Waziri mkuu wa China Wen Jiabao tarehe 6 alitoa hotuba katika Chuo kikuu cha Ecole Polytechnique cha Paris cha Ufaransa. Kwenye hotuba hiyo isemayo "Kuheshimu ustaarabu wenye tofauti, kujenga dunia yenye masikilizano", Bwana Wen Jiabao amefahamisha kutoka historia na hali ya sasa ilivyo kuhusu ulazima na uthamini wa aina nyingi za utamaduni na kujulisha hali ya nchini na mambo ya kidiplomasia ya China.
Bwana Wen Jiabao kwanza alifahamisha umuhimu wa aina nyingi za utamaduni kwa jamii ya binadamu, akisema:
Hivi leo, mageuzi ya kina yanatokea katika ustaarabu wa binadamu, maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia na mawasiliano ya kiuchumi na kiutamaduni yanapunguza umbali kati ya ustaarabu wa aina mbalimbali. Kwa taifa la China au taifa la Ufaransa, kila upande umerithi na kuenzi utamaduni ulio wa msingi wa taifa na roho ya taifa. Aina nyingi za utamaduni ni umaalum muhimu wa ustaarabu wa binadamu, aina nyingi za utamaduni za jamii ya binadamu ni kama zilivyo aina nyingi za viumbe duniani, yote ni hali halisi iliyopo. Tukiheshimu aina nyingi za utamaduni, ndipo tutakapoweza kuuwezesha ustaarabu wa binadamu upate maendeleo.
Bwana Wen Jiabao amesisitiza pia kuwa kama tukitimiza amani kati ya nchi na nchi, masikilizano kati ya watu na watu na mapatano kati ya binadamu na dunia ya kimaumbile, ndipo ustaarabu wa binadamu utakapoweza kupata maendeleo endelevu.
Bwana Wen Jiabao alijulisha hasa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ya China inayotekelezwa kuanzia mwishoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita. Akisema:
Mageuzi ya China yanafanyika katika pande zote, tunapohimiza mageuzi ya mfumo wa uchumi, tunajitahidi kuhimiza mageuzi ya mfumo wa kisiasa, kiutamaduni na mfumo wa usimamizi wa jamii. Kutekeleza mageuzi na ufunguaji mlango, kunatakiwa kuhamasisha ipasavyo mamilioni ya wananchi wa China wafanye juhudi na mavumbuzi, kukomboa na kuendeleza zaidi nguvu kazi, kukidhi siku hadi siku mahitaji ya kimali na kiutamaduni ya watu yanayoongezeka siku hadi siku, ambapo tunatakiwa kujifunza na kuiga vya kutosha matokeo mazuri ya ustaarabu wa aina zote duniani, kutekeleza wazo la kujiendeleza kwa njia za kisayansi, kujenga jamii yenye masikilizano, kukamilisha mfumo wa kidemokrasia na kutekeleza mikakati ya kimsingi kwa mujibu wa sheria. Kwa ujumla kwa kupitia mageuzi, tutaijenga jamii yetu iwe na ustawi zaidi, uhuru zaidi na usawa zaidi, yenye utaratibu na sheria zaidi ili kuufanya ustaarabu wa taifa la China ung'are zaidi.
Bwana Wen Jiabao alisisitiza pia kuwa, China inayojitahidi kuondokana na umaskini na kutafuta maendeleo, imeleta fursa kubwa zaidi kwa dunia kutokana na njia iliyochagua ya maendeleo ya kiamani. Alisema:
China inashika kithabiti njia ya maendeleo ya kiamani, kutekeleza sera ya ufunguaji mlango ya kunufaishana na kupata maendeleo ya pamoja. Watu wenye busara duniani wanaweza kuona kuwa maendeleo ya China yatakuwa ni fursa kwa dunia, bali siyo tishio. Utulivu na maendeleo ya China yanachangia amani na ustawi wa duniani. China kushika njia ya maendeleo ya kiamani, ni chaguo la lazima, la muda mrefu na la thabiti kutokana na historia na utamaduni wa jadi na mahitaji ya maslahi halisi ya China.
Bwana Wen Jiabao alitoa mwito vijana wa nchi zenye ustaarabu tofauti washirikiane, kuimarisha mawasiliano na kuongeza maelewano ili kujenga dunia mpya yenye amani na masikilizano.
Idhaa ya Kiswahili 2005-12-07
|