Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-20 20:02:14    
Maafa mengi yaliyotokea mwaka huu yatoa onyo kwa binadamu

cri

Tathmini iliyofanywa na shirika la hali ya hewa duniani kuhusu hali ya hewa kwa mwaka 2005 inawatia wasiwasi mkubwa watu duniani. Taarifa hiyo inasema mwaka 2005 ni mwaka ambo joto kali limetokea kwa uliotokea kwa mara ya pili joto kali, maafa mengine yakiwa ni pamoja na ukame, mafuriko na kimbunga pia yalikuwa mengi kuliko zamani. Maafa hayo yaliyotokea mara kwa mara duniani siyo tu kwamba yalileta hasara kubwa ya kiuchumi kwa nchi na sehemu zilizokumbwa na maafa ya kimaumbile, bali pia yalileta majeraha makubwa mioyoni mwa watu. Maafa ya kimaumbile yametoa onyo kali kwa binadamu kwa maafa.

Watu bado wanakumbuka sana tetemeko la ardhi na tsunami vilivyotokea kwenye pwani ya bahari ya Hindi ya Asia ya kusini mashariki mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu ambavyo viliua watu laki 2.75 katika dakika chache tu na kuwa moja ya matetemeko ya ardhi makubwa kabisa kuwahi kutokea katika miaka zaidi ya 100 iliyopita. Na katika siku za kukaribia mwisho wa mwaka huu, dhoruba kali iliyopeperusha theluji na hewa ya baridi kali vilizikumba nchi za Ulaya??

Taarifa iliyotolewa mwezi Desemba na shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani inasema, mabadiliko ya hali ya hewa yaliyotokea mwaka 2005 yalikuwa makubwa zaidi kuliko miaka ya nyuma: Mwaka 2005 ulikuwa na joto kali zaidi kuliko miaka ya nyuma, ambapo barafu nyingi zilizoko kwenye ncha ya kaskazini ya dunia ziliyeyuka, kimbunga kilitokea kwenye bahari ya Atlantiki na ujoto wa maji ya bahari ya Caribbean ulikuwa wa kiwango cha juu. Aidha, sehemu zote za mtiririko wa mto Amazon zilikumbwa na ukame mkubwa zaidi kuliko miaka yote iliyopita. Ingawa baadhi ya mambo yaliyosababisha maafa hayo yalikuwa ya kimaumbile, lakini ukweli ni kwamba vitendo vingi vya binadamu vinavyokiuka kanuni za kimaumbile na kuharibu uhusiano wa kutegemeana kwa viumbe, yalikuwa chanzo muhimu cha maafa hayo, hususan ongezeko la utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto limezidisha ujoto wa dunia. Mshauri wa suala la mabadiliko ya hali ya hewa ya dunia wa Umoja wa Mataifa aliye mtaalamu wa hali ya hewa ya dunia Bw. Mohammad Reza Salamat alitoa onyo akisema,

"Tukiangalia kwa makini, mwelekeo wa hali ya hewa ya dunia kubadilika kuwa joto kwa mfululizo na kasi ya mabadiliko hayo zinafanya watu kuwa na wasiwasi mkubwa."

Wanasayansi wamesema kutokana na kutumia ovyo rasilimali za dunia, uwezo wa kujikinga kwa mazingira ya asili umepungua, hivyo maafa yanatokea mara kwa mara na yamekuwa makali zaidi, matokeo yake ni kupungua kwa ubora wa mazingira ya kuishi kwa binadamu.

Mkurugenzi wa shirika la uratibu la upunguzaji wa maafa la Umoja wa Mataifa, Bw. Salvano Bricano alisema katika miaka 10 iliyopita, ubora wa mazingira ya kuishi kwa binadamu uliharibika zaidi kuliko zamani.

Kutokana na kukabiliwa na maafa makali ya kimaumbile, binadamu wameanza kuchukua hatua kuhifadhi mazingira yao ya kuishi. Mwishoni mwa mwaka 2005, wawakilishi zaidi ya elfu 10 kutoka nchi karibu 190 walishiriki kwenye mkutano wa 11 wa nchi zilizosaini "mkataba wa kanuni wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa" uliofanyika huko Montréal, Canada ili kujadili mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika karne ya 21.

Ofisa husika amesema kuwa kutumia silaha ya sayansi na kujenga mfumo mwafaka wa kupunguza maafa ya kimaumbile katika dunia, kutasaidia jamii ya binadamu kukabiliana na maafa ya kimaumbile.

Idhaa ya Kiswahili 2005-12-20