Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-16 16:35:06    
Mkutano wa jumuiya ya upashanaji habari wa Tunisia wafuatilia suala la usimamiaji wa internet

cri

Mkutano wa jumuiya ya upashanaji habari wa Tunisia duniani unatazamiwa kufanyika kuanzia tarehe 16 hadi tarehe 18 nchini Tunisia. Mkutano huo utakaoendeshwa na jumuiya ya upashanaji habari ya kimataifa utakuwa mkutano wa kipindi cha pili baada ya kufanyika kwa mkutano huo mwezi Desemba mwaka 2003 mjini Geneva. Mkutano huo utajadili suala la namna ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kukuza huduma za upashanaji habari, lakini vyombo vya habari vinakadiria kuwa majadiliano ya mkutano huo bado yatazingatia suala la usimamiaji wa internet.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan, viongozi wa jumuiya za kimataifa, wakuu wa nchi zaidi ya 30 na wajumbe wengine elfu kumi watahudhuria mkutano huo. Naibu waziri mkuu wa China Bw. Huang Ju pia atahudhuria mkutano huo kutokana na mialiko ya serikali ya mwenyeji Tunisia na katibu mkuu Kofi Annan.

Mawasiliano ya internet yameendelezwa kwa kasi na kuleta nguvu kubwa kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi mbalimbali, lakini nchi zinazoendelea zina upungufu mkubwa katika matumizi na teknolojia ya upashanaji wa habari zikilinganishwa na nchi zilizoendelea. Baraza la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD hivi karibuni lilitoa ripoti likiainisha kuwa, ingawa idadi ya watu wanaotumia internet wa nchi zinazoendelea inaongezeka kwa kasi, lakini kiasi cha kutumia internet cha nchi hizo ni kidogo sana ikilinganishwa na nchi zilizoendelea. Asilimia 89 ya kampuni za nchi za Umoja wa Ulaya zinatumia internet, lakini ni asilimia 3.1 tu ya watu wa Afrika wanaotumia internet.

Nchi zinazoendelea hazina hali nzuri katika raslimali za internet ya kimataifa, hali hiyo inazihimiza zibadili mfumo uliopo sasa wa internet kujiunga na mambo ya tovuti duniani kwa nguvu za serikali. Matakwa hayo yanahitilafiana na mfumo uliopo wa mtandao wa internet. Hivi sasa mtandao wa internet unasimamiwa na kampuni binafsi chini ya wizara ya biashara ya Marekani. Kampuni hiyo iitwayo ICANN imehimiza maendeleo ya haraka ya mtandao wa internet na kuifanya iwe njia kuu ya biashara na upashanaji habari wa kimataifa tangu mwaka 1998 ilipoanzishwa, lakini utaratibu huo wa usimamiaji wa upande mmoja una upungufu wake.

Kwanza, katika siasa, kampuni ya ICANN inawajibika tu na serikali ya Marekani na kuiwezesha Marekani kupooza mtandao wa internet katika nchi nyingi na kuzifanya nchi hizo kuwa na wasiwasi katika siasa. Pili, katika uchumi, utaratibu uliopo sasa wa kufunga hesabu kwa tovuti sio wa usawa kwa nchi nyingi zinazoendelea. Ukweli ni kuwa nchi zinazoendelea zinatoa msaada wa kifedha kwa mtandao wa internet wa nchi zilizoendelea. Tatu, katika utamaduni na usalama wa teknolojia, nchi zilizoendelea kwa kutumia hali yao bora zinaathiri utamaduni asili na maadili ya kijamii ya nchi zinazoendelea, ambapo nchi zinazoendelea zinashindwa kupambana na hali hiyo.

Upungufu uliopo katika utaratibu wa usimamiaji wa mtandao wa internet wa kimataifa unafuatiliwa ipasavyo na jumuiya ya kimataifa. Nchi mbalimbali zinaelewa kuwa inapaswa kuimarisha ushirikiano na kujadili kwa makini suala hilo kubwa linalohusika na maendeleo ya siku za usoni ya binadamu ndani ya mpango wa Umoja wa Mataifa.

Idhaa ya kiswahili 2005-11-16