Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-08 18:20:43    
Sun Zhenyu aeleza msimamo wa China kuhusu mazungumzo ya Doha

cri

Balozi wa China katika Shirika la Biashara Duniani, WTO Bw. Sun Zhenyu hivi karibuni alipohojiwa na mwandishi wa habari alieleza msimamo wa China kuhusu mazungumzo ya duru la Doha.

Ofisa wa China katika WTO tarehe 7 huko Geneva alidokeza kuwa Bw. Sun Zhenyu alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema kuwa, China ikiwa mwanachama mpya wa WTO inachukua msimamo kuhimiza mazungumzo ya duru la Doha. China pamoja na nchi wanachama zinazoendelea zinajitahidi kurekebisha makosa ya nchi zilizoendelea kuhusu biashara ya mazao ya kilimo. Kutokana na kuwa mazungumzo ya duru la Doha ni duru la mazungumzo la maendeleo, hivyo yanatakiwa kuzingatia zaidi matatizo yanayozikabili nchi zinazoendelea na kuziunga mkono nchi hizo, hususan kuchukua msimamo wa wenye unyumbufu na kuzipa nchi hizo muda mrefu zaidi kuhusu maeneo muhimu yanayohusiana na maisha ya watu, maendeleo ya sehemu za vijijini na usalama wa chakula ili ziweze kukamilisha marekebisho kuhusu muundo wa sekta husika na kuendana na hali mpya duniani.

Bw. Sun Zhenyu alisema, "katika muda wa zaidi ya miaka minne iliyopita tangu kuanzishwa kwa mazungumzo ya duru la Doha, nchi wanachama zina maoni mengi tofauti kuhusu ajenda za mazungumzo, hususan masuala kuhusu mazao yasiyo ya kilimo na biashara ya utoaji huduma, na tatizo kubwa lililopo ni kukosa dhamira ya kisiasa kwa nchi zilizoendelea zinazoongozwa na Ulaya na Marekani, kuhusu kupunguzwa kwa kiwango kikubwa cha utoaji ruzuku ya kilimo na kulegeza masharti kwa maombi ya kuingia soko la dunia."

Alisema, "tokea miaka mingi iliyopita, nchi zilizoendelea, hususan Marekani na nchi za Ulaya, zilitoa ruzuku kubwa kwa sekta ya kilimo, hatua ambayo imepotosha biashara ya mazao ya kilimo na kudhuru sana maslahi ya nchi zinazoendelea. Kutokana na kuathiriwa na mambo mengi ya nchini na duniani, hivi sasa Marekani na Ulaya bado hazijaamua kubadilisha hali hiyo isiyo ya haki. Hivyo zimechukua msimamo wa ukaidi wa kukwamisha mazungumzo hayo.

Katika eneo la mazao yasiyo ya kilimo, kuna maoni tofauti sana kuhusu upunguzaji wa ushuru wa forodha, nchi nyingi wanachama zinaelekea kuweka viwango tofauti kwa nchi za viwanda na nchi zinazoendelea. Nchi za viwanda zinazoongozwa na Marekani, Ulaya na Japan zinataka tofauti hiyo iwe ndogo, wakati nchi zinazoendelea zinazoongozwa na China na Pakistan zinataka tofauti hiyo iwe kubwa kiasi; na nchi nyingine Brazil na India zinataka wastani wa kiwango cha ushuru wa forodha uzingatiwe ili kuzipa unyumbufu mkubwa zaidi nchi zinazoendelea.

Katika eneo la utoaji huduma, nchi zinazoendelea zinashikilia kuwa kila nchi mwanachama ina haki ya kupanga bei kwa mujibu wa kiwango cha maendeleo ya uchumi wake. Lakini nchi zilizoendelea zinataka kiwekwe kiwango cha utoaji bei kutokana na mapendekezo ya pande nyingi, ambapo nchi wanachama zinatakiwa kufikia kiwango cha ulingano kuhusu idadi na kiwango cha maeneo yanayofungua mlango, lakini pendekezo hilo lilipingwa na nchi nyingi zinazoendelea.

Bw. Sun Zhenyu alisema nchi nyingi zinazoendelea zinatarajia kufikia jumla ya makubaliano kwenye mkutano utakaofanyika huko Hong Kong kuhusu kusamehewa ushuru kwa nchi zilizokuwa nyuma kabisa kimaendeleo pamoja na masuala kuhusu afya za umma, pamba na utoaji msaada wa kibiashara ili kunufaika mapema kadiri iwezekanavyo.

Kuhusu mustakabali wa mkutano wa Hong Kong wa WTO, Bw. Sun alisema kuwa mkutano huo ni vigumu kutimiza kabisa lengo lililowekwa hapo awali na kupiga hatua halisi. Ingawa mkutano wa Hong Kong hautaweza kupata mafanikio makubwa kama ya mazungumzo ya duru la Doha, lakini pia hautaweza kushindwa kabisa kama mkutano wa Cancun.

Idhaa ya Kiswahili 2005-12-08