Tarehe 1 mwezi Desemba mwaka huu ni siku ya kutimiza miaka 18 tangu iwekwe "siku ya Ukimwi duniani". Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Afya duniani WHO inasema kuwa, ingawa maambukizi ya Ukimwi yamepungua katika nchi za Caribbean na nchi chache za Afrika, lakini maambukizi ya Ukimwi duniani bado ni makubwa.
Tangu kugunduliwa mgonjwa wa kwanza wa Ukimwi duniani mwaka 1981 hadi hivi sasa, idadi ya watu waliokufa kutokana na Ukimwi, imefikia milioni 25 na kuwa ugonjwa mkubwa katika historia ya binadamu. Mwaka 2005, duniani kuna watu milioni 3.1 waliokufa kutokana na Ukimwi wakiwemo watoto laki 5 na elfu 70; Mwaka huu idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi iliongezeka kwa milioni 4.9, na kuifanya idadi ya watu wenye virusi vya Ukimwi duniani kufikia milioni 40 na laki 3, ongezeko hilo ni kubwa zaidi katika historia ya binadamu.
Sehemu ya Afrika kusini mwa Sahara bado ni sehemu iliyoathiriwa vibaya zaidi na Ukimwi, ambapo watu zaidi ya milioni 25 na laki 8 wameambukizwa virusi vya Ukimwi, na ongezeko la watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi linakaribia milioni 1 katika miaka miwili iliyopita. Theluthi mbili za idadi ya watu wenye virusi vya Ukimwi na 65% ya ongezeko la idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi ni wa sehemu hiyo. Barani Asia ambako kuna idadi kubwa kabisa ya watu, hivi sasa idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi inaongezeka kwa kasi. Hivi sasa 20% ya watu wenye virusi vya Ukimwi wanaishi katika barani Asia, ikilinganishwa na hali ya zamani ambayo uwiano huo ulikuwa 10 kwa 1. Ongezeko la watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi barani Asia katika mwaka 2005 lilikuwa milioni 1.1, na kufanya idadi ya watu wenye virusi vya Ukimwi kuongezeka hadi kufikia milioni 8.3. Katika nchi moja ya India, idadi ya watu wenye virusi vya Ukimwi imefikia milioni 5.13, ambayo inachukua nafasi ya kwanza barani Asia na kuchukua nafasi ya pili katika duniani. Idadi ya watu wenye virusi vya Ukimwi kwenye sehemu ya Asia ya mashariki imeongezeka kwa 20% kuliko miaka miwili iliyopita. Licha ya hayo, kasi ya maambukizi ya Ukimwi kwenye sehemu ya Ulaya ya mashariki pia ni ya kushangaza, mwaka huu idadi ya watu waliokufa kutokana na Ukimwi ni maradufu kuliko miaka miwili iliyopita.
Kuhusu China, Shirika la kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa na WHO zinaona kuwa kwa jumla maambukizi ya Ukimwi hivi sasa bado yako miongoni mwa watu wenye hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo, lakini katika baadhi ya sehemu maambukizi hayo yanaelekea kati ya watu wa kawaida, hivyo udhibiti wa maambukizi ya Ukimwi nchini China uko katika kipindi muhimu sana.
Mashirika hayo mawili ya Umoja wa Mataifa yanaona kuwa hivi sasa udhibiti wa maambukizi ya Ukimwi unakabiliwa na changamoto kali. Kwanza kuhusu ufahamu, njia ya maambukizi na kuchukua tahadhari dhidi ya Ukimwi, watu bado hawajafahamu vizuri. Uchunguzi uliofanywa juu ya wasichana na wanawake vijana 24 unaonesha kuwa theluthi 2 ya wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24 hawafahamu vizuri njia za kuambukiza virusi vya Ukimwi. Hivyo mashirika hayo mawili ya Umoja wa Mataifa yamesisitiza kuwa uenezi na uelimishaji kwa umma, ni njia ya msingi kabisa ya kudhibiti maambukizi ya Ukimwi.
Pili, sehemu tofauti za dunia zinakabiliwa na matatizo yake ya kipekee. Kwa baadhi ya nchi za Asia, Latin Amerika na Ulaya ya mashariki, tatizo kubwa zaidi ni matumizi ya mihadarati na ukahaba. Kwa Afrika ya kaskazini, mashariki ya kati na sehemu ya Caribbean tatizo lake ni udhaifu wa upimaji, na baadhi ya watu wenye hatari kubwa ya maambukizi hawajawekwa katika mpango wa udhibiti. Aidha, katika nchi zilizoendelea hali ya mama kuwaambukiza watoto wao kwa kuwanyonyesha imetokomea, lakini katika sehemu ya Afrika ya kusini mwa sahara tatizo hilo bado ni kubwa.
Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanaona kuwa, uzoefu umethibitisha kuwa maambukizi ya Ukimwi hayataweza kudhibitiwa vizuri bila kushikilia mambo mawili ya kinga na tiba za Ukimwi.
|