Mikutano kadha wa kadha ya Umoja wa Asia kusini mashariki imefunguliwa tarehe 12 huko Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia. China ikiwa mshiriki muhimu wa mikutano hiyo, maendeleo yake ya haraka yataleta athari gani kwa nchi majirani yake, hili limekuwa ni suala moja linalofuatiliwa sana na pande mbalimbali.
Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao siku hiyo ametoa hotuba kuhusu "Maendeleo ya kiamani ya China na fursa ya Asia ya kati", ambapo amesema, maendeleo ya China si kama tu yamewanufaisha wananchi wa China wapatao bilioni 1.3, pia yameleta fursa nyingi kwa nchi za Asia ya mashariki.
Katika hotuba aliyotoa kwa wanaviwanda, wanakampuni na wafanyabiashara wa nchi mbalimbali za Umoja wa Asia ya kusini mashariki wapatao zaidi ya 600, Bwana Wen Jiabao kwanza amesema, katika hali ya utandawazi wa uchumi na pilikapilika za mapinduzi ya kisayansi na kiteknolojia duniani, Asia ya mashariki inakabiliwa na fursa ya kihistoria ya kutimiza maendeleo ya kuruka hatua, lakini wakati huo huo hatari zinazoyakabili maendeleo ya uchumi pia zinaongezeka. Akidhihirisha alisema:
Kwa ujumla, kiwango cha utandawazi wa viwanda cha sehemu nzima ya Asia ya mashariki bado kiko chini, miundo ya uchumi bado haijawa mwafaka, matatizo ya mazingira ya viumbe yamekuwa makubwa na dhahiri siku hadi siku, na hali isiyo ya uwiano imekuwepo katika maendeleo kati ya nchi na nchi ya sehemu hiyo, hivyo kutimiza maendeleo endelevu, maendeleo ya haraka na maendeleo yenye uwiano katika sehemu hiyo bado ni changamoto kubwa inayoikabili sehemu hiyo. Kutokana na kukabiliwa na hali mpya, tunapaswa kujumuisha maarifa na mafunzo kutokana na maendeleo ya Asia ya mashariki, na kujadili kwa pamoja maendeleo ya kimkakati yanayoweza kuipatia sehemu hiyo maendeleo ya haraka na mazuri zaidi.
Maendeleo ya China yataleta nini kwa sehemu hiyo, pia ni jambo linalofuatiliwa na watu wanaohudhuria mkutano. Bwana Wen Jiabao amejulisha hali ya maendeleo ya China, amesema baada ya kupata ongezeko la uchumi la asilimia 9.4 kwa mwaka kwa miaka kadhaa mfululizo, maendeleo ya China bado yako katika kipindi kipya cha kihistoria. Akisema:
Maendeleo ya China si kama tu yamenufaisha wananchi wa China wapatao bilioni 1.3 wa China, bali pia yameleta fursa nyingi zaidi kwa nchi za Asia ya mashariki. Katika miaka mitano ijayo, China itaagiza bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani zaidi ya trilioni 2 kutoka kwa nchi za Asia, asilimia 80 ya miradi inayowekezwa na mashirika ya China iko katika sehemu ya Asia, na kutokana na kuimarishwa kwa nguvu halisi ya mashirika ya China, China itaonesha umuhimu wake mkubwa zaidi katika kuhimiza ongezeko la uchumi wa kisehemu. Mwezi Julai mwaka huu, China imepiga hatua kubwa katika mageuzi ya utaratibu wa ubadilishaji wa fedha za Renminbi za China, na itaendelea kufanya hivyo katika siku zijazo.
Bwana Wen Jiabao pia amefahamisha wazi lengo la China la kufanya juhudi kushiriki kwenye ushirikiano na Asia ya kusini. Akisema:
China inafanya juhudi kushiriki kwenye ushirikiano na Asia ya mashariki, madhumuni yake ni kufanya ujirani mwema, kuleta usalama kwa nchi jirani na kupata maendeleo pamoja na nchi jirani. China inatumai kuhimiza amani na ustawi wa sehemu hiyo kwa kupitia ushirikiano, pia kujenga mazingira mazuri ya nje kwa ajili ya maendeleo yake.
Watu waliohudhuria mkutano huo wamesifu sana hotuba hiyo ya Bwana Wen Jiabao.
Idhaa ya Kiswahili 2005-12-12
|