Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-14 20:17:37    
Mkutano wa kwanza wa wakuu wa Asia ya mashariki wapitisha na kusaini "Taarifa ya Kuala Lumpur"

cri

Mkutano wa kwanza wa wakuu wa Asia ya mashariki tarehe 14 umefungwa huko Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia. Mkutano huo umepitisha na kusaini "Taarifa ya Kuala Lumpur", ikithibitisha mkutano huo uwe baraza la wakuu na Umoja wa Asia ya kusini mashariki ufanye kazi ya uelekezaji, na kukubali mkutano huo uoneshe umuhimu wake katika ujenzi wa umoja wa sehemu hiyo.

Wakuu wa nchi au serikali za nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki, Australia, China, India, Japan, Korea ya kusini na New Zealand walihudhuria mkutano huo wa kwanza wa Asia ya mashariki. Taarifa ya Kuala Lumpur iliyosainiwa kwenye mkutano huo imedhihirisha kuwa, mkutano wa wakuu wa Asia ya mashariki utakuwa baraza moja la ufunguaji mlango, lenye uwazi na kupokea maoni mbalimbali kutoka nje, ambapo Umoja wa Asia ya kusini mashariki utafanya kazi ya uelekezaji kwenye baraza hilo. Mkutano wa baraza hilo utaweka mkazo katika kufanya mazungumzo na ushirikiano kuhusu masuala ya siasa na usalama; kusukuma mbele maendeleo, utulivu wa fedha na usalama wa nishati katika sehemu ya Asia ya mashariki, kutimiza utandawazi wa uchumi na ongezeko la uchumi, kuondoa umaskini, kupunguza pengo la maendeleo, kuhimiza upanuzi wa biashara na uwekezaji na mchakato wa biashara huria; kuongeza uaminifu na mshikamano na kusukuma mbele ushirikiano katika hifadhi ya mazingira, kukinga maradhi ya maambukizi na kupunguza maafa.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, washika wa mkutano wa wakuu wa Asia ya mashariki wanapaswa kulingana na kigezo kilichowekwa na Umoja wa Asia ya kusini mashariki, yaani wana uhusiano halisi na Umoja wa Asia ya kusini mashariki, ni wenzi wa mazungumzo na umoja huo, tena wameshajiunga na "Mkataba wa urafiki na ushirikiano wa Asia ya kusini mashariki. Taarifa hiyo imedhihirisha kuwa, mkutano wa wakuu wa Asia ya mashariki utafanyika kila baada ya muda, na utaendeshwa na nchi mwenyekiti wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki, na utafanyika wakati mmoja na mkutano wa wakuu wa mwaka wa Umoja wa Asia ya kusini mashariki.

Aidha mkutano huo pia umetoa taarifa kuhusu kukinga, kudhibiti na kukabiliana na homa ya mafua ya ndege. Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao tarehe 14 ametoa hotuba kwenye mkutano wa kwanza wa wakuu wa Asia ya mashariki, akisema China inapinga sera ya kujifungia na kutengana na nyingine ama kulenga upande wowote maalum katika ushirikiano wa Asia ya mashariki. China kamwe haitatafuta hadhi ya uongozi katika sehemu hiyo. Bwana Wen Jiabao alisema, China inapendekeza kushikilia wazo la ufunguaji mlango katika ushirikiano wa kikanda. China inaendelea kuunga mkono Umoja wa Asia ya kusini mashariki uoneshe umuhimu wake wa uelekezaji katika ushirikiano wa Asia ya mashariki, pia inatumai kuwa maslahi halali katika sehemu ya Asia mashariki ziliyo nayo nchi zilizo nje ya sehemu hiyo. Bwana Wen Jiabao pia amesema China inatarajia kujiunga na India, Australia na New Zealand katika kusukuma mbele kwa pamoja mambo makuu ya maendeleo na ushirikiano ya Asia ya mashariki, kuikaribisha Russia ijiunge na Baraza la wakuu wa Asia ya mashariki, pia kukaribisha Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi na jumuiya nyingine zilizo nje ya sehemu hiyo zianzishe mawasiliano na Asia ya mashariki.

Wachambuzi wanaona kuwa, mkutano wa kwanza wa Asia ya mashariki umeonesha matumaini ya pamoja ya nchi za Asia ya mashariki kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kikanda, na pia kuonesha tena athari ya Asia ya mashariki inayozidi kuongezeka duniani siku hadi siku. Lakini mchakato wa utandawazi umeanzishwa kwa hatua ya kwanza tu, bado itakabiliwa na changamoto nyingi katika njia yake ndefu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-12-14