Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-20 16:04:13    
Baraza la wakuu wa miji mikubwa kiasi na midogo lafanyika mjini Beijing kujadili maendeleo endelevu

cri

"Kuendeleza uchumi kisayansi?kubana matumizi ya nishati, na kupata maendeleo endelevu" ni mada iliyopewa kipaumbele katika baraza la pili la wakuu wa miji mikubwa kiasi na midogo lililofanyika tarehe 16 katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kwa lengo la kubadilisha namna ya kuendeleza uchumi, kubadilishana maoni kati ya viongozi wa miji na wataalamu ili kuhimiza kubana matumizi ya nishati, kuinua tija ya uzalishaji mali na kutumia maliasili kwa marudio na kuhakikisha maendeleo endelevu yanapatikana.

Mkutano mkuu wa tano wa Kamati Kuu ya 16 ya Chama cha Kikomunisti cha China ulisema kwamba, wazo la kuendeleza uchumi kisayansi liwe linatawala katika shughuli za kuendeleza uchumi wa taifa, na kugeuza namna ya kuendeleza uchumi kwa juhudi na kuharakisha aina ya uchumi unaoongezeka kwa kutumia nishati mfululizo na kujenga jamii inayobana matumizi ya nishati na yenye mazingira bora. Mkutano huo wa tano pia ulitoa wito wa kupunguza matumizi ya nishati kwa kiasi cha asilimia 20 katika kipindi cha "mpango wa 11 wa miaka mitano wa maendeleo ya uchumi wa taifa". Lakini namna ya kufikia lengo hilo na ni matatizo gani yanaweza kutokea katika kutimiza lengo hilo, ni suala linalofuatiliwa sana.

Baraza hilo ambalo liliandaliwa na kituo cha utafiti wa maendeleo ya uchumi na mazingira ya miji katika Taasisi ya Sayansi ya Jamii ya China na Kamati ya Maendeleo ya Miji Mikubwa Kiasi na Midogo katika Taasisi ya Uchumi wa Miji ya China, lilijadili mambo matatu muhimu: Kwanza, namna ya kuendeleza uchumi kwa ulinganifu kati ya miji na kanda, kutatua matatizo yaliyokosa ulinganifu katika maendeleo ya uchumi ya miji na namna ya kugeuza njia ya sasa ya kuendeleza uchumi kwa kutumia nishati nyingi na kupata tija ndogo, na namna ya kuinua tija ya uzalishaji mali. Pili ni kutatua tatizo ambalo uwekezaji mkubwa unaotoa uchafuzi mkubwa na tija ndogo, na namna ya kujenga miji yenye matumizi madogo ya nishati na kuzalisha mali nyingi, na viongozi wa serikali wawe na fikra sahihi za ufanisi wa uongozi. Tatu ni kikundi cha utafiti wa maendeleo ya uchumi kutangaza matokeo ya upimaji wa maendeleo ya uchumi ya miji mikubwa kiasi na midogo kwa kigezo cha kanuni zilizotajwa. Kigezo hicho cha kupima maendeleo ya uchumi badala ya kigezo cha ongezeko la pato la taifa inasaidia kutekeleza itikadi ya kuendeleza uchumi kisayansi.

Kwenye baraza hilo, baadhi ya wataalamu walitoa maoni yao yenye thamani kuhusu uchumi unaoendelezwa kwa ulinganifu kati ya miji na kanda, kugeuza namna ya kuendeleza uchumi na namna ya kujenga miji inayotumia nishati kidogo na kuendeleza uchumi kwa mtindo wa kutumia nishati inayotumika tena. Viongozi wa miji mikubwa kiasi na midogo walieleza hatua na uzoefu wao wa namna ya kuifanya miji yao ielekee kwenye jamii inayobana matumizi ya nishati na mazingira bora.

Miji kumi mikubwa kiasi na midogo inayobana matumizi ya nishati ya kupigiwa mfano mwaka 2005, ilipendekezwa na wataalamu, na viongozi wa miji karibu mia moja walisaini "Tangazo la Kubana Matumizi ya Nishati".

Idhaa ya Kiswahili 2005-12-20