Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-18 18:16:31    
Li Changchun akutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Namibia

cri

Mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bwana Li Changchun ambaye yuko Namibia kwa ziara, tarehe 17 asubuhi huko Windhoek alikutana na rais wa Namibia ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Chama cha SWAPO Bw Hifikepunye Pohamba na pia kukutana na mwenyekiti wa chama cha SWAPO Bw Sam Nujoma.

Alipokutana na Bw Pohamba, Bw Li Changchun alimpongeza kwa kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Namibia mwezi Machi mwaka huu. Bwana Li Changchun alisema mwaka huu ni mwaka wa 15 tangu Namibia ipate uhuru, pia ni mwaka wa 15 tangu China na Namibia zianzishe uhusiano wa kibalozi. Katika miaka 15 iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea vizuri, pande zote zimefanya ushirikiano wenye mafanikio katika sekta mbalimbali, na zinaelewana na kuungana mkono katika mambo ya kimataifa. Vyama viwili vya China na Namibia na uhusiano wa nchi hizo mbili umedumishwa na kuimarishwa siku hadi siku. Amesema China inathamini sana urafiki na Namibia, inapenda kufanya juhudi pamoja na Namibia katika kuendeleza kwa kina uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kutia nguvu mpya ya uhai. Bwana Li Changchun pia ameishukuru Namibia kwa uungaji mkono wake wa siku zote kwa China juu ya suala la Taiwan na masuala mengine makubwa.

Rais Pohamba alisema kuwa, Bwana Li Changchun kuongoza ujumbe wa chama cha kikomunisti cha China kuitembelea Namibia, ni jambo linaloonesha kuwa urafiki na ushirikiano kati ya Namibia na China unaimarishwa siku hadi siku, na urafiki na mshikamano kati ya wananchi wa Namibia na China unaimarishwa zaidi. Katika mapambano ya kujipatia uhuru na ukombozi wa taifa yaliyofanywa na wananchi wa Namibia, chama, serikali na wananchi wa China waliwapa misaada na uungaji mkono mkubwa, chama, serikali na wananchi wa Namibia wanawashukuru na daima hawatasahau misaada kutoka China. Tokea Namibia na China zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi hizo mbili zimeimarisha siku hadi siku maingiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali za uchumi, utamaduni, sayansi na teknolojia, na ushirikiano huo umeleta na utaendelea kuleta maslahi halisi kwa wananchi wa nchi hizo mbili. Wananchi wa Namibia wanapongeza mafanikio mapya yaliyopatikana katika kazi ya kurusha chombo chenye binadamu kwenye safari ya anga ya juu, na kuwatakia wananchi wa China wapate maendeleo mapya siku hadi siku katika ujenzi wa mambo ya ujamaa na kutimiza muungano wa taifa.

Baada ya mkutano huo, Bwana Li Changchun alihudhuria sherehe kuhusu serikali ya China kutoa mkopo wenye masharti nafuu kwa Namibia, kusaini mkataba wa hifadhi ya uwekezaji wa China na Namibia na China kuzawadia vifaa vya utamaduni kwa Namibia.

Alipokutana na Bw Sam Nujoma, Bwana Li Changchun alisema kuwa, mwenyekiti Nujoma ni rafiki wa tangu zamani kwa wananchi wa China, ambaye ametoa mchango mkubwa kwa ajili ya kuendeleza urafiki kati ya vyama viwili na nchi mbili za China na Namibia. Ujumbe wa chama cha kikomunisti cha China safari hii kuitembelea Namibia, madhumuni yake ni kuongeza uaminifu, kupanua ushirikiano na kuzidisha uhusiano, pia kubadilishana maoni kuhusu masuala yanayozihusu pande hizo mbili. Amesema China inapenda kufanya juhudi pamoja na Namibia katika kusukuma mbele maendeleo ya kina ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali.

Bwana Sam Nujoma alisema kuwa, ziara hiyo ya Bwana Li Changchun hakika itaimarisha zaidi urafiki na ushirikiano kati ya vyama hivyo viwili, nchi mbili na wananchi wa nchi mbili.