Mkutano wa kwanza wa wakuu wa Asia ya mashariki ulifungwa tarehe 14 huko Kuala Lumpur, ambapo mikutano ya wakuu ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki pia inakaribia kumalizika. Kwenye mikutano mfululizo iliyofanyika huko, waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao alitoa mapendekezo na wazo kuhusu ushirikiano ambayo inaonesha sera ya kidiplomasia ya China kuhusu ujirani mwema, usalama na ustawi wa sehemu ya nchi majirani.
Kupanua ushirikiano kati ya China na Umoja wa Asia ya kusini mashariki ni pendekezo muhimu alilotoa Bwana Wen Jiabao kwenye mikutano mbalimbali. China imechukuliwa na nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki kuwa ni nguvu muhimu ya kusukuma mbele ongezeko la uchumi wa sehemu ya Asia ya kusini mashariki. China si kama tu imeanzisha uhusiano wa kimkakati na kiwenzi na nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki, bali pia itakuwa mwenzi wa maendeleo ya sehemu ya mashariki ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki; pande hizo mbili pia zinahimiza kuanzisha sehemu ya biashara huria . Hivyo kwenye mikutano mbalimbali, Bwana Wen Jiabao alipotoa hotuba alifahamisha hali ya maendeleo ya China na masuala yanayoikabili China, ambapo ameeleza wazi kuwa China haiwezi kujiendeleza tu, inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali za Asia ya mashariki hasa nchi mbalimbali za Umoja wa Asia ya kusini kwa ajili ya kupata maendeleo na ustawi wa pamoja. Bwana Wen Jiabao ametoa mapendekezo mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya China na Umoja wa Asia ya kusini mashariki kwenye sekta 5 muhimu za mawasiliano, nishati, utamaduni, utalii na afya za umma, na kujadili uwezekano wa kuanzisha njia kubwa ya upashanaji habari kati ya China na Umoja wa Asia ya kusini mashariki; kusameheana viza za kidiplomasia na mambo ya kiserikali ndani ya mwaka kesho; kuitisha mkutano wa mawaziri wa China na nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki kuhusu magonjwa mapya ya maambukizi, ili kujadili hasa kinga na tiba ya homa ya mafua ya ndege, na utafiti na utengenezaji wa chanjo za mafua ya ndege. Mapendekezo hayo yamefuatiliwa siku hizi kwenye vyombo vya habari vya nchi mbalimbali.
Kwenye mkutano wa wakuu wa nchi 10 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki pamoja na nchi tatu za China, Japan na Korea ya kusini, Bwana Wen Jiabao ameahidi zaidi kuwa China itaongeza mikopo yenye riba nafuu ya dola za kimarekani bilioni 5 kwa kuunga mkono mashirika ya China katika miradi yao ya uwekezaji katika nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki. Bwana Wen Jiabao ametangaza kuwa uungaji mkono wa China kwa Umoja wa Asia ya kusini mashariki ni wa dhati na wa kunufaishana, pia ni kwa ajili ya kupata maendeleo ya pamoja bila sharti lolote la kisiasa, hakika China itatimiza ahadi yake hiyo. Aidha Bwana Wen Jiabao pia amependekeza nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki pamoja na China, Japan na Korea ya kusini ziimarishe ushirikiano katika sekta za usalama, nishati, kuwasaidia watu maskini kujiendeleza, utamaduni na elimu, kukabiliana na maafa makubwa na matukio ya dharura. Amedhihirisha wazi kuwa, China itaendelea kuunga mkono Umoja wa Asia ya kusini uoneshe umuhimu wake wa uelekelezaji, pia kupendekeza China, Japan na Korea ya kusini ziongeze usawazishaji na kila upande uoneshe nguvu zake bora na umuhimu wake.
Mapendekezo aliyotoa Bwana Wen Jiabao kwenye mikutano mbalimbali huko Kuala Lumpur yamesifiwa na nchi mbalimbali. Vyombo vya habari vya Kuala Lumpur viliisifu China kuwa ni "mwanzilishi wa harakati za amani, urafiki na ushirikiano wa sehemu hiyo". Nchi majirani za China zinatarajia kushirikiana na China katika kutekeleza mapendekezo ya Bwana Wen Jiabao ili kunufaika pamoja matokeo ya maendeleo ya China na kupata ustawi na maendeleo kwa pamoja.
|