Vyombo vya habari vya Lebanon tarehe mosi Disemba vilitangaza kuwa maofisa watano wa upelelezi Syria wanaotuhumiwa kushiriki kwenye tukio la kuuawa kwa Rafik al-Hariri, waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, tarehe 5 watahojiwa huko Vienna, mji mkuu wa Austria. Lakini kutokana na kuwa mtu mmoja muhimu alitoa ushahidi wa uwongo, mjumbe wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa Bw. Faisal Miqdad ametaka Umoja wa Mataifa ufanye uchunguzi upya kuhusu tukio hilo.
Mtu aliyetoa ushahidi wa uwongo ni raia wa Syria, anaitwa Husam Taher Husam. Tarehe 28 mwezi uliopita kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini Damascus alisema, kutokana na kushinikizwa na kuhongwa alitoa ushahidi wa uwongo unaodhuru Syria kwa tume ya uchunguzi ya kimataifa. Na kwamba aliishi nchini Lebanon miaka 13, na aliwahi kuifanyia kazi idara ya upelelezi ya Syria. Muda si mrefu baada ya Hariri kuuawa tarehe 14 Februari alifungwa na wafuasi wa mtoto wa Hariri Saad al-Hariri na kuteswa vibaya, alilazimishwa kusema uongo kuwa watu waliopanga kumwua Hariri ni ndugu wa rais wa Syria na shemeji yake, waziri wa mambo ya ndani wa Lebanon Hassan al-Sabaa alimpa dola za Kimarekani milioni 1.3 atoe ushahidi wa uwongo kwa mkuu wa tume ya uchunguzi ya kimataifa Bw. Detlev Mehlis. Kutokana na kuwa Mehlis hakujua ukweli ulivyo alimnukuu Husam maneno yake mengi ya ushahidi katika ripoti yake ya mwezi Oktoba kwa Umoja wa Mataifa.
Kutokea kwa Husam kumefanya uchunguzi kugubikwa na wingu. Tume ya sheria inayoshughulikia kesi ya Hariri ilisema kuwa, kwa kuwa ripoti ya Mehlis ilitolewa katika msingi wa ushahidi wa uwongo uliotolewa na Husam, shutuma kwa Syria lazima zisahihishwe, ikitaka tume ya uchunguzi ya kimataifa ipime upya matokeo yaliyofanywa kabla hapo. Serikali ya Lebanon na familia ya Hariri mara moja ilikanusha kuwa iliwahi kumlazimisha Husam kuisingizia Syria. Na askari wa usalama wa Lebanon waliwatia mbaroni mchumba wake pamoja na baba wa mchumba wake. Bw. Mehlis alishutumu Syria kumtumia Husam kama ni chombo cha uenezi wa siasa na kuuwekea vizuizi upelelezi.
Mbadiliko hayo ya ghafla yanafuatiliwa kwenye udadisi kwa maofisa waandamizi wanaotuhumiwa waliopo huko Vienna. Bw. Mehlis alisema, kikundi maalumu cha tume ya uchunguzi ya kimataifa kitakwenda Vienna, lakini yeye mwenyewe hatakwenda huko kuwahoji. Alisema, kwenye kuwahoji hakutakuwa na masharti yoyote. Ili kuhakikisha haki ya watuhumiwa na uadilifu wa upelelezi, Syria haikutangaza majina ya maofisa hao. Wizara ya mambo ya nje ya Syria imesisitiza kuwa maofisa hao watahojiwa kwa mujibu wa mkataba kati Mehlis na mshauri wa sheria wa Syria. Kitu kinachofuatiliwa ni kwamba kutokana na mabadiliko hayo, kuwahoji watu hao kutaweza kuendelea kama mpango ulivyopangwa na matokeo ya kuwahoji yataathiri vipi uchunguzi.
Wachambuzi wanaona kuwa tarehe 15 iliyowekwa ya kuwasilisha ripoti ya uchunguzi itakayotolewa na Mehlis imekaribia. Kutokana na kuwa uchunguzi unakwenda pole pole na kutokea kwa mabadiliko hayo, uwezekano wa kupata matokeo ya uchunguzi kwa bayana utakuwa mdogo. Imefahamika kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan ameziarifu nchi wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akitaka kurefusha muda wa uchunguzi. Msaidizi wake alikadiria kuwa baada ya ripoti ya mwisho itakayotolewa na Mehlis tarehe 15 mwezi huu, atamwagiza mwingine kazi ya uchunguzi huo. Kwa hiyo, jinsi uchunguzi unavyofanywa kwa kina zaidi ndivyo mgongano unaohusu tukio hilo utakuwa mkali zaidi.
Idhaa ya kiswahili 2005-12-02
|