Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-24 19:12:17    
Li Changchun akutana na rais Benjamin Mkapa wa Tanzania

cri

Mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China Bwana Li Changchun tarehe 23 asubuhi kwa saa za huko Dar es Salaam alikutana na rais wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi cha Tanzania Benjamin William Mkapa, ambapo Bwana Li Changchun alisema kuwa Bara la Afrika lina utamaduni mwingi unaong'ara na ustaarabu wa kale, hadhi na athari ya Bara la Afrika inaongezeka siku hadi siku katika hali mpya duniani. Amesema China imeona kwa furaha kuwa, vyama vya nchi mbalimbali za Afrika vinawaongoza wananchi wao katika kujenga taifa, kutafuta njia ya maendeleo inayofuata hali halisi ya kila nchi, na kupata maendeleo siku hadi siku. Katika hali mpya, maslahi ya pamoja ya China na Afrika yameongezeka; na sekta za ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika pia zinaongezeka zaidi. Pia amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika katika kutafuta njia mpya za ushirikiano, aina mpya na sekta mpya za ushirikiano, na kushirikiana pamoja kutoa mchango kwa ajili ya kulinda amani ya duniani, kusukuma mbele maendeleo ya dunia na kuhimiza maendeleo ya binadamu.

Bwana Li Changchun alisema kuwa, uhusiano wa kirafiki kati ya China na Tanzania ulianzishwa na viongozi wazee wa nchi hizo mbili, baadaye umetunzwa vizuri na viongozi wa awamu kadhaa wa nchi hizo mbili. Katika miaka ya hivi karibuni, China na Tanzania zimeanzisha ushirikiano wenye mafanikio katika sekta za siasa, uchumi, elimu, utamaduni na afya. Mawasiliano kati ya vyama vya China na Tanzania siku zote ni msingi wa kisiasa wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Bwana Li Changchun ameishukuru Tanzania kwa uungaji mkono wake wenye thamani kwa China katika suala la Taiwan na masuala mengine, na amesema chama na serikali ya China zitafanya juhudi kama zilivyofanya miaka mingi iliyopita katika kuendeleza urafiki kati ya China na Tanzania na kuimarisha zaidi ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.

Bwana Li Changchun pia amesifu mafanikio aliyopata rais Mkapa katika kuwaongoza wananchi wa Tanzania kuendeleza uchumi wa taifa na kusukuma mbele maendeleo ya jamii kwa pande zote. Alisema chama, serikali na wananchi wa China wanafurahi kuona Tanzania imekuwa moja kati ya nchi ambazo uchumi wake unaendelezwa kwa haraka zaidi barani Afrika, na wanaitakia Tanzania ustawi na baraka zaidi katika siku zake za usoni.

Rais Mkapa alisema ziara ya Bwana Li Changchun imetuwezesha kukumbuka tena historia ndefu ya urafiki na ushirikiano kati ya vyama viwili, nchi mbili na wananchi wa nchi mbili Tanzania na China. Tanzania na China kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, si kama tu kunalingana na maslahi ya kimsingi ya nchi mbili na wananchi wa nchi hizo mbili, bali pia kunasaidia kuinua hadhi na athari ya nchi zinazoendelea. Rais Mkapa alidhihirisha kuwa, maingiliano kati ya chama cha mapinduzi cha Tanzania na chama cha kikomunisti cha China ni nguzo kubwa ya uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta mbalimbali. Chama cha mapinduzi cha Tanzania kinakishukuru chama, serikali na wananchi wa China kutokana na uungaji mkono wao kwa mapinduzi na ujenzi wa Tanzania, na kinapenda kushirikiana na China katika kutafuta njia mpya ya kuimarisha mawasiliano kati ya vyama vyao na kuanzisha ushirikiano wa kunufaishana.

Baada ya mkutano huo, Bwana Li Changchun na rais Mkapa walihudhuria sherehe ya kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia kati ya China na Tanzania.