Waziri mkuu wa Israel Sharon tarehe 21 alitangaza kujiondoa rasmi kutoka kwenye chama cha Likurd na kuanzisha chama kipya cha wajibu wa taifa. Siku hiyo bunge la Israel lilipitisha mswada wa sheria na kukubali bunge hilo livunjwe, na ufanyike uchaguzi mkuu tarehe 28 Machi mwakani kabla ya mpango uliowekwa. Wachambuzi wameainisha kuwa, hayo yote yameonesha kuwa, jukwaa la kisiasa la Israel linakabiliwa na mabadiliko makubwa.
Mwezi Agosti mwaka huu Israel ilianza kutekeleza mpango wa upande mmoja wa kuondoka kutoka ukanda wa Gaza na sehemu ya kaskazini ya Mto Jordan, baadaye hali mbaya ya ufarakanishaji na mapambano kati ya Sharon na wapinzani wa ndani ya chama cha Likurd ilitokea, ambapo habari kuhusu Sharon kuwa na nia ya kujitoa kutoka kwenye chama cha Likurd na kuanzisha chama kipya zilianza kuchapishwa mara kwa mara kwenye magazeti. Mapema mwezi huu, chama cha leba kinachoshika hatamu za kiserikali pamoja na chama cha Likurd kilimchagua mwenyekiti wake mpya, mwenyekiti huyo mpya Bwana Amir Peretz anashikilia kukitaka chama cha leba kijitoe kutoka kwenye serikali ya muungano, na kuifanya serikali ya Sharon ianguke na uchaguzi mkuu kufanyika kabla ya mpango uliowekwa. Hii imekuwa hali ya mambo isiyoweza kufutika. Bwana Sharon akikabiliwa na chaguo lake la kisiasa, baada ya kutafakari kwa makini, akapiga "chesi ya hatari" ya kuondokana na chama cha Likurd na kuanzisha chama kipya.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 21 Bwana Sharon alisema kuwa, ameamua kujitoa kutoka kwenye chama cha Likurd, sababu kuu ni kuwa yeye hataki kupoteza wakati bila sababu kutokana na mvutano wa kisiasa, asije akapoteza fursa ya kihistoria inayoletwa na utekelezaji wa mpango wa kuondoka kutoka sehemu za Palestina. Chama cha wajibu wa taifa kinachoanzishwa naye ni chama kimoja chenye uhuru ambacho kitaleta matumaini mapya ya amani kwa waisrael. Bwana Sharon alisema, ataendelea kuunga mkono mpango wa amani ya mashariki ya kati, na kufikia makubaliano ya amani na Palestina baada ya kufanya mazungumzo; amekanusha kuwa kama akishinda katika uchaguzi mkuu wa siku za usoni, ataendelea kutekeleza mpango wa upande mmoja katika kando ya magharibi ya Mto Jordan.
Bwana Sharon tarehe 21 aliendesha mkutano wa kwanza wa chama cha wajibu wa taifa. Wabunge 14 waliokuwa wa chama cha Likurd akiwemo naibu waziri mkuu Ehud Olmert wamemfuata katika chama hicho kipya na kuwa uti wa mgongo wa chama hicho. Aidha, watu mashuhuri kadha wa kadha pia watajiunga na chama cha wajibu wa taifa. Msaidizi wa Sharon alisema kuwa, chama kipya kilichoanzishwa na Sharon kitakuwa chama chenye msimamo wa katikati katika mambo ya kisiasa, kiuchumi ama sera za kijamii, na chama cha wajibu wa taifa kinatazamiwa kuwa chama kikubwa kabisa katika bunge la awamu mpya baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa siku zijazo.
Lakini Bwana Sharon alianzisha chama kipya kwa haraka, akitaka kupata ushindi katika uchaguzi mkuu bado atakabiliwa na taabu nyingi. Wachambuzi wanaona kuwa, chama hiki kipya kilichoanzishwa na Bwana Sharon kileta athari kubwa kwa mambo ya kisiasa ya Israel.
Wachambuzi wameainisha kuwa, kutokana na kuanzishwa kwa chama cha wajibu wa taifa, nguvu ya mrengo wa kulia ya chama cha Likurd imedhoofishwa, na nguvu ya mrengo wa kushoto ya chama cha leba siku hadi siku inajitoa kutoka hali ya kudidimia ya miaka kadhaa iliyopita kutokana na mageuzi anayopendekeza mwenyekiti wake mpya Bwana Peretz.
|