Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-09 20:48:16    
Daktari wa mkoa wa Hunan anliyekuwa anafanya kazi nchini Sierra Leone

cri

Tarehe 14 Oktoba mwaka huu, muda si mrefu baada ya naibu mkuu wa Hospitali ya umma ya wilaya ya Dong'an Bw. Jiang Songquan kurejea nchini China kutoka Afrika, alipata barua kutoka Sierra Leone. Barua hiyo ilitoka kwa mwanamke mmoja wa nchi hiyo Bi Kuba.

Kwenye barua hiyo Bi. Kuba alisema, "Daktari Jiang, wewe ni uliokoa maisha yangu. Nakutumia kadi hiii ya salamu, na kutumaini kuwa wewe utapokea shukrani na heshima zangu za dhati."

Akiwa kiongozi wa kikundi cha 11 cha madaktari wa China nchini Sierra Leone Bw. Jiang Songquan aliposoma barua hiyo alisisimka sana, na alikumbuka jinsi alivyokuwa akifanya kazi nchini Sierra Leone katika miaka miwili iliyopita.

Tarehe 14 mwezi Julai, mwaka 2003, baada ya kupewa mafunzo kwa miezi mitatu, kikundi cha madakatari 9 kilichoongozwa na Bw. Jiang Songquan kiliwasili kwenye hospitali iliyoko karibu na Freetown, mji mkuu wa Sierra Leone.

Walipokuwa wanafika kwenye mlango wa hospitali, Bw. Jiang Songquan na msafara wake walizungukwa na wenyeji wa huko. Mkuu wa hospitali hiyo Bw. Kanu aliyewakaribisha madaktari hao wa China, aliwaambia kwa lugha ya kichina kuwa: Watu hao wote wanagombea kutaka kutibiwa."

Kati ya wagonjwa hao, mwanamume ambaye uso wake unaonekana hana afya nzuri alimvutia Bw. Jiang. Mwanamume huyo kijana anaitwa Kubebapi, mke wake mwenye umri wa miaka 31 Bi. Kuba alikuwa ameumwa kwa miaka kadhaa, na alikuwa anajisikia ganzi kwenye mikono na miguu yake, kichwa chake huhisi kizunguzungu na alikuwa analazwa kitandani na maisha yake yalikuwa hatarini.

Bw. Jiang Songquan na mwuguzi walimtembelea Bi. Kuba mara moja. Baada ya kuthibitisha hali yake ya ugonjwa, Bw. Jiang Songquan alichukua hatua mbalimbali za kuhimiza mzunguko wa damu mwilini mwake zikiwemo kufanya akyupancha na kumchoma sindano. Usiku huo, hali ya Bi. Kuba ilikuwa imekuwa nzuri zaidi. Baada ya hapo, Bw. Jiang Songquan alimpa dawa za kutumia kwa wiki moja bila malipo.

Baada ya siku tatu, Bibi Kuba ambaye hali yake ilikuwa inabadilika kuwa nzuri zaidi, alichukua kikapu cha maua na kwenda ofisi ya Bw. Jiang Songquan kutoa shukrani kwake, na kuwasifu madaktari wa Chinakuwa madaktari hodari.

Bi. Kuba hakuweza kukisindikiza kikundi cha madaktari wa China kilipoondoka kutoka Sierra Leone, hivyo alikwenda kwenye ubalozi wa China nchini humo na kupata anwani ya Bw. Jiang, na kumwandikia barua.

Tarehe 3 Januari mwaka 2004, Bw. Jiang Songquan alipata taarifa kutoka Ubalozi wa China nchini Sierra Leone, ikisema kuwa rais Ahmad Tejan Kabbah alikuwa anaumwa na mgongo na kiuno kutokana na uchovu wa kupita kiasi, na kumwambia aende kumfanyia ukaguzi na kumpa matibabu.

Bw. Jiang aliona ni jukumu kubwa kufanya kazi ya kumtibu rais. Baada ya Bw. Jiang na msaidizi wake kufikia Ikulu, walimfanyia rais ukaguzi kwa makini, na walichukua hatua mfululizo na kuanza kumtibu kwa utaratibu.

Baada ya matibabu ya wiki moja, hali ya rais Kabbah ilikuwa imekuwa nzuri zaidi. Usiku huo, wakati Bw. Jiang Songquan na wasaidizi wake walipoondoka kutoka Ikulu, Rais Kabbah aliyekuwa amepona alimsindikiza Bw. Jiang Songquan na kuburudika katika mandhari nzuri ya usiku ya mji wa Freetown, na baada ya hapo, Bw. Jiang alikuwa anatembelea Ikulu mara kwa mara.

Katika muda wa zaidi ya miaka miwili alipokuwa akifanya kazi nchini Sierra Leone, Daktari Jiang na wenzake walikuwa wameondoa matatizo mbalimbali, na kufanikiwa kuwafanyia upasuaji mamia ya wagonjwa wa huko kila mwaka, na kuwaokoa wagonjwa zaidi ya 500 wenye hali mbaya.

Kikundi cha madaktari wa China kiliunda urafiki mkubwa na hospitali ya Sierra Leone. Kila ilipofika sikukuu, wenyeji wa huko walikuwa wakiwapa matunda na zawadi, ili kutoa shukurani na heshima zao.

Mwezi Julai mwaka 2005, kazi ya utoaji wa huduma iliyofanyika kwa miaka miwili ilikuwa inamalizika. Baada ya kikundi cha madaktari wa China kuandaa kurudi nchini China, wananchi wa Sierra Leone waliwaaga madaktari wa China kwa njia mbalimbali.

Tarehe 25 Julai, siku ambapo kikundi cha madaktari wa China kilipokuwa kinaondoka kwenye uwanja wa ndege huko Freetown, mji mkuu wa Sierra Leone, maelfu ya watu waliwasindikiza kwenye uwanja wa ndege. Kati ya watu hao, wengi walikuwa wagonjwa waliotibiwa na madaktari wa China na jamaa zao za wagonjwa hao. Walipeleka matunda mabichi, kadi za salamu, na kubeba mabango yenye maneno "tunawatakia safari njema madaktari wa China" na "tunashukuru kwa huduma bora za madaktari wa China." Bw. Jiang akikumbuka hayo alisema, daima hatasahau hali hiyo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-12-09