Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-14 20:50:25    
Mapishi ya supu ya figili na samaki

cri

Mahitaji

Samaki mmoja, figili gramu 400, chaza gramu 300, kiasi kidogo cha vitunguu maji, tangawizi, giligilani, chumvi na pilipili manga, na mvinyo wa kupikia kijiko kimoja.

Njia

1. osha samaki, figili, na kata figili. Weka chaza kwenye maji yenye chumvi kwa saa mbili.

2?pasha moto, tia mafuta kwenye sufuria halafu tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, halafu tia samaki kwenye sufuria mkaange, mimina mvinyo wa kupikia, na maji vikombe sita, baada ya kuchemka punguza moto kidogo na endelea kuchemsha kwa dakika 5, tia figili, endelea kuchemsha na tia chaza, baada ya chaza iive tia chumvi na pilipili manga korogakoroga, ipakue. Weka giligilani katika supu hiyo. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari kuliwa.