Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-17 18:09:01    
Rais Hu Jintao alihutubia bunge la Korea ya kusini

cri

Rais Hu Jintao wa China tarehe 17 ametoa hotuba kwenye bunge la taifa la Korea ya kusini, akifahamisha msimamo wa China kuhusu uhusiano kati ya China na Korea ya kusini, hali ya Asia, na suala la nyuklia la peninsula ya Korea.

Katika hotuba yake, rais Hu Jintao alikumbusha maendeleo yaliyopatikana katika uhusiano kati ya China na Korea tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi, alisema, hivi leo uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeingia katika kipindi kizuri kabisa katika historia yake, na mustakbali wa maendeleo ya uhusiano huo ni mzuri sana.

Rais Hu Jintao anaona kuwa, maarifa ya pande tatu yamepatikana katika maendeleo ya uhusiano kati ya China na Korea ya kusini.

Nchi hizo mbili zinafuata kithabiti sera ya ujirani mwema na urafiki, kufanya juhudi za kulinda amani na utulivu wa sehemu zilizo pembezoni mwa nchi hizo mbili; kuweka mkazo katika kufanya ushirikiano halisi kwa kusukuma mbele maendeleo ya pamoja, maendeleo ya amani na ushirikiano wa kunufaishana; kushikilia moyo wa kuheshimiana, kuaminiana na kutendeana kwa usawa, na kufanya juhudi kubwa katika kuendeleza vizuri uhusiano wa muda mrefu na wa utulivu kati ya nchi hizo mbili.

Rais Hu amesema, sehemu ya Asia inakabiliwa na mabadiliko makubwa yenye utatanishi. Kutafuta amani, kuhimiza maendeleo na kufanya ushirikiano ni matumaini ya pamoja ya wananchi wa nchi mbalimbali za Asia, pia ni mustakbali wa nchi mbalimbali za Asia. Alisema:

Kutokana na kukabiliwa na hali mpya yenye fursa na changamoto, taabu na matumaini, namna ya kujenga dunia yenye masikilizano, ambapo nchi mbalimbali zinaishi kwa amani kisiasa, kuwa na usawa na kunufaishana kiuchumi, na kuwa na uaminifu na ushirikiano kiusalama, na kuingiliana na kufundishana kiutamaduni, hili ni somo kubwa linalozikabili serikali za nchi mbalimbali za Asia na wananchi wao. China na Korea ya kusini zinapaswa kufanya juhudi kwa ajili ya amani na maendeleo ya Asia.

Kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea, rais Hu amesema:

China ina msimamo wazi wa siku zote kuhusu suala hilo. Tunaunga mkono mambo yoyote yanayosaidia kulinda amani na utulivu wa peninsula ya Korea. Tunapendekeza kuifanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na nyuklia, kufanya mazungumzo kwa kutatua ufuatiliaji wa pande mbalimbali, na China imefanya juhudi thabiti ili kufanikisha malengo hayo.

Rais Hu ameainisha kuwa, China siku zote inaona kuwa, suala la peninsula la Korea hatimaye linapaswa kutatuliwa na Korea ya kaskazini na Korea ya kusini katika mazungumzo na mashauriano kati yao. China itafanya kama ilivyofanya siku zote zilizopita, itaziunga mkono Korea ya kaskazini na Korea ya kusini ziboreshe uhusiano kati yao baada ya kufanya mazungumzo, na kujenga uhusiano wa kuaminiana ili hatimaye zitimize muungano wa amani na wa hiari. Rais Hu amesema China inapenda kushirikiana na Korea ya kusini katika kufanya juhudi za kiujenzi kuhusu masuala makubwa ya amani ya utulivu wa Asia ya kaskazini mashariki na bara zima la Asia.

Kabla ya rais Hu Jintao kutoa hotuba, spika wa Korea ya kusini Bwana Kim One Ki ameeleza tena kukaribisha ziara ya rais Hu Jintao nchini Korea ya kusini.