Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-07 16:58:21    
Mapishi ya slesi za viazi mviringo kwa pilipili hoho na siki

cri

Mahitaji

Viazi mviringo gramu 250, nyama ya nguruwe gramu 50, siki gramu 20, pilipili hoho gramu 5, vitunguu maji gramu 2, chumvi gramu 5, M.S.G gramu 2.

Njia

1. kata viazi mviringo viwe slesi, viioshe kwa maji halafu vikaushe.

2. kata nyama ya nguruwe iwe vipande vipande, na kata pilipili hoho iwe vipande vipande.

3. pasha moto na tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi 60, tia vipande vya pilipili hoho, korogakoroga, halafu tia vipande vya nyama ya nguruwe, korogakoroga na tia slesi za viazi mvirongo kisha korogakoroga kwa haraka, tia M.S.G, chumvi na korogakoroga mimina siki korogakoroga, tia vipande vya vitunguu maji. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.