, muda si mrefu aliacha shughuli hizo na kuondoka Beijing kwa masikitiko makubwa. Mwaka 1999 Ma Yun alianzisha kampuni ya Alibaba baada ya kurejea Hangzhou, ambapo shughuli za mawasiliano ya Internet zilikuwa na maendeleo makubwa. Lakini hali hiyo nzuri haikudumu kwa muda mrefu, uchumi wa mtandao wa mawasiliano ya kompyuta ulididimia mwaka 2000, watu wengi wa kampuni yake waliondoka, na baadhi ya matawi ya kampuni ya Alibaba yaliyoko nchini China na nchini Marekani yalifungwa. Lakini Ma Yun alikuwa mkaidi na alishikilia hadi mwisho.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya shughuli za biashara za elektroniki ya 6688 ya Beijing Bw. Wang Juntao alisema, katika kipindi hicho cha kuzorota kwa kampuni, ambacho watu wengi walisema ni "Majira ya baridi", hakikuwa jambo baya kwa Mayun. Alisema,

"Majira ya baridi ya Internet, kusema kwa usahihi ni majira ya baridi ya wawekezaji wa Internet, na ni majira ya baridi ya vyombo vya upashanaji habari vya Internet, endapo kipindi hicho kingekuwa kirefu zaidi, pengine ni jambo zuri kwa kampuni ya Alibaba, ambayo imekuwa na nguvu muhimu ya ushindani. Kwani mazingira ya sekta inayojitegemea hayakuwa baridi sasa, idadi ya watu waliotumia Internet na idadi ya viwanda na kampuni zilizoanzisha shughuli za biashara za elektroniki nchini China ziliongezeka kwa haraka katika miaka ile."

Mtindo ya njia ya kampuni ya shughuli za Internet ya Alibaba iliyoanzishwa na Ma Yun ilikuwa ya BTOB, yaani kuvitia viwanda na kampuni ndogo na za wastani kufanya shughuli za biashara moja kwa moja kwa kutumia Internet, mtindo wa aina hiyo ni njia yenye shida kubwa na kuchosha zaidi katika sekta ya Internet, hata katika nchi zilizoendelea katika sekta ya Internet, ikiwemo Marekani, ni kampuni chache tu zilizopata mafanikio. Katika wakati wa shida sana ambapo Ma Yun alikaribia kushindwa, mkurugenzi mkuu wa Soft Bank Bw. Sun Zhengyi alimpa msaada.

Mwaka 2001, Alibaba ilipata uwekezaji vitega-uchumi vyenye hatari wenye dola za kimarekani milioni 20 ambazo zilimsaidia sana Ma Yun kupita majira ya baridi ya Internet. Mwaka 2003, ingawa China ilikumbwa ghafla na ugonjwa wa SAS, ofisi za kampuni ya Alibaba zilitengwa na wengine, lakini shughuli za kampuni hiyo ziliendelea kama kawaida na shughuli za biashara za elektroniki zilifanya kazi nyingi muhimu katika kipindi cha maambukizi ya ugonjwa wa SARS, Bw. Ma Yun alibadilisha changamoto hiyo kuwa nafasi nzuri, ambapo shughuli za kampuni ya Alibaba ziliongezeka mara 6. Katika mwaka huo, pato la kampuni ya Alibaba lilifikia Yuan za renminbi milioni 1 kwa siku; Mwaka 2004, kampuni ya Alibaba ilipata maendeleo ya kushangaza, ambapo ilipata wastani wa faida ya Yuan milioni 1 kwa siku.

Shughuli za sekta ya biashara ya miaka mingi hazikumfanya Ma Yun kuwa mwerevu, na mafanikio ya shughuli zake hayakumfanya awe na majivuno, alipozungumzia imani na uthabiti wa tabia ya Bw. Ma Yun, mtaalamu wa raslimali ya nguvukazi Bw. Chen Anzhi alisema kuwa, hakuna mtu asiyeweza kushindwa, hata yeye siyo mtu wa kawaida, na kama mtu aliyesimuliwa katika hadithi, binadamu anapaswa kujikosoa katika hali ya kujiamini, nafikiri kuwa mtu akiweza kufanya hivyo hatashindwa kwa urahisi. Mimi ninaheshimu sana moyo wa Bw. Ma Yun wa kujiamini, kujiamini siyo majivuno.

Bw. Ma Yun anaendelea kufuata njia anayochagua bila kujali jinsi watu wanavyomwona. Machoni pa Ma Yun shughuli za biashara za elektroniki ni mgodi wa dhahabu ambao haujavumbuliwa kabisa. Bw. Ma Yun amepata faida kubwa kutokana na shughuli hizo ambazo watu walidhani shughuli za Internet ni zenye shida na za kuchosha. Sababu ya kampuni ya Yahoo kukubali kununua kwa bei kubwa hisa za kampuni ya Alibaba ni kutokana na imani yake kuhusu mustakabali wa soko la Internet nchini China ambalo linakua kwa haraka.

Idhaa ya kiswahili 2005-11-15