Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-18 19:07:01    
Wataalamu wa China wa chombo cha safari ya anga ya juu cha Shenzhou No.6 waliokuwa wanafanya kazi nchini Kenya

cri
Saa 9 dakika 47 ya tarehe 17, Oktoba kwa saa ya Beijing, China, Chombo cha safari ya anga ya juu cha Shenzhou No.6 kilichomaliza mizunguko 77 ya kuizunguka dunia kwenye anga ya juu, kilikuwa kinajiandaa kuanza safari ya dakika 46 ya kurejea kwenye dunia.

Mamilioni ya watu duniani walikuwa wakiangalia tukio hilo kwenye televisheni, na kutarajia safari hiyo ya kurudi kutoka kwenye anga ya juu ipate mafanikio kwa mara nyingine tena. Kikundi cha usakaji na uokoaji kilichoko mkoani Mongolia ya Ndani, China, kiliangalia kwa makini tarakimu mbalimbali kwenye vyombo vilivyokuwa mbele yao, na kazi yao ilikuwa ni kuthibitisha sehemu ya kutua kwa chombo cha Shenzhou No.6 cha safari ya anga ya juu.

Wakati huo huo, wataalamu 8 wa China waliokuwa kwenye kijiji cha pwani cha Ngomeni nchini Kenya, pia walikuwa wakishughulikia mawasiliano na upashanaji habari wa Chombo cha Shenzhou No.6. Dakika 4 baada chombo hicho kuanza safari ya kurejea kwenye dunia, katika muda wa dakika 9, habari za kitarakimu zilizohitajika katika kazi zinazohusika za safari hiyo ya chombo hicho zilikuwa zinategemea kazi za Kikundi cha upimaji na udhibiti wa Chombo cha Shenzhou No.6 kilichoko huko Malindi nchini Kenya.

Malindi ni kijiji chenye uhusiano maalum na China: katika miaka 600 iliyopita, msafiri mkubwa wa baharini wa China Zheng He aliongoza msafara mkubwa wa merikebu na kuacha kumbukumbu za ustaarabu wa China huko Malindi; safari hiyo, kutokana na hali maalum ya kijiografia, Malindi iliacha kumbukumbu pia katika historia ya China kwenye safari ya anga ya juu.

Kikundi cha upimaji na udhibiti kilichoko huko Malindi kilianzishwa mwaka 2003. Wakati huo, China ilikuwa imefanikiwa kurusha vyombo vinne visivyo na binadamu watu kwenye anga ya juu kuanzia mwaka 1999 hadi 2002, na kuanzisha vituo viwili vya upimaji na udhibiti nchini Namibia na Pakistan. Lakini majaribio yalionesha kuwa, tarakimu za vyombo vya safari za anga ya juu zilikuwa haziwezi kupatikana kwenye sehemu iliyo katikati ya vituo viwili nchini Namibia na Pakistan.

Wakati huo, Chombo cha Shenzhou No.5 kilikuwa kimeamuliwa kurushwa mwezi Oktoba, mwaka 2003. Kutokana na hali hiyo, wataalamu wa safari za anga ya juu walifanya mazungumzo na Chuo Kikuu cha Rome na Idara ya safari za anga ya juu ya Italia, kukodi baadhi ya zana za kituo cha anga ya juu kilichoanzishwa na Italia huko Malindi, na kuanzisha kwa muda mfupi sana kituo cha upimaji na udhibiti cha China huko Malindi. Ingawa kwa kawaida kuna wafanyakazi mia moja hivi kwenye vituo vya upimaji na udhibiti nchini China, lakini kituo hiki cha Malindi kina wataalamu 10 tu wakiwa ni pamoja na waatalmu 8 wa China na wawili wa Italia.

Katika safari ya mizunguko 77 ya Chombo cha Shenzhou No. 6 kuizunguka dunia kwenye anga ya juu katika muda wa saa 115 na dakika 33, mizunguko 16 ilifuatiliwa na kituo cha upimaji na udhibiti cha Malindi.

Saa 10 na dakika 47 alasiri ya tarehe 12, Oktoba, kwa saa za Beijing, yaani saa 5 na dakika 47 asubuhi kwa saa za Afrika ya Mashariki, antena ya upimaji na udhibiti iliyowekwa huko Malindi ilipokea kwa mara ya kwanza ishara kutoka kwenye Chombo cha Shenzhou No.6.

Wakati huo, tarakimu mbalimbali zikiwemo tarakimu za upimaji, hali ya mwili ya wanaanga, sauti na picha za chombo, zilipelekwa kwa kupitia satilaiti na kufika kwenye miji ya Beijing na Xi'an, China.

Lakini wataalamu waligundua kuwa, wakati Chombo cha Shenzhou No.6 kilipopita Kenya mara mbili katika siku ya kwanza baada ya kurushwa, ishara kadhaa zilizotolewa kutoka chombo hicho yalikuwa si ya kawaida, wataalamu wa Italia walioko kwenye kituo cha Malindi waliona kuwa, kosa hilo lilitokana na tatizo la Chombo cha Shenzhou No.6.

Lakini baada ya kulinganisha tarakim kati ya kituo cha Malindi na vituo vingine, wataalamu wa China walithibitisha kuwa, hali hiyo ilitokana na tatizo la zana za upimaji na udhibiti huko Malindi. Baada ya kufanya ukaguzi kwa makini, waligundua kuwa, kichwa cha waya ya umeme cha zana zilizoandaliwa na Italia kiliharibika, na kusababisha kosa hilo.

Mtaalamu wa China Bw. Yang Fangying alieleza kuwa, upimaji na udhibiti wa zana za mambo ya anga ya juu unahitaji umakini sana, na tatizo lolote la antena linaathiri moja kwa moja mawasiliano kati ya wanaanga na kituo cha udhibiti cha Beijing. Kama tatizo hilo halikugunduliwa kwa wakati linaweza kusababisha kushindwa kwa kazi ya upimaji itakayofanyika baadaye.

Msimamo wa makini na uwezo wa wataalamu hao wa China ulisifiwa na wataalamu wa Italia waliokuwepo kwenye kituo hicho.

Tarehe 17 alfajiri, wataalamu wote walioko kwenye kituo cha Malindi, Kenya, walikusanyika kuangalia Chombo cha Shenzhou No.6 kwenye televisheni.

"Chombo cha Shenzhou No.6 kimetua salama kwenye dunia!" Wakati mtangazaji alipotangaza mafanikio ya safari ya chombo hicho, wataalamu wa Italia walifungua shampeni kupongeza kwa furaha kubwa mafanikio ya wenzao wa China.

Katika nusu mwaka uliopita, kutokana na tofauti ya saa kati ya Beijing na Kenya, tangu chombo cha Shenzhou No.6 kirushwe, wataalamu wote kwenye kituo cha Malindi walifanya kazi kwa kufuata hali ya usafiri wa chombo hicho, na wataalamu 8 wa China walitiliwa shinikizo kubwa la kikazi katika nchi ya kigeni iliyoko mbali sana na kutoka nyumbani kwao China, lakini wanaona furaha na fahari kubwa kutokana na mafanikio ya Chombo cha Shenzhou No.6.