Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-18 18:14:20    
Kuwa na mtizamo wa kufungua mlango na kutimiza ushirikiano wa kunufaishana

cri

Rais Hu Jintao wa China tarehe 17 huko Pusan alitoa hotuba kwenye mkutano wa wakuu wa viongozi wa viwanda na biashara wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya Asia APEC, ambapo alibadilishana maoni na wanakampuni na wafanyabiashara wapatao mia kadhaa kuhusu suala la ustawi wa pamoja wa dunia.

Shughuli za viwanda na biashara ni kazi muhimu ya kusukuma mbele maendeleo mazuri yenye utulivu ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara wa kimataifa. Jumuiya ya APEC ni baraza muhimu la ushirikiano huo wa sehemu ya Asia na Pasifiki. Kutokana na kanuni za kawaida, wakati wa mkutano wa APEC, huitishwa mkutano wa wakuu wa viwanda na biashara, na kuwaalika viongozi wa nchi wanachama wa APEC watoe hotuba.

Katika hotuba yake ya tarehe 17, rais Hu Jintao alibadilishana maoni na viongozi wa viwanda na biashara kuhusu ushirikiano wa kunufaishana. Alisema:

Hivi sasa maendeleo ya China yanafuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Wakati dunia inapoifuatilia China kwa mtizamo wake mpya, China pia inazingatia suala moja muhimu yaani namna ya kupitia maendeleo yake yenyewe kuendelea kuchangia kazi ya kuhimiza ustawi wa pamoja wa sehemu na dunia.

Rais Hu alisema, tokea China ianze kufanya mageuzi na kuzifungulia mlango nchi za nje, uchumi wa China unaongezeka kwa miaka mfululizo, nguvu za nchi zinaimarishwa hatua kwa hatua, na maisha ya wachina wapatao bilioni 1.3 yanaboreshwa siku hadi siku. Alisema, ukweli wa mambo unaonesha kuwa, maendeleo ya uchumi wa China si kama tu yameleta manufaa kwa wananchi wa China, bali pia yameleta nafasi nyingi za uwekezaji na soko kubwa zaidi kwa nchi mbalimbali duniani, China inakuwa nguvu kubwa ya msukumo kwa ongezeko la uchumi wa sehemu ya Asia na Pasifiki na dunia.

Lakini tungeona kuwa, ingawa mafanikio makubwa yamepatikana katika maendeleo ya uchumi wa China, lakini China bado ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani. Rais Hu alidhihirisha kuwa, China itafuata kithabiti njia ya kujiendeleza kwa amani, kufanya juhudi za kujipatia mazingira ya amani ya kimataifa ili kujiendeleza, pia kupitia maendeleo yake yenyewe kwa kuhimiza amani ya dunia. Alisema:

China itashikilia sera ya kimsingi ya kuzifungulia mlango nchi za nje, kuanzisha ushirikiano na nchi mbalimbali duniani, kuboresha mazingira ya uwekezaji, kufungua soko na kutimiza ushirikiano wa kunufaishana na nchi mbalimbali duniani. Ukweli wa mambo umeonesha kuwa, maendeleo ya China hayawezi kuweka kizuizi kwa mtu yeyote, au kutisha mtu yeyote, bali yanaweza tu kusaidia amani, utulivu na ustawi wa dunia.

Hivi leo wakati utandawazi wa uchumi duniani unapoendelea kwa kina, maendeleo ya uchumi wa dunia yanakabiliwa na taabu na matatizo mengi. Suala la nishati linahusiana moja kwa moja na ongezeko la uchumi wa dunia. Rais alisema:

Hivi sasa nchi mbalimbali duniani zinapaswa kufanya juhudi kwa pamoja, kudumisha utulivu wa soko la nishati duniani ili kuleta nishati za kutosha, zenye usalama, zenye bei chini na zisizoweza kuleta uchafuzi kwa mazingira. Wakati huo huo zinapaswa kuongeza nguvu za kuendeleza nishati na kufanya kwa kina ushirikiano katika sekta ya nishati.

Rais Hu pia ameeleza msimamo wa China kuhusu kuondoa hali isiyo ya uwiano katika biashara duniani.