Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-29 17:00:16    
Mkoa wa Henan, kituo muhimu cha viwanda vya kutengeneza chakula nchini China

cri
Takwimu zinaonesha kuwa, kati ya kila mifuko 3.5 ya tambi za haraka zinazouzwa nchini China mmoja unatengenezwa mkoani Henan, na kampuni 9 za Henan zimeorodhishwa kwenye kampuni 50 kubwa zaidi katika sekta ya chakula cha nyama nchini China. Habari kutoka kwenye Maonesho ya pili ya viwanda vya chakula vya kimataifa vya sehemu ya kati na ya magharibi ya China zinasema kuwa, baada ya juhudi kubwa katika kipindi cha utekelezaji wa Mpango wa 10 wa "Miaka Mitano" wa taifa, thamani ya jumla ya uzalishaji wa mkoa wa Henan katika viwanda vya chakula imeshika nafasi ya nne nchini China, na kushika nafasi ya kwanza katika sehemu ya kati na ya magharibi, na mkoa huo umekuwa kituo muhimu cha viwanda vya chakula nchini China.

Mkoa wa Henan uko katika tambabare ya kati nchini China, ni mkoa unaozalisha kwa wingi bidhaa za kilimo na chakula kinachouzwa masokoni nchini China, na mkoa huo una msingi mzuri na nguvu bora katika kuendeleza viwanda vya chakula. Katika miaka ya hivi karibuni, mkoa huo umekuwa ukitilia maanani kuendeleza viwanda vya chakula katika mipango yake minne mfululizo ya "Miaka Mitano", na imekuwa ikiweka mkazo katika kuendeleza sekta hiyo kama nguzo ya kiuchumi ya mkoa huo. Katika miaka mitano iliyopita, ili kutimiza lengo la kuanzisha kituo muhimu cha utengenezaji wa ngano na mazao ya mifugo nchini China, mkoa wa Henan uliunganisha kazi ya uongozi wa soko na uelekezaji wa serikali, kurekebisha miundo ya shughuli, na kuimarisha kampuni za mkoa huo zenye sifa nzuri nchini China. Wakati wa utekelezaji wa mpango wa 10 wa "Miaka Mitano", wastani wa ongezeko la mapato ya mauzo ya viwanda vya chakula mkoani Henan lilifikia asilimia 23. 6, kiasi ambacho kilizidi asilimia 5 kuliko kiwango cha wastani nchini kote. Mwaka 2004, mapato ya mauzo ya chakula mkoani humo yalifikia yuan bilioni 10.68, na kutimiza lengo la kuongezeka maradufu kwa mwaka mmoja kuliko iliyotazamiwa, na viwanda vya chakula vinachukua asilimia 15 katika viwanda vyote mkoani Henan.

Wakati viwanda vya chakula vya mkoa wa Henan vinapoendelea kwa kasi, kampuni na bidhaa mbalimbali zenye sifa nzuri na uwezo mkubwa wa ushindani nchini na nchi za nje vimejitokeza mkoani humo. Mkurugenzi wa Ofisi ya viwanda vya chakula ya mkoa wa Henan Bw. Chen Zhenjie anaeleza kuwa, hivi sasa mkoa wa Henan umekuwa kituo kikubwa cha kutengeneza mazao ya mifugo, tambi za haraka, biskuti na kadhalika. Aidha aina 19 za bidhaa za kampuni 16 za mkoa huo zikiwemo Shuang Hui, Jin Xing, Lian Hua, Bang Jie, San Quan, Si Nian na Hai Jia zimesifiwa kuwa ni chapa maarufu za bidhaa za China, na kampuni 6 za China zikiwemo Shuang Hui, Nan Jie Cun na Jin Si Hou zimesifiwa kuwa nembo maarufu za bidhaa za China.

Licha ya hayo, maendeleo ya kasi ya viwanda vya chakula vya Henan na kufunguliwa kwa soko zinavutia kampuni maarufu nchini na nchi za nje kuwekeza vitega uchumi na kuanzisha biashara mkoani humo. Imefahamika kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, kampuni mbalimbali maarufu kutoka nchini na nchi za nje zikiwemo Dubond, Danisco, Kang Shi Fu, Tong Yi, Hui Yuan, Meng Niu, Wa Ha Ha na Le Bai Shi zimeanzisha shughuli zao mkoani Henan.