Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-23 20:20:40    
Mapishi ya vipande vya nyama ya ng'ombe pamoja na mayai

cri

Mahitaji

Mayai matatu, vipande vya nyama ya ng'ombe gramu 250, mchuzi wa soya, gramu 5, wanga gramu 15, chumvi gramu 5, M.S.G gramu 3?kiasi kidogo cha mafuta ya ufuta, pilipili manga, vipande vidogo vya vitunguu maji

Njia

1. tia vipande vya nyama ya ng'ombe ndani ya bakuli moja, mimina mchuzi wa soya, maji kidogo, tia wanga, halafu mimina mafuta kidogo kisha korogakoroga.

2. koroga mayai halafu tia M.S.G, chumvi, pilipili manga, vipande vya vitunguu maji, mafuta kisha korogakoroga.

3. Washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya nyama ya ng'ombe koroga koroga mpaka viive viweke kwenye mayai yaliyokorogwa.

4. Washa moto tena, tia vipande vya nyama ya ng'ombe ndani ya sufuria tena, koroga koroga na mimina mafuta kidogo, halafu mimina mafuta ya ufuta, korogakoroga vipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.