Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-30 19:52:33    
Mapishi ya supu ya vipande vya nyama ya nguruwe pamoja na nyanya

cri

Mahitaji

Nyanya mbili, vipande vya nyama ya nguruwe gramu 600, kabichi 1/4, kiasi kidogo cha giligilani, sosi ya nyanya vijiko vinne, chumvi kijiko kimoja, maji ya wanga vijiko vinne.

Njia

1. Pasha moto na chemsha maji mpaka yachemke, tia vipande vya nyama ya nguruwe ndani ya maji ya moto baada ya dakika mbili, vipakue.

pasha moto tena tia vipande vya nyama ya nguruwe ndani ya chungu, mimina maji, tia chumvi, yachemshe baada ya kuchemka tia sosi ya nyanya na punguza moto kidogo na endelea kuchemsha kwa dakika 30, tia vipande vya kabichi na nyanya, endelea kuchemsha kwa dakika 5, mimina maji ya wanga, pakua na tia vipande vya giligilani kwenye supu hiyo. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari kuliwa.