Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-23 19:14:08    
Katiba mpya ya Kenya yakataliwa katika upigaji kura wa maoni ya raia wote nchini humo

cri

Tume ya uchaguzi ya Kenya tarehe 22 ilitangaza kuwa, katiba mpya ya Kenya imekataliwa katika upigaji kura wa maoni ya raia wote uliofanyika tarehe 21. Wachambuzi wamedhihirisha kuwa, matokeo hayo yataleta utatanishi wa kiasi fulani kwa serikali ya Kenya inayoongozwa na rais Mwai Kibaki, lakini hayawezi kutikisa kimsingi hadhi yake ya utawala.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Kenya Bwana Samuel Kivuitu siku hiyo alitangaza kuwa, kutokana na takwimu zilizopatikana, asilimia 58 ya raia wanapinga katiba mpya, na waliopiga kura za ndio ni asilimia 42. Ingawa matokeo ya mwisho hayajatolewa, lakini katiba mpya imekataliwa katika upigaji kura huo, hali hii imeonekana. Kabla ya hapo, rais Kibaki alipotoa hotuba kwa njia ya televisheni akikiri kuwa katiba mpya imeshindwa kupitishwa, na ameahidi kuwa atafuata nia ya wananchi na kupokea matokeo hayo.

Mchakato wa marekebisho ya katiba ya Kenya umepitia miaka mingi. Katiba inayotekelezwa sasa nchini Kenya ni ile iliyotolewa mwaka 1964. Tangu Kenya ianze kutekeleza mfumo wa vyama vingi mwezi Desemba mwaka 1991, watu wa sekta mbalimbali za jamii wa Kenya wanaona kuwa katiba ya sasa ni katiba iliyotolewa katika kipindi cha utekelezaji wa mfumo wa chama kimoja, ambayo hailingani na mfumo wa vyama vingi, hivyo walitaka katiba hiyo irekebishwe. Mwezi Septemba mwaka 2002, tume ya marekebisho ya katiba ya Kenya ilitangaza mswada wa katiba mpya ambayo imewekwa vifungu kuhusu kupunguza madaraka ya rais, na kuongeza wadhifa wa waziri mkuu na manaibu wake na kadhalika, lakini katiba hiyo ilipingwa vikali na chama tawala cha wakati huo, na mchakato wa marekebisho ya katiba ya Kenya ulikwama kwa muda.

Mwezi Desemba mwaka huo, muungano wa National rainbow ulioundwa na vyama 14 vya upinzani ulikishinda chama cha KANU na kushika hatamu za serikali, na Mwai Kibaki alichaguliwa kuwa rais wa tatu wa Kenya. Ili kutimiza ahadi yake ya kukamilisha marekebisho ya katiba, mwezi April mwaka 2003, rais Kibaki alianzisha tena mchakato wa marekebisho ya katiba, lakini kutokana na maoni tofauti juu ya kuwekwa kwa wadhifa wa waziri mkuu, madaraka ya rais na masuala mengine kadhaa muhimu, mchakato wa marekebisho ya katiba ulikwama tena. Mwezi Julai mwaka huu bunge la Kenya lilipitisha mswada wa katiba mpya, na kuamua kufanya upigaji kura wa maoni ya raia wote juu ya mswada huo.

Wachambuzi wanaona kuwa, kukataliwa kwa katiba hiyo mpya, chama cha Liberal Democratic na chama cha KANU vitafanya juhudi kubwa katika kulihimiza bunge likubali mswada wake wa katiba wa "kuongeza madaraka ya waziri mkuu na kupunguza madaraka ya rais", hii itatoa shinikizo kubwa zaidi kwa serikali ya Kibaki inayojaribu kudumisha madaraka kabisa ya rais.

Wachambuzi wanaona kuwa, baada ya kukataliwa kwa katiba mpya, ingawa serikali ya Kibaki inakabiliwa na matatizo ya kuondoa ufarakanishaji wa jamii na kuimarisha mshikamano wa ndani, lakini hakuna uwezekano wa kutingishwa kimsingi kwa hadhi yake ya utawala. Sababu zake ni kuwa, rais Kibaki ana heshima kubwa, ambaye siku zote anatilia maanani kudumisha haki na mshikamano, anasifiwa na watu wa pande mbalimbali pamoja na viongozi kadhaa wa upinzani, aidha, muungano wa Rainbow bado unaongoza katika bunge la taifa, ni vigumu kwa wapinzani kumtaka rais ajiuzulu. Zaidi ya hayo, serikali ya Kibaki imechukua hatua mbalimbali za kupunguza migongano kati ya pande mbalimbali, na imepata mafanikio kwa kiasi fulani.

Hayo yote yameonesha kuwa, serikali ya Kibaki bado inadhibiti hali ya mambo, na mabadiliko makubwa hayataweza kutokea katika jukwaa la kisiasa la Kenya.