Chama tawala cha uhuru na demokrasia cha Japan hivi karibuni kimetangaza mswada wa marekebisho ya katiba utakaowasilishwa kwenye bunge la nchi hiyo, mambo makuu ya mswada huo ni kuacha kifungu kilichoko kwenye katiba inayofuatwa sasa kuhusu Japan haipaswi kumiliki jeshi. Hali hiyo ya mambo imefuatiliwa kwa makini sana na jumuiya ya kimataifa hasa nchi za Asia zilizo majirani ya Japan.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bwana Liu Jianchao tarehe 24 alisema kuwa, kutokana na sababu za kihistoria, nchi za Asia siku zote zinafuatilia sana mwelekeo wa Japan kurekebisha katiba, China inaona kuwa, Japan kushikilia mwelekeo wa maendeleo ya kiamani, hii inalingana na maslahi ya kimsingi ya Japan yenyewe, na kusaidia amani, utulivu na maendeleo ya sehemu hiyo.
Kutokana na mafunzo ya huzuni kuhusu Japan ilifanya uvamizi wa kiwazimu dhidi ya nchi za Asia kwa kufuata sera ya upanuzi wa nje iliyowekwa na wanajeshi wa Japan waliopenda vita katika miaka ya 30 na 40 ya karne iliyopita, baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, Japan iliweka katiba mwaka 1947, kifungu cha 9 cha katiba hiyo kilieleza bayana kuwa, "daima kuacha mbinu za kuanzisha vita kwa ajili ya mamlaka ya nchi, na kuacha tishio la kijeshi au kutumia nguvu za kijeshi katika utatuzi wa migogoro ya kimataifa. Ili kutimiza lengo hilo, Japan haidumishi nguvu za majeshi ya nchi kavu, baharini na angani na nguvu nyingine za kivita, na kutotambua haki ya nchi ya kushiriki vita." Katiba hiyo iliitwa kuwa "katiba ya amani", na ikawa msingi wa mambo ya ndani ya Japan na sera nyingi za kidiplomasia ya nchi hiyo, na kanuni zake za kimsingi zimetekelezwa tangu hapo mpaka sasa.
Katika mchakato wa maendeleo ya uchumi wa Japan baada ya vita, "katiba ya amani" ilifanya kazi yake isiyoweza kuchukuliwa na nyingine. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kadiri nguvu halisi ya uchumi wa Japan inavyoongezeka na mambo yake ya kisiasa yanavyoelekea mrengo wa kulia, ndivyo Japan inavyotaka kujitoa kutoka kivuli cha "nchi iliyoshindwa katika vita", na kutaka kuwa "nchi kubwa kisiasa. Ndiyo maana, ikatokea sauti ya kukiuka "katiba ya amani" na kuacha kifungu cha 9 cha katiba hiyo. Kwa kweli kikosi cha kujilinda cha Japan kimekuwa jeshi la nchi hiyo, nguvu yake halisi inachukua nafasi ya pili duniani baada ya Marekani. Aidha, Japan ikipitia utungaji wake wa sheria mbalimbali za kijeshi kama vile "sheria kuhusu hali ya mambo ya pembezoni mwa Japan", "sheria kuhusu hali ya mambo ya mashambulizi ya kijeshi" na kadhalika, imeondoa vikwazo vya kisheria kwa ajili ya kutuma kikosi chake cha kujilinda kwa nchi za nje.
Tarehe 22 mwezi huu, chama cha uhuru na demokrasia cha Japan kiliposherehekea miaka 50 ya chama hicho, kilitangaza rasmi mswada wa marekebisho ya sheria. Mswada huo umerekebishwa kutoka "Japan haipaswi kumiliki majeshi ya baharini, nchi kavu na angani pamoja na vikosi vingine vya kufanya vita" kuwa " Ili kulinda amani, uhuru wa nchi na usalama wa taifa na wananchi, Japan inapaswa kuwa na jeshi la kujilinda, ambapo waziri mkuu awe kiongozi mkuu", imekifanya waziwazi kikosi cha kujilinda kuwa "jeshi la kujilinda", tena kuruhusu kutuma vikosi nchi za nje.
Mswada huo marekebisho ya katiba umetoa ishara wazi kwa dunia nzima yaani: kumiliki jeshi, kutambua haki ya nchi ya kushiriki vita, na kurasimisha kupelekea jeshi kwa nchi za nje. Japan inafanya chini juu kusukuma mbele hatua ya kurekebisha katiba, kuendeleza kwa nguvu kubwa nguvu yake ya kijeshi, na kutumia fursa mbalimbali kutuma kikosi chake kwa nchi za nje ili kujifanya kuwa nchi kubwa ya kijeshi, mwelekeo huo unapaswa kufuatiliwa na watu, ambapo watu wana wasiwasi kuwa Japan inaweza kukumbuka mafunzo yake ya kihistoria na kufuata kweli njia ya maendeleo ya kiamani au la.
|