Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-19 15:50:57    
Kwenda kwenye mji mdogo Tongli uliozungukwa na mito

cri

Mkoani Jiangsu, mashariki ya China kuna mji mdogo wa kale unaoitwa Tongli ambao umezungukwa na mito. Mji huo uko umbali wa kilomita zaidi ya 10 tu toka Suzhou, mji maarufu wenye vivutio vya utalii nchini China. Mji huo una historia ya zaidi ya miaka 1000, ni mji wa kale unaohifadhiwa vizuri zaidi mkoani Jiangsu kwa hivi sasa. Mji huo uko kwenye kando ya mashariki ya Ziwa Taihu, ambapo umegawanywa na mito iliyo kama wavu, mjini humo majengo yote yalijengwa kwa kuegemea mito, mji huo unaonekana kama lulu iliyoko kwenye maji.

Mwenyeji wa mji huo Bwana Zhang Fusheng ametuambia kuwa, katika mji wa Tongli wenye mito mingi, hakika kuna madaraja mengi. Akisema:

Mjini Tongli, tunaweza kusema kila familia inakaribiana na mto, ambapo watu wanaweza kupanda ngalawa kwenda popote mjini. Kila ukienda mjini, unaweza kuona mito. Ingawa mji huo una eneo dogo, lakini mito midogo 15 inapita mji huo, na mito hiyo imegawanya mji kuwa visiwa 7 vidogo, na visiwa hivyo vimeunganishwa kuwa sehemu moja nzima kwa kutegemea madaraja ya kale zaidi ya 40.

Kama alivyosema Bwana Zhang, mjini Tongli, njia na mito inakwenda sambamba, madaraja na njia pia zinafungamana, ukitembea mjini, si muda mrefu utapita madaraja kadha wa kadha. Miongoni mwa madaraja hayo, kuna daraja moja la kale zaidi kuliko mengine linaloitwa "Siben", ambalo lilijengwa zaidi ya miaka 700 iliyopita, ingawa daraja hilo limekabiliana na mvua na upepo kwa miaka mingi iliyopita, lakini daraja hilo bado ni la imara sana; daraja lingine dogo linalopendeza linaitwa "Dubu", urefu wake haufikii mita 2, upana wake ni chini ya mita moja; watu wawili wakikutana kwenye daraja hilo, hawawezi kupita bila kugeuza mwili.

Mwongoza watalii Bi.Wang Qiao alituambia kuwa, kati ya madaraja yote mjini Tongli, daraja la "Fuguan" ni lenye miujiza zaidi. Hadithi moja ya China ilisema kuwa, kama samaki wa aina ya syprinoid ataweza kuruka juu kwa kupita poromoko moja liitwalo "Mlango wa dragon", basi samaki wa huyo aina ya cyprinoid atabadilika kuwa dragon na kuingia dunia ya peponi. Inasemekana kuwa, huko Tongli alikuwepo samaki mmoja aina ya cyprinoid aliyelichukulia "Daraja la Fuguan" kuwa ni "Mlango wa dragon" akiruka juu ya daraja hilo kujaribu bahati yake.

Bi.Wang alisema kwenye daraja la Fuguan kuna mchongo wa mawe kuhusu samaki aliyeruka mlango wa dragon na kuwa dragon anayeingia peponi, mchongo huo unatokana na hadithi ya zamani. Hadithi hiyo ilisema kuwa, siku moja ya mwezi Machi wakati maua ya mpichi yalipochanua, samaki mmoja aina ya cyprinoid alitaka kujaribu kuruka juu ya mlango wa dragon ili aingie peponi, lakini aliporuka kwa nguvu kubwa alivutiwa na msichana mmoja mrembo aliyekuwa anapita kwenye daraja hilo, bahati mbaya samaki huyo aliruka hadi nusu ya mlango wa dragon, ambapo kichwa cha samaki kiligeuka kuwa kichwa cha dragon, lakini mwili wake bado ulibaki kwa wa samaki.

Mjini Tongli, mbali na madaraja mengi ya kale, bado kuna nyumba nyingi zilizojengwa zamani ambazo zinastahili kutazamwa na watu. Mjini humo, zaidi ya asilimia 40 ya majengo yamekuwa na historia ya zaidi ya miaka mia moja, hasa nyumba kubwa kadha wa kadha zilizopambwa kwa nakshi za aina mbalimbali za mbao au michongo ya matofali, mtindo wa kale wa nyumba hizo ulionekana dhahiri. Mtaalamu maarufu wa China kuhusu elimu ya ujenzi wa mabustani Bwana Chen Congzhou alisifu mji Tongli kama ni Jumba la makumbusho ya majengo ya zama za kale.

Bustani la Tuisiyuan mjini Tongli ni bustani iliyoorodheshwa na Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa kuwa ni mali ya urithi wa utamaduni duniani.

Bustani la Tuisiyuan ilikuwa bustani la binafsi lililojengwa na diwani mmoja wa Enzi ya Qing ya kale ya China, aliyerudi kwenye maskani yake baada ya kuondolewa wadhifa. Bustani hilo lilijengwa katika karne ya 19. Diwani huyo aliyeondolewa wadhifa alipojenga bustani hiyo, alikuwa anataka kuonesha wazo lake la kupumzika nyumbani kwa kujikosoa, hivyo maumbo ya jumla ya bustani la Tuisyuan yanaonekana karibu kama jengo la kawaida, siyo sawasawa na mabustani mengine yaliyojengwa na madiwani wengine wa zama za kale ambayo huonesha zaidi hali ya anasa kutokana na wazo la kupenda kuonesha makuu na utajiri walio nao madiwani hao waliokuwa madarakani.

Bustani la Tuisiyuan ni ndogo sana, eneo lake ni hekta 0.6 tu, lakini wasanifu wa bustani hilo walizingatia umaalum wa sehemu iliyoko kusini mwa Mto Changjiang, walisanifu kwa ustadi mzuri, maumbo ya bustani hilo yanaonekana kuwa na hali mbalimbali tofauti na mabadiliko ya aina mbalimbali. Ndani ya bustani, eneo la maji limechukua nusu zaidi ya eneo la bustani, vibanda mbalimbali vya kupendeza vimetapakaa kando ya maji, jinsi vilivyo ni kama vinaelea juu ya maji. Kila sehemu ya bustani hilo ina mandhari yake pekee, lakini sehemu zote zinaungana na kuonekana kwa pamoja kwa kuambatana na miti, maua, kando ya dimbwi inayozungukazunguka. Maumbo ya bustani hiyo yanaonekana kama ya kimaumbile, bustani hilo inastahili kusifiwa kuwa ni bustani murua kabisa miongoni mwa mabustani mengi binafsi nchini China.

Mtalii Bi. Li Lu alituambia kuwa, Bustani la Tuisyuan ni yenye hali nzuri ya utulivu na usafi, inaweza kumfanya kama akae katika sehemu iliyo nje ya dunia, alisema:

Nimewahi kutembelea mabustani mengi katika sehemu za kusini mwa Mto Changjiang, lakini naipenda zaidi bustani la Tuisyuan, kwani nikitembelea bustani hiyo, najisikia utulivu na starehe zaidi.

Mji mdogo Tongli unaonekana ni mji mdogo wa kawaida lakini unawavutia watu kama mtindo ulivyo wa Bustani la Tuisiyuan. Kwenye magulio yaliyoko kote mjini, hakuna makelele, mtindo pekee wa mji Tongli unaonekana dhahiri pote mjini.

Idhaa ya kiswahili 2005-12-19