Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-22 20:08:20    
Panchen Lama wa 11 amekuwa kiongozi anayeheshimiwa sana na waumini wa dini ya kibudha ya kitibet

cri

Zaidi ya miaka 10 iliyopita, mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 5 wa kabila la watibet alirithi rasmi kuwa Panchen Lama wa 11 kutokana na utaratibu wa dini ya kibudha ya kitibet. Tarehe 8 mwezi huu sherehe ya kuadhimisha miaka 10 tangu Panchen Lama wa 11 arithi nafasi hiyo, ilifanywa kwa shangwe kwenye hekalu la Tashilhungpo mkoani Tibet anakoishi na kujifunza mambo ya kibuda.

Siku hiyo kwenye hekalu la Tashilhungpo lililoko kwenye mji wa Xigaze, sehemu ya kusini ya mkoa unaojiendesha wa Tibet, watawa na waumini wa dini ya kibudha ya kitibet walivaa mavazi maridadi wakishika udi, kitambaa cheupe cha Hada na maua mikononi, wakiadhimisha miaka 10 ya urithi rasmi wa Panchen Lama wa 11. Bwana Jampa Tashi kutoka sehemu ya Qamdo, mashariki ya Tibet alisema kuwa, kabla ya nusu mwezi uliopita alipata habari kwenye televisheni kuhusu sherehe hiyo, hivyo yeye na wenzake walikwenda kushiriki kwenye sherehe hiyo. Akisema:

"Mara hii sisi si kama tu tulipata fursa ya kumwabudu Panchen Lama, bali pia tulipewa baraka kwa kupapaswa utosi, tulifurahi sana. Natumai kuwa, Budha hai wa Panchen ataweza kufanya shughuli za kibudha nyumbani kwetu, ili kuwabariki waumini wote wa nyumbani kwetu."

Panchen Lama ni mmoja kati ya viongozi wa dini ya kibuda ya kitibet, maana ya Panchen ni mtu mwenye elimu ya juu. Kuanzia mwanzoni mwa karne ya 18, Panchen wote wanapaswa kuidhinishwa na serikali kuu. Zaidi ya miaka 16 iliyopita, Panchen wa 10 alifariki dunia, na kazi ya kumtafuta mtoto wa kiume aliyeaminiwa kuingiwa roho ya marehemu Panchen Lama wa 10 ilianza kufanyika kwa kufuata kanuni za kibudha za kitibet. Kikundi kilichoundwa na watawa kadhaa maarufu kilikwenda kwenye sehemu mbalimbali mkoani Tibet kumtafuta mtoto aliyeaminiwa kuingiwa na roho ya marehemu Panchen Lama wa 10. Baada ya miaka 6, watoto watatu walithibitishwa kuwa wagombea Panchen Lama wa 11. Mwezi Novemba mwaka 1995, sherehe ya kumthibitisha mtoto halisi aliyeingiwa roho ya marehemu Panchen Lama wa 10 ilifanyika kwenye hekalu la Jokhang la Lhasa, mji mkuu wa mkoa wa Tibet kwa njia ya kuchagua moja ya vibao vitatu vyenye majina kwa njia ya bahati nasibu. Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 5 wa kabila la watibet aliyeitwa Gyantsen Norpo alithibitishwa kuwa mtoto aliyeingiwa roho ya marehemu Panchen wa 10. Baada ya kuidhinishwa na serikali kuu ya China, tarehe 8 Desemba mwaka 1995 Gyantsen Norpo alirithi rasmi kuwa Panchen Lama wa 11 kwenye hekalu la Tashilhungpo.

Hekalu la Tashilhungpo lilijengwa katikati ya karne ya 15, kuanzia Panchen Lama wa kizazi cha 4, hekalu hilo limekuwa makazi na mahali pa kujifunza mafundisho ya kibuda kwa Panchen. Kwenye hekalu hilo, Panchen Lama wa 11 alianza kujifunza ujuzi wa aina mbalimbali kuhusu dini ya kibudha ya kitibet. Bwana Jamyang Gyatso ni mwalimu wa Panchen Lama wa 11. Alisema:

"Mafundisho ya dini ya kibudha ya kitibet yana sehemu mbili za dini ya kibudha ya ndani, na ya madhehebu yanayofahamika kwa watu wote, si rahisi kufikia kiwango kinachotakiwa."

Jambo linalomfurahisha mwalimu huyu ni kwamba, Panchen wa 11 ana akili nyingi, ni rahisi kwake kujifunza mafundisho ya kidini.

Katika mafundisho ya mahekalu ya dini ya kibuda ya kitibet, kusoma na kulumbana msahafu ni njia mbili muhimu. Katika miaka 10 iliyopita, Panchen wa 11 alikuwa analumbana mara kwa mara na watawa wengine wenye ngazi ya juu kuhusu mambo yaliyomo kwenye msahafu, ili kujiandaa kipaji cha kusema, na kuzidisha ufahamu wake kwa mafundisho ya dini ya kibudha. Mtawa Nyandrak alisema, katika miaka 10 iliyopita, Panchen Lama wa 11 amepata maendeleo ya ajabu.

"Panchen Lama wa 11 anaweza kughani misahafu mingi ya kibudha. Pia ameendesha shughuli nyingi za kibudha. Vitendo vyake vinaambatana na imani ya dini ya kibudha, akiwa amerithi jadi za mapanchen waliomtangulia. Naamini kuwa, Panchen Lama wa 11 atakuwa kiongozi maarufu wa dini ya kibudha ya kitibet atakayetoa mchango mkubwa kwa dini ya Budha na waumini wa dini hiyo, na amani ya China na dunia kwa ujumla.

Katika miaka 10 iliyopita Panchen Lama wa 11 ametembelea sehemu nyingi za kabila la watibet, kufanya mihadhara mia moja hivi ya kidini, kuwabariki waumini zaidi ya laki tatu kwa kupapasa utosi, vitendo vyake vimeleta athari nzuri sana katika watawa na waumini wa Tibet. Kwenye mahekalu makubwa na madogo ya Tibet, kama vile kasri la Potala, hekalu la Jokhang, na hekalu la Zhaibung, sanamu ya Panchen wa 11 inaonekana hapa na pale, na watu wanaoamini dini hiyo wanaabudu sanamu yake. Katika hekalu la Tashilhungpo, watawa wenye ngazi ya juu kutoka sehemu mbalimbali humiminikia kukutana na Panchen wa 11, na kumpatia sanamu za kibudha na vitabu vya misahafu, hata Buddha hai anayeishi katika nchi za nje aliongoza wafuasi wake kwenda Tibet kumwabudu Panchen Lama wa 11.

Kwenye sherehe ya maadhimisho. Panchen Lama wa 11 aliahidi:

"Nitaendelea kujifunza mafundisho ya dini ya kibudha, kufuata jadi nzuri za mapanchen walionitangulia ya kupenda taifa na dini ya kibudha ya kitibet, ili kuchangia kuleta muungano wa taifa na mshikamano wa makabila, utulivu na maendeleo ya Tibet, na kueneza dini ya kibuddha ya kitibet."