Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-22 17:01:39    
Kitu muhimu kwa mazungumzo ya nyukilia kati ya Umoja wa Ulaya na Iran kiko wapi

cri

Maofisa wa ngazi ya juu wa Ufaransa, Uingereza na Ujerumani wanaowakilisha Umoja wa Ulaya na wa Iran, tarehe 21 huko Vienna walikuwa na mazungumzo ya kwanza rasmi kuhusu kurejeshwa kwa mazungumzo ya suala la nyukilia, ambayo yalisitishwa kwa miezi zaidi ya 4. Hali hiyo inaonesha kuwa si Umoja wa Ulaya wala Iran, zote zinatarajia kutatua suala la nyukilia la Iran kwa njia ya mazungumzo.

Viongozi wa idara ya siasa za wizara za mambo ya nje za nchi tatu za Ufaransa, Uingereza na Ujerumani pamoja na ofisa wa kamati ya usalama ya taifa ya Iran anayeshughulikia usalama wa kimataifa Bw. Javad Vaidi ,walishiriki kwenye mazungumzo hayo. Kiongozi wa idara ya siasa ya wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa Bw. Stanislas de Laboula alisema, mazungumzo hayo yalifanyika katika hali ya kufuatilia maendeleo na urafiki, pande mbili zilibadilishana maoni kwa uwazi na zimeamua kufanya mazungumzo mengine huko Vienna mwezi Januari mwaka kesho ili kuondoa tofauti ya maoni na kuthibitisha kanuni kwa mazungumzo ya pande mbili.

Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu, kutokana na Iran kurejesha shughuli za kusafisha uranium, Umoja wa Ulaya ulisimamisha mazungumzo ya nyukilia na Iran. Baada ya hapo Umoja wa Ulaya ulijisogeza kwa Marekani, kushauriana nayo mara kwa mara na kuchukua hatua za pamoja. Kutokana na kuongozwa na nchi hizo, Shirika la Nishati la Atomiki Duniani mwishoni mwa mwezi Septemba lilipitisha azimio kuhusu kuwasilisha suala la nyukilia la Iran kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa isipokuwa haikuthibitishwa tarehe kamili ya kuwasilisha azimio hilo. Kutokana na kukabiliwa na shinikizo, Iran licha ya kutotekeleza matakwa husika ya azimio, bali ilianza shughuli za usafishaji wa uranium za kundi la pili. Bunge la Iran nalo lilipitisha sheria ikitaka serikali isitishe hatua inayochukua yenyewe kwa muda ya kuacha usafishaji wa uranium wakati suala la nyukilia la Iran linapowasilishwa mbele ya baraza la usalama. Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran hivi karibuni amesaini sheria hiyo.

Ili kuvunja hali ya kukwama kwa mazungumzo ya suala la nyuklia la Iran, Russia ilitoa pendekezo moja la utatuzi ambalo liliwahi kukataliwa na nchi za magharibi, yaani kuiruhusu Iran ifanye shughuli za kiwango cha chini za uranium katika nchi hiyo, na kuhamisha kazi yake ya usafishaji wa uranium mzito nchini Russia. Kufanya hivyo kunaweza kuifanya Iran kuwa na haki ya matumizi ya kiamani ya nishati ya nyuklia, pia kunaweza kuondoa wasiwasi zilio nao nchi za magharibi juu ya mpango wa nyuklia wa Iran. Umoja wa Ulaya haukuwa na la kufanya, ila tu kuamua kukubali pendekezo la Russia baada ya kukubaliwa na Marekani. Lakini Iran ilikataa pendekezo hilo na kushikilia kufanya shughuli za usafishaji wa uranium nzito nchini mwake.

Vyombo vya habari vya Ulaya viliona kuwa, kukubali pendekezo la Russia kunamaanisha kuwa Umoja wa Ulaya Umeacha msimamo wake ulioshikilia siku zote kuhusu Iran lazima kuacha shughuli zake za usafirishaji wa uranium, ama sivyo mazungumzo yasingeweza kufufuliwa. Nchi za magharibi zimerudi nyuma sana kuhusu suala hilo tangu mgogoro utokee. Katika hali hiyo mkutano wa baraza la nishati ya atomiki duniani uliofanyika mwishoni mwa Novemba, uliamua kutowasilisha kwa muda suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama, na kutumai kuwa Umoja wa Ulaya na Iran zinaweza kufanya mazungumzo juu ya pendekezo la Russia.

Wachambuzi wanaona kuwa suala la kurejeshwa kwa shughuli za kusafisha uranium ni kiini cha mgongano kati ya Umoja wa Ulaya na Iran, na itakuwa mada muhimu itakayojadiliwa katika mazungumzo ya pande hizo mbili katika siku za baadaye.