Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-23 20:40:25    
Familia za China zaanza kutumia taa zenye globu za kubana matumizi ya nishati

cri

globu ni moja ya vitu vinavyotumiwa na watu, lakini siku hizi globu za kubana matumizi ya nishati zinazoweza kutumika kwa muda mrefu zaidi zimekidhi mahitaji mapya. Familia nyingi nchini China zimeanza kutumia globu za aina hiyo mpya.

Kwenye soko moja la taa mjini Beijing, Bi. Xu Rong alikuwa anachagua taa kwa ajili ya kupamba nyumba yake mpya. Kuna aina nyingi za taa zinazouzwa sokoni, lakini alichagua tu taa zenye globu za kubana matumizi ya nishati. Alimwambia mwandishi wetu wa habari:

"kununua taa zenye globu za kubana matumizi ya nishati ni kwa ajili ya kuokoa nishati, pia zinaweza kupunguza gharama za matumizi ya umeme. Kwa kuwa Beijing ni mji wa matumizi na pia ni mji wenye upungufu wa nishati, hivyo naona nikiwa mkazi wa mji huu, nina jukumu la kufanya hivyo na kubana matumizi ya nishati kadri niwezavyo."

Taa zenye globu za kubana matumizi ya nishati mwanzoni zilikuwa zikiletwa kutoka nchi za nje, na zimeingia China katika miongo kadhaa iliyopita. Zamani ili kueneza matumizi ya taa za aina hiyo, serikali na mashirika husika zilifanya kazi nyingi za kuzieneza taa zenye globu hizo sokoni, lakini kutokana bei ya globu za aina hiyo ilikuwa ya ghafi sana, ikiwa ni mara 20 ya bei ya taa za kawaida. Hivyo hakuna familia nyingi zilizotumia taa za aina hiyo nyumbani. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya uchumi wa China, uwezo wa watu wa China kununua vitu umeongeza kidhahiri; na serikali ya China pia imetoa mwito wa kutunza nishati na kujenga jamii yenye kubana matumizi. Hatua hiyo imeinua mwamko wa umma kutunza nishati. Kutokana na hali hiyo, taa zenye globu za kubana matumizi ya nishati zimeanza kupendwa na watu wengi zaidi.

Mtaalamu wa Shirikisho la madini adimu la China Bw. Lu Xianli aliainisha kuwa, taa zenye globu za kubana matumizi ya nishati zilitengenezwa kwa kutumia madini adimu, kutokana na uwezo maalum wa madini hayo, taa zenye globu za aina hiyo zinaweza kubana matumizi ya umeme. Alisema

"globu za kawaida zinatoa mwanga na joto nyingi hewani, kwa hivyo kiasi kikubwa cha nishati kinabadilishwa kuwa joto. Lakini globu za kubana matumizi ya nishati zinatoa joto kidogo, ikiwa ni robo ya joto linalotolewa na globu za kawaida. Hivyo ikilinganishwa na globu za kawaida, globu hizo mpya zinaweza kuokoa nishati kwa asilimia 60 hadi 80."

Wataalamu wanakadiria kuwa, kama globu za kawaida za watt 40 zikibadilishwa kuwa globu za watt 11 za kubana matumizi ya nishati, si kama tu hazitapunguza kiwango cha mwanga, bali zinaweza kupunguza matumizi ya umeme kwa aslimia 80. aidha, globu za kubana matumizi ya nishati zinaweza kutumika kwa muda mrefu zaidi. Kwa kawaida kila globu ya aina hiyo inaweza kufanya kazi kwa saa 8000, ikiwa ni mara 8 kuliko globu za kawaida.

Ikilinganishwa na globu za kawaida, globu za kubana matumizi ya nishati zina miundo yenye utatanishi zaidi, hivyo kuna mambo kadhaa yanayotakiwa kuzingatiwa wakati wa kutumia globu za aina hiyo. Bi. Zhang Li ametumia globu za aina hiyo kwa miaka kadhaa, alisema:

"kwa mfano, usiwashe na kuzima mara kwa mara globu zilizowekwa kwenye mahali kama jiko au choo ambapo watu wanaingia na kutoka mara kwa mara. Kwa sababu globu za aina hiyo zinatumia nishati nyingi wakati wa kuwasha, ingawa kuacha globu imewaka kwa muda mrefu kutaongeza matumizi ya nishati, lakini kutokana na uwezo wake maalum, kwa jumla inaweza kubana matumizi ya nishati kwa njia hiyo."

Ili kutoa chaguo vingi zaidi kwa wanunuzi wa globu za kubana matumizi ya nishati, hivi sasa viwanda vya kutengeneza globu za aina hiyo vimeendelea kutengeneza globu za aina au mtindo mpya. Ukiinga kwenye soko la taa nchini China, hivi sasa unaweza kuona taa zenye globu za watt tofauti na zenye mtindo tofauti, na hasa zenye rangi tofauti.

Aidha, teknolojia ya utengenezaji wa globu za kubana matumizi ya nishati bado inaendelea kukamilika. Globu zenye uwezo mpya zinaendelea kutolewa. Mtaalamu wa shirikisho la madini adimu la China Bw. Lu Xianli alieleza:

"globu inayoweza kuhifadhi umeme ikiwekwa kwenye mwanga wa jua kwa dakika 5 hadi 10, itaweza kutoa mwanga kwa saa 12 hadi 15 baadaye. Pia taa ya aina hiyo inaweza kutumika kwa muda mrefu zaidi, na aina nyingi nyingine kama hiyo zimetolewa."

Imefahamika kuwa, mbali na kutumika nyumbani, hivi sasa taa zenye globu za kubana matumizi ya nishati zimeanza kutumika kwenye vituo vya basi, maduka makubwa na cinema. Ingawa matumizi ya taa za aina hiyo yanaongeza siku hadi siku nchini China, lakini kwa jumla bado zinachukua asilimia ndogo kwenye soko la globu nchini China, hivyo uwezo wake wa kubana matumizi ya nishati bado haujaonekana kikamilifu. Ili kueneza zaidi matumizi ya taa zenye globu za aina hiyo, wataalamu husika wamependekeza kuwa wakati serikali inapoendelea kueneza mwamko wa kubana matumizi ya nishati, pia inapaswa kuviunga mkono zaidi viwanda vya kutengeneza taa zenye globu za aina hiyo. pia serikali inapaswa kuchukua hatua mbalimbali kuhimiza viwanda hivyo vitoe bidhaa mpya ili kukidhi mahitaji ya wateja.