Mkutano mkuu wa 60 wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama tarehe 20 ulipitisha azimio la kuanzisha tume ya kujenga amani. Hii ni hatua inayochukuliwa na Umoja wa Mataifa kwa ili kusaidia sahemu na nchi, hasa nchi za Afrika, kupata amani ya kudumu baada ya migogoro ya vita. Hatua hiyo itasaidia utekelezaji wa "waraka wa matokeo" uliotolewa na mkutano wa viongozi wa dunia uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu baada ya "mfuko wa misaada ya dharura" uliokubaliwa kuanzishwa na mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wiki iliyopita.
Hapo awali ushauri wa kuanzisha tume hiyo ulitokana na wataalamu wa mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan aliukubali ushauri huo kwenye ripoti yake kuhusu mapendekezo ya mageuzi ya Umoja wa Mataifa katika mkutano mkuu wa 59. Mwezi Septemba mwaka huu, "waraka wa matokeo" uliotolewa na mkutano wa viongozi wa dunia kimsingi ulikubali ushauri huo wa kuanzisha tume hiyo mwishoni mwa mwaka huu.
Katika miaka mingi iliyopita, mashirika na idara nyingi za Umoja wa Mataifa zilikuwa zikijitahidi kusukuma mbele mchakato wa amani katika sehemu na nchi nyingi duniani, lakini kulikuwa hakuna idara maalumu ya kusimamia mchakato huo na kuhakikisha juhudi za kujenga amani zinaendelea. Hali ya juhudi za kujenga amani kusimama baada ya vita, imezifanya juhudi hizo kuwa kazi mara mbili. Na lengo la kuanzisha tume hiyo ni kwa ajili ya kuondoa hali hiyo.
Kwa mujibu wa azimio la tarehe 20 kazi ya tume hiyo ni kufuatilia hali ya nchi zilizowahi kukumbwa na migogoro ya vita ili kukwepa vita kuzuka tena kwa kufuata matakwa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo tume hiyo itatoa mkakati kamili wa utulivu, maendeleo ya uchumi na kutoa ushauri kwa ajili ya Umoja wa Mataifa kushiriki kwenye mashauriano, ili kuhakikisha nchi husika zinakamilisha kipindi cha mpito tokea hali ya kuwepo vita mpaka hadi amani.
Tume hiyo ina wajumbe 31 ikiwa ni pamoja na nchi saba wanachama wa Baraza la Usalama, nchi saba wanachama wa Baraza la Jamii ya Uchumi, ECOSOC, nchi tano zinazotoa ada na msaada mkubwa kwa Umoja wa Mataifa, nchi tano zinazotoa mchango mkubwa katika kulinda amani duniani na nchi saba zenye uzoefu mkubwa kwenye ukarabati wa taifa baada ya vita. Kwa mujibu wa maelezo ya mwenyekiti wa mkutano wa 60 wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson tume hiyo ni idara ya msaada chini ya Baraza la Usalama. Hii ni tume ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa.
Bw. Kofi Annan aliridhishwa na azimio la kuanzisha tume hiyo. Alisema kuanzishwa kwa tume hiyo kutasaidia sana juhudi za kujenga upya taifa baada ya vita. Aliona kuwa kuanzishwa kwa tume hiyo ni hatua yenye maana ya kihistoria, na sekretarieti ya Umoja wa Mataifa itaanzisha "ofisi ya kuunga mkono tume ya kujenga amani" ikisaidia kutoa habari na uchambuzi.
Idhaa ya Kiswahili 2005-12-21
|