Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-02 17:13:28    
Naibu waziri mkuu wa China Bw. Huang Ju kutoa mapendekezo matano kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika

cri

Naibu waziri mkuu wa China Bw. Huang Ju na waziri mkuu wa Madagascar Bw. Jacques Sylla tarehe 23 huko Antananrivo walishiriki kwenye ufunguzi wa Kongamano la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Madagascar. Bw. Huang alitoa hotuba kuhusu "Kushirikiana na kujenga mustakabali mzuri", na kutoa mapendekezo matano kuhusu kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika.

Bw. Huang alisema, China siku zote inatilia maanani uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati yake na nchi za Afrika. Katika mawasiliano ya muda mrefu kati ya China na Madagascar na nchi za Afrika, pande hizo mbili zinatendeana kwa usawa, kuelewana, kuungana mkono na kusaidiana, na kuwa marafiki wa dhati na wenzi muhimu wa ushirikiano. Katika miaka ya hivi karibuni, pande hizo mbili zimepata mafanikio mapya ya ushirikiano ndani ya mfumo wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, kumekuwa na maendeleo makubwa katika uhusiano wa kibiashara kati ya pande hizo mbili, uwekezaji vitega uchumi umekuwa ukiongezeka, maeneo ya ushirikiano yamezidi kupanuka, kiwango cha ushirikiano kinazidi kuongezeka siku hadi siku, na uhusiano wa kirafiki na ushirikiano umeingia katika kipindi kipya cha maendeleo.

Bw. Huang Ju alisema, China na nchi za Afrika zote ni nchi zinazoendelea, na katika hali mpya, kukuza urafiki wa jadi, kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano, kunalingana na maslahi ya pamoja ya pande hizo mbili. Mwezi Septemba mwaka huu, kwenye Mkutano wa ngazi ya juu ya kukusanya fedha kwa maendeleo wa Mkutano wa viongzi wa Umoja wa Mataifa, rais Hu Jintao wa China alitangaza hatua tano muhimu za China za kuunga mkono kuhimiza maendeleo ya nchi zinazoendelea. Hii imetoa fursa nzuri katika kuleta hali mpya ya uhusiano wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta zote.

Bw. Huang Ju alisema, ili kutekeleza hatua hizo, na kutimiza lengo la kupata maendeleo ya pamoja, ametoa mapendekezo kuhusu kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Madagascar na nchi za Afrika katika hali mpya:

Kwanza, kupanua ushirikiano wa kibiashara kwa msingi wa usawa na kunufaishana. Maendeleo ya kasi ya China yametoa soko kubwa na fursa nyingi kwa Afrika. China ingependa kuendelea kufanya juhudi za pamoja na Afrika kuzidi kuboresha miundo ya biashara, pia itaendelea kuhimiza kampuni za China kuweka mkazo kuagiza bidhaa kuoka Afrika, na kuongeza thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 100 kutoka bilioni 30 ya hivi sasa ndani ya miaka mitano. China inaunga mkono kutafuta mazingira ya haki ya biashara ya kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya Afrika.

Pili, kujitahidi kuendeleza ushirikiano na uwekezaji. China itahimiza kampuni zenye uwezo na sifa nzuri kuanzisha biashara barani Afrika, na kufanya uwekezaji wa China barani Afrika uongezeke kwa maradufu ndani ya miaka 5 ijayo, ili kutoa ajira nyingi zaidi barani Afrika na kuleta manufaa ya pamoja. China inahimiza kuimarisha ushirikiano kati ya mashirika ya fedha ya pande hizo mbili, na kutoa huduma za fedha kwa shughuli za uwekezaji za kampuni za pande hizo mbili.

Tatu, kupanua maeneo, kuongeza mambo ya ushirikiano na njia za ushirikiano. China na Afrika zinaweza kusaidiana katika maeneo makubwa ya kiuchumi. Pande hizo mbili zinatakiwa kuimarisha ushirikiano kati yao katika maeneo ya jadi yakiwemo kilimo, ujenzi wa miundo mbinu, tiba na afya na elimu, huku zikihimiza ushirikiano wa utalii, fedha na teknolojia na kupanua maeneo ya ushirikiano kwa kuunganisha njia mbalimbali za biashara, miradi na uwekezaji vitega uchumi.

Nne, kuimarisha ushirikiano wa kuendeleza nguvu kazi. Wataalamu ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi. China itaziandalia nchi za Afrika aina mbalimbali za makongamano katika sekta za usimamizi wa uchumi, kilimo, tiba na afya, utamaduni na elimu, forodha na mambo ya kidiplomasia kutokana na mahitaji ya nchi hizo, kuzisaidia kuimarisha ujenzi wa uwezo na kutimiza maendeleo endelevu.

Tano, kutoa mazingira mazuri kwa ushirikiano kati ya China na Afrika. Pande hizo mbili zinapaswa kutoa ushauri kuhusu sera na huduma za upashanaji habari kwa kampuni za kila upande kuanzisha ushirikiano, kukamilisha sheria za kuzisaidia kampuni za pande hizo mbili kufanya ushirikiano, na kuongoza na kuhimiza kampuni kufanya aina mbalimbali za mawasiliano na ushirikiano. Pia inapaswa kutumia mfumo wa ushirikiano wa serikali za pande hizo mbili kuimarisha mawasiliano na majadiliano, ili kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili zipate maendeleo mazuri.