Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-14 20:33:25    
Dawa za mitishamba ya kichina zinafanya kazi kubwa katika utaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano vijijini

cri

Hivi karibuni naibu waziri wa afya Bw. She Jing kwenye mkutano wa utekelezaji wa kazi ya majaribio ya utaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano vijijini na dawa za mitishamba ya kichina vijijini alisema kuwa, kutumia dawa za mitishamba ya kichina, hasa kutumia teknolojia mwafaka ya dawa za mitishamba ya kichina yenye bei nafuu, ambayo ufanisi wake ni mzuri na salama, kunaweza kupunguza gharama za matibabu kwa wakulima, na kutoa mchango katika kutatua tatizo la wakulima kuwa maskini kutokana na maradhi.

Idara ya taifa ya usimamizi wa dawa za mitishamba ya kichina imegundua kuwa, katika sehemu nyingi za China hasa katika sehemu zenye watu wengi maskini gharama za dawa za mitishamba ya kichina zinazokubaliwa na wakulima kwa wastani ni Yuan za RMB 6 hadi 8, na gharama za zahanati kwa kila mtu kwa wastani ni ndogo kwa asilimia 20 hadi 30 kuliko dawa za magharibi. Kwenye mkutano huo Bw. She Jing alisema kuwa, bei nafuu za dawa za mitishamba ya kichina na matumizi ya teknolojia mwafaka ya dawa za mitishama ya kichina yamepunguza gharama za matibabu kwa wakulima wanaoshiriki kwenye matibabu ya ushirikiano, pia yamepunguza utoaji wa fedha za utaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano. Alisema hatua hii sio tu inakaribishwa sana na wakulima hao, bali pia inatiliwa maanani na serikali ya ngazi mbalimbali na sekta mbalimbali za jamii.

Bw. She Jing amesema majaribio hayo yamethibitisha kwamba dawa za mitishamba ya kichina zinafanya kazi kubwa katika kazi ya majaribio ya utaratibu mpya wa matibabu ya ushirikiano, pia zina uwezo mkubwa, vilevile kazi ya majaribio imetoa fursa nzuri kwa kazi ya dawa za mitishamba ya kichina vijijini.

Idhaa ya Kiswahili 2005-12-14