Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-16 19:56:22    
China yathibitisha malengo ya maendeleo ya elimu ya wakulima wakati wa mpango wa 11 wa miaka mitano

cri

Naibu waziri wa kilimo wa China Bwana Zhang Baowen tarehe 15 mwezi Novemba alisema kuwa, wakati wa utekelezaji wa mpango wa 11 wa miaka mitano ya maendeleo ya uchumi na jamii ya China, China itachukua hatua mbalimbali za kutoa mafunzo ya kisayansi na kiteknolojia ili kuandaa aina mpya ya wakulima, na kuwawezesha wakulima milioni moja kupata elimu ya mafunzo ya kazi za kiufundi kwenye shule za sekondari za juu, ambapo wakulima wengi watakuwa wakulima wa aina mpya wenye sifa nzuri ya elimu, ustadi mzuri wa kiteknolojia na uwezo mkubwa wa uendeshaji shughuli, na kutokana na juhudi hizo kupunguza shinikizo kubwa la idadi ya watu vijijini na kuongeza nguvukazi bora ya watu wenye ujuzi vijijini.

Bwana Zhang Baowen aliyasema hayo kwenye mkutano kuhusu kuandaa aina mpya ya wakulima wa kuhudumia vijiji vipya. Alisema kuwa, katika wakati wa kutekeleza mpango wa 11 wa miaka mitano, China itaweka mkazo katika kuwaandaa wakulima wa aina mpya, kufanya juhudi kubwa za kuanzisha kazi ya kutoa mafunzo ya kisayansi na kiteknolojia kwa wakulima. Ili kuendelea kutoa mafunzo ya kazi za kiufundi kwa wakulima ili wapate vitambulisho rasmi, China itajitahidi kumwezesha mmoja kati ya wakulima wa familia 8 vijijini aweze kushiriki kwenye mafunzo ya kazi za kiufundi; kufanya juhudi kubwa za kutoa mafunzo ya kisayansi na kiteknolojia kwa wakulima ili wawe wakulima wa aina mpya, na ifikapo mwaka 2010, kuwawezesha wakulima wenye ujuzi wa kisayansi na kiteknolojia waongezeke kwa milioni 8 kwenye msingi wa milioni 2.8 ya mwaka 2003; kuanzisha kwa wakati mwafaka mradi wa kuandaaa aina mpya ya wakulima wanaoweza kuanzisha shughuli mbalimbali, ifikapo mwaka 2010 China itajitahidi kuwaandaa waendeshaji wa mashamba makubwa na wanakampuni wakulima wapatao laki moja watakaoshughulikia kazi maalum ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, kujitahidi kuiwezesha kila tarafa au kila wilaya iwe na waendeshaji wa mashamba makubwa na wanakampuni wakulima wawili au watatu. China itafanya juhudi kutekeleza miradi ya utoaji mafunzo wa mpango wa muda mrefu kuhusu kazi za kilimo. Kutumia mbinu za kisasa za elimu kama vile elimu kwa kupitia njia ya radio, televisheni, mtandao wa internet, satlaiti au video na disc kueneza ufundi wa kilimo wa kisasa wenye matumizi halisi pamoja na habari kuhusu namna ya kujiendeleza ili wakulima wengi wajue kwa wakati habari mbalimbali zinazowahusu.

Aidha China itaweka mkazo katika kuwaandaa wakulima wenye ujuzi wa kiufundi, na kusukuma mbele mafunzo ya kazi ya kiufundi ili wakulima walio ziada ya nguvu kazi vijijini waweze kupata ajira mijini. Kuanzia mwaka 2004, wizara ya kilimo na wizara nyingine za China zimeshirikiana kutekeleza mradi wa kuhamisha nguvukazi vijijini, katika siku zijazo, kazi hiyo itatekelezwa kwa juhudi kubwa zaidi, China itatenga fedha nyingi zaidi kuunga mkono utekelezaji wa mradi huo, kupanua mafunzo, kurekebisha mambo ya utekelezaji na kuinua sifa ya utoaji mafunzo.

Zaidi ya hayo, China itaweka mkazo katika kuwaandaa watu wenye ujuzi watakaoweza kusaidia kazi vijijini. Wizara ya kilimo ya China imeamua kutumia miaka 10 kuanzia sasa, kutegemea shule za vijijini na shule za sekondari za juu za kazi za kiufundi za kilimo kwa kutekeleza mpango wa kuwaandaa wakulima milioni moja, ili wawe wanafunzi watakaohitimu shule za sekondari za juu za kazi za kiufundi za kilimo, ambao watakuwa mafundi wa kupanda mimea, kufuga mifugo na kutengeneza mazao ya kilimo, ama watu wenye uwezo wa kuendesha shughuli mbalimbali vijijini na mafundi wa kisayansi na kiteknolojia vijijini.

Bwana Zhang Baowen pia alisema kuwa, wakati wa utekelezaji wa mpango wa 11 wa miaka mitano wa maendeleo ya uchumi na jamii ya China, shule za matangazo na televisheni za kilimo kote nchini China zitaanzisha semina kuhusu mafunzo ya ufundi wenye matumizi halisi katika kazi za kilimo, ambapo wakulima wapatao milioni 60 watashiriki kwenye mafunzo hayo. Kwa kupitia hayo yote, kuwawezesha wakulima wengi wapate ujuzi mpya, mitizamo mipya, kupata teknolojia mpya na kuwa na mienendo mipya ili kujenga vijiji vya aina mpya.