Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-16 21:52:41    
Mapishi ya kupika samaki ya tuna pamoja na vitunguu saumu

cri

Mahitaji

Samaki ya tuna moja, kiasi kidogo cha vitunguu saumu, vitunguu maji, tangawizi, wanga wa pilipili manga, maji, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, mchuzi wa soya vijiko vitatu, sukari kijiko kimoja, siki kijiko kimoja, chumvi kijiko 1/4,.

Njia

1. osha samaki na ondoa gamba lake na matumbo, osha tena na umkaushe.

2. pasha moto na tia mafuta kwenye sufuria, tia vitunguu maji na tangawizi ndani ya sufuria hadi vibadilike kuwa rangi ya hudhurungi kisha pakua. Tia vitunguu saumu ndani ya sufuria vikaange kwa moto kidogo halafu vipakue.

3? Washa moto, tia samaki ndani ya sufuria ikaange kwa pande mbili, tia mvinyo wa kupikia, mchuzi wa soya, sukari, siki, chumvi, wanga wa pilipili manga, mimina maji, baada ya kuchemka, tia vitunguu saumu, punguza moto kidogo na endelea kuchemsha kwa dakika 10, ndani ya dakika hizo 10, unapaswa kumgeuzageuza samaki aive pande zote. Mimina maji ya wanga, kisha pakua.