Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-14 20:25:28    
Mafunzo ya kazi za kiufundi yanapamba moto nchini China

cri

Katika muda mrefu uliopita, wachina wengi walikuwa wanathamini na kupendelea zaidi elimu ya juu bila sababu yoyote ya msingi na kudharau kazi za kiufundi. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, hali hiyo imebadilika, na mafunzo ya kazi za kiufundi yameanza kupamba moto nchini China.

Kuna shule za aina mbili zinazotoa mafunzo ya kazi za kiufundi nchini China, yaani sekondari za juu za mafunzo ya kazi za kiufundi na vyuo vya mafunzo ya kazi za kiufundi. Gao Zhong mwenye umri wa miaka 20 anajifunza teknolojia za kompyuta kwenye chuo cha mafunzo ya kazi za kiufundi cha Beijing. Alisema:

"naona wanafunzi wa shule za mafunzo ya kazi za kiufundi wanalingana zaidi na hali ya ajira ya hivi sasa, watu wenye uwezo ambao waliwahi kuwa na uzoefu wanahitajika sana hivi sasa, na wala sio wale wenye elimu ya juu peke yake."

Gao Zhong alisema kuwa, asilimia 90 ya wanafunzi waliohitimu kutoka chuo hicho mwaka huu wamepata ajira, ikiwa imezidi kwa kiasi kikubwa asilimia 72 ambayo ni kiasi cha wastani cha wanafunzi wa vyuo vikuu waliopata ajira. Alisema, wanafunzi wenzake wengi wamepata kwa urahisi ajira yenye mapato makubwa. Kuhusu hali hiyo, wachambuzi wameainisha kuwa, hivi sasa wafanyakazi wenye ustadi wa kazi za kiufundi wanahitajika zaidi kutokana na maendeleo ya uchumi na jamii ya China. Hivi sasa, makampuni mengi maarufu duniani yameanzisha viwanda hata taasisi za utafiti nchini China, na China pia inajitahidi kutengeneza bidhaa kwa teknolojia zaidi, ili kuinua uwezo wake wa ushindani wa bidhaa hizo kwenye soko la kimataifa. Hali hiyo inahitaji wafanyakazi wengi wenye ujuzi maalum na uzoefu wa kazi. Aidha, pato la wafanyakazi kama hao pia linaongezeka siku hadi siku. Kutokana na hali hiyo, katika miaka ya hivi karibuni, mafunzo ya kazi za kiufundi yameanza kupamba moto nchini China.

Serikali ya China pia inazingatia umaalmu wa kuendeleza mafunzo ya kazi za kiufundi, waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao kwenye mkutano husika uliofanyika hivi karibuni aliainisha,

"sekta mbalimbali za uchumi wa taifa si kama tu zinahitaji wanasayansi, wahandisi na wataalamu wa usimamizi, bali pia zinahitaji mamilioni ya wataalamu wenye ustadi wa juu na wafanyakazi wenye uwezo mkubwa. Ni kundi la nguvu kazi kama hilo tu litaweza kubadilisha sanyasi na tekenolojia na vifaa vya kisasa kuwa uwezo halisi wa uzalishaji mali."

Kutokana na hali hiyo, katika miaka ya hivi karibuni, China imechukua hatua mbalimbali kusukuma mbele maendeleo ya mafunzo ya kazi za kiufundi, kwa mfano, kuongeza mapato, kuboresha vifaa na miundombinu ya shule za mafunzo ya kazi, kuanzisha ushirikiano wa kimataifa na kujifunza kutokana na uzoefu wa nchi za nje, kutilia maanani kuongeza uwezo wa wanafunzi kufanya uzoefu wa kazi na kuweka masomo kutokana na mahitaji ya jamii.

Chuo cha mafunzo ya kazi za kiufundi cha Beijing zamani kilikuwa na vitivo na kozi chache, lakini katika miaka ya hivi karibuni, chuo kilirekebisha mpango huo na kuweka vitivo na kozi kutokana na mahitaji halisi ya jamii. Mwalimu wa chuo hicho Bw. Ren Fengguo alieleza:

"Chuo chetu kinaweka vitivo na kozi kutokana mahitaji halisi ya jamii, na mpango huo wenye malengo umeshaleta manufaa."

Chuo hicho kina vitivo 6 vya uhandisi wa mitambo na eleketroniki (mechanical & electronic engineering), uhandisi wa upashanaji habari, uhandisi wa ujenzi, na kozi zaidi ya 30. hivi sasa chuo hicho kina wanafunzi zaidi ya elfu sita.

Kwa jumla, mafunzo ya kazi za kiufundi yanapiga hatua kwa haraka kote nchini China. Idadi ya wanafunzi walioandikishwa katika sekondari za mafunzo ya kazi za kiufundi mwaka huu imeongezeka kwa milioni moja kuliko mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18; na idadi ya wanafunzi walioandikishwa katika vyuo vya mafunzo ya kazi za kiufundi pia imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 8. hivi sasa kuna shule hizo zaidi ya elfu 15 zenye wanafunzi zaidi ya milioni 2 kote nchini China.

Naibu waziri wa elimu wa China Bi. Wu Qidi aliainisha kuwa, katika siku za baadaye China itaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuharakisha maendeleo ya mafunzo ya kazi za kiufundi. Alieleza:

"inapaswa kuendeleza kwa nguvu mafunzo ya kazi za kiufundi, hasa kuichukulia kuwa kazi muhimu ya kimkakati ya elimu katika kipindi kijacho, na kuichukulia shughuli ya kupanua elimu hiyo kuwa lengo muhimu la elimu katika mpango wa 11 wa maendeleo wa miaka mitano. Mwaka kesho shule za mafunzo ya kazi za kiufundi zitaandikisha wanafunzi milioni moja, na kuifanya idadi ya wanafunzi wa shule hizo ifikie milioni 8 baada ya miaka michache, ikiwa inafanana na shule za sekondari za kawaida."

Imefahamika kuwa, katika miaka mitano ijayo serikali kuu ya China peke yake itatenga yuan za Renminbi milioni moja katika elimu hiyo, na kupanga kutoa mafunzo ya kazi za kiufundi kwa wanafunzi vijana, kutoa mafunzo ya kazi kwa wafanyakazi mijini, nguvukazi ya watu kutoka vijijini wanaofanya kazi mijini na wakulima.