Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-21 18:05:24    
Upigaji kura wa maoni ya raia wafanyika mara ya kwanza nchini Kenya

cri

Kenya imeamua kufanya upigaji kura wa maoni ya raia kuhusu mswada wa katiba mpya tarehe 21 mwezi huu. Hii ni mara ya kwanza kwa Kenya kufanya upigaji kura huo tangu nchi hiyo ipate uhuru, na upigaji kura huo pia ni sehemu muhimu ya mchakato wa marekebisho ya katiba ya nchi hiyo, matokeo yake yatakuwa na athari kubwa kwa mfumo wa kisiasa ya nchi hiyo ya siku zijazo, hivyo upigaji kura huo unafuatiliwa na watu wa pande mbalimbali.

Ofisa wa tume ya uchaguzi ya Kenya alisema kuwa, wapigaji kura wapatao milioni 11.6 waliojiandikisha watashiriki kwenye upigaji kura huo wa maoni ya raia, ambapo wataeleza wazi kama wanakubali mswada wa katiba mpya uliotolewa na bunge la Kenya katikati ya mwezi Julai mwaka huu au la. Kama mswada huo wa katiba mpya utapitishwa, utaanza kutekelezwa kuanzia mwishoni mwa mwaka huu, na Kenya itaongeza wadhifa wa waziri mkuu, jambo hili litabadilisha hali ya hivi sasa ya nchi hiyo ya kuwepo kwa wadhifa wa rais tu, ambalo litaleta mabadiliko makubwa kwa mfumo wa kisiasa.

Habari zinasema kuwa, tume ya uchaguzi ya Kenya imewaalika wajumbe wa jumuiya za kimataifa na kikanda zikiwemo pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na kundi la wanadiplomasia wa nchi za nje walioko nchini humo kushiriki kwenye usimamizi wa upigaji kura huo. Matokeo ya upigaji kura huo yatajulikana tarehe 22 kwa saa za huko. Kabla ya upigaji kura huo kufanyika, ofisa wa tume ya uchaguzi ya Kenya alisema kuwa, bila kujali matokeo ya upigaji kura huo ni yatakavyo kuwa, wanawataka wananchi wa Kenya wataweza wayakubali, na kushirikiana kama kitu kimoja katika kufanya juhudi kwa ajili ya kulinda amani na utulivu wa taifa.

Mchakato wa marekebisho ya katiba ya Kenya umepitia miaka mingi. Katiba inayotekelezwa sasa nchini Kenya ni ile iliyotolewa mwaka 1994. Tangu Kenya itekeleze mfumo wa vyama vingi mwezi Desemba mwaka 1991, watu wa sekta mbalimbali za jamii wa Kenya wanaona kuwa katiba ya sasa ni katiba iliyotolewa katika kipindi cha utekelezaji wa mfumo wa chama kimoja, ambayo hailingani na mfumo wa vyama vingi, hivyo walitaka kurekebisha katiba hiyo. Mwezi Septemba mwaka 2002, tume ya marekebisho ya katiba ya Kenya ilitangaza mswada wa katiba mpya ambayo imewekwa vifungu kuhusu kupunguza madaraka ya rais, na kuongeza wadhifa wa waziri mkuu na manaibu wake na kadhalika, lakini katiba hiyo ilipingwa vikali na chama tawala cha wakati huo, na mchakato wa marekebisho ya katiba ya Kenya ulikwama kwa muda.

Mwezi Desemba mwaka huo, muungano wa National rainbow ulioundwa na vyama 14 vya upinzani uliushinda chama cha KANU na kushika hatamu za serikali, na Mwai Kibaki alichaguliwa kuwa rais wa tatu wa Kenya. Ili kutimiza ahadi yake ya kukamilisha marekebisho ya katiba, mwezi Aprili mwaka 2003, rais Kibaki alianzisha tena mchakato wa marekebisho ya katiba, lakini kutokana na maoni tofauti juu ya kuwekwa kwa wadhifa wa waziri mkuu, madaraka ya rais na masuala mengine kadhaa muhimu, mchakato wa marekebisho ya katiba ulikwama tena. Mwezi Julai mwaka huu, bunge la Kenya lilipitisha mswada wa katiba mpya, na kuamua kufanya upigaji kura wa maoni ya raia wote juu ya mswada huo.

Muungano wa National rainbow unaoongozwa na rais Kibaki unaunga mkono katiba mpya, lakini chama cha KANU kina maoni tofauti. Katika miezi kadhaa iliyopita, pande hizo mbili zimeanzisha shughuli kubwa za uenezi wa maoni yao tofauti. Hivi sasa bado ni vigumu kuona kuwa upande gani utashinda kwenye upigaji kura wa maoni ya raia wote, lakini bila kujali matokeo ya upigaji kura huo, upigaji kura huo hakika utaleta athari kubwa katika mchakato wa demokrasia ya Kenya.