Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-16 19:53:42    
Mabadiliko ya hewa ya dunia yatadhuru afya ya binadamu

cri

Taarifa ya uchunguzi mpya iliyotolewa na wanasayansi wa Marekani tarehe 1 inakadiria kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ya dunia yatadhuru sana afya za binadamu, kuharibu mfumo wa mazingira ya viumbe na kusababisha hasara kubwa ya kiuchumi kwa binadamu.

Wanasayansi wa kituo cha utafiti wa uhusiano wa afya na mazingira ya dunia cha kitivo cha udakatari cha chuo kikuu cha Hafo nchini Marekani wamesema kuwa, mabadiliko ya hali ya hewa ya dunia yataleta hasara kubwa kuliko ilivyokadiriwa hapo awali, kwani mabadiliko ya hali ya hewa yataleta mfululizo wa uharibifu.

Utafiti huo unaungwa mkono na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa na kampuni za bima nchini Uswisi. Wanasayansi walisema kuwa hali ya hewa kubadilika kuwa joto na kuongezeka kwa siku zenye hali ya hewa mbaya kabisa inafaa sana kwa virusi kuzaliana kwa urahisi, ambapo ugonjwa wa malaria, ugonjwa wa Lyme, Homa ya Nile ya magharibi na ugonjwa wa pumu utaleta madhara makubwa zaidi kwa binadamu.

Kwa mfano, virusi vya Burgdorfer vya ugonjwa wa Lyme vinaambukizwa na aina moja ya kupe. Pamoja na hali ya hewa ya dunia kubadilika kuwa joto, maeneo yanayofaa kuzaliana kwa kupe wa aina hiyo yataongezeka kwa zaidi ya mara dufu ifikapo mwaka 2080, hivyo ugonjwa wa Lyme utawasumbua sana binadamu. Mbu wa kuambukiza ugonjwa wa malaria na homa ya Nile ya magharibi wanazaliana kwa haraka zaidi katika hali ya hewa ya joto.

Mfano mwingine ni kuwa kubadilika kuwa joto kwa hali ya hewa ya dunia kusababisha ongezeko la hewa ya carbon dioxide ambayo itahimiza kukua kwa aina ya majani ya ragweed, lakini unga wa maua ya majani ya ragweed ni kitu kimoja kinachosababisha ugonjwa wa pumu, tena hali ya hewa ya dunia kubadilika kuwa joto inasababisha mara kwa mara kimbunga kikubwa kinachopeperusha vumbi na mchanga, ambavyo vinaleta matatizo ya watu kushindwa kupumua vizuri.

Wanasayansi wanaona kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ya dunia pia yataharibu mfumo wa kimaumbile wa misitu, mashamba na ardhi oevu, ambapo afya za binadamu zitatishiwa vibaya zaidi. Hasara zote hizo zitakuwa mzigo mzito sana kwa jamii ya binadamu.

Mtaalamu anayeongoza utafiti huo Bw. Paulo Apostan alisema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni sawa na maafa mengine ya kimaumbile ambayo yana uhusiano na maafa yanayoikumba jamii ya binadamu, ni sawa kabisa na kimbunga cha Katrina ambayo si kama tu kilisababisha moja kwa moja vifo na hasara ya mali kwa binadamu, bali pia kilileta uchafuzi kwa mazingira ya kimaumbile na kuwafanya watu kutokuwa na mahali pa kujisetiri pamoja na matokeo mengi mabaya yaliyohusiana nacho.

Mkurugenzi wa mradi wa mazingira wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa Bw. Chars Maicnir alisema kuwa, nchi za viwanda zina mfumo kamili wa matibabu, mambo ya afya, hifadhi ya mazingira ya kimaumbile na bima, hivyo zina uwezo mkubwa wa kukabiliana hasara kubwa ya uchumi na jamii zinazosababishwa na hali ya hewa ya dunia kubadilika kuwa joto, hivyo sehemu kubwa sana ya hasara hizo zitabebeshwa nchi zinazoendelea.

Katika taarifa hiyo wanasayansi walitoa wito wa kutaka viwanda na kampuni hususan kampuni kubwa za nchi zilizoendelea zifuate njia ya maendeleo endelevu, kuharakisha kubadilisha wazo la zamani kuhusu matumizi ya nishati za mafuta ya petroli, na badala yake kutumia nishati za upepo, mwangaza wa jua, hewa ya hydrogen au kutumia nishati ya nyukilia ili kupunguza utoaji wa hewa inayosababisha hali ya hewa kubadilika kuwa joto.