Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-23 20:16:14    
Ushirikiano kati ya Afrika na China katika sekta ya biashara wanufaisha pande mbili

cri

Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari alipotembelea nchini Kenya, aliwahi kupata nafasi na kuzungumza na mhudumu wa hoteli moja nchini Kenya, ambapo walizungumzia masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta mbalimbali, usikivu wa matangazo ya idhaa ya kiswahli nchini Kenya na kadhalika. Sasa tunawaletea mahojiano kati ya mwandishi wetu wa habari na mhudumu huyo wa hoteli moja ya Kenya.

Jina lako nani? Unafanya kazi katika hoteli hiyo?

Ndiyo, nafanya kazi katika hoteli hiyo inayoitwa Simba hoteli ambayo inawapokea watalii kutoka nchi mbalimbali duniani. Hoteli yetu hapa kuna mazingira mazuri, na chakula cha hoteli hiyo pia ni nzuri, tunawakaribisha wageni wanaotembelea nchini Kenya waje hoteli yetu.

Wewe unajua serikali za China na Kenya zimesaini makubaliano kuhusu Kenya kuwapokea watalii kutoka China?

Ndiyo, najua, hivi sasa kila mara ndege ya Kenya inaweza kuwachukua watalii kutoka China kuja Kenya kutembelea wataweza kukaa hoteli yetu yenye huduma nzuri.

Na nyini mnaona ushirikiano kati ya China na Afrika na kati ya China na Kenya unaweza kuleta manufaa?

Naona ushirikiano kati ya China na Kenya ni mzuri sana, ambao unaweza kuleta manufaa kwa wananchi, kama sisi wageni wa China wakija, mapato ya hoteli yetu yanaongezeka, na pato letu pia linaongezeka.

Kwenye ushirikisho huo unasaidia uchumi, unaonaje, serikali za China na Kenya na wananchi wake wangefanya juhudi kuendeleza ushirikiano huo, siyo?

Ndiyo, ushirikiano huo ungedumishwa daima, kwani ushirikiano kati ya nchi zetu mbili unatunufaisha watu wa pande mbili, tunapenda ushirikiano huo uendelee siku hadi siku.

Naona unajua kusema vizuri kiswahili zaidi kuliko wengine?

Ndiyo mimi niliwahi kusoma shuleni, tena nafanya kazi ya mhudumu, wageni wetu wengi wanajua kusema kiswahili, hata watu kutoka nchi za Ulaya, ninaongea sana kiswahili.

Niliambiwa kuwa wakenya wengi siku hizi wameanza kuongeza zaidi kwa kiswahili.

Ndiyo siku hizi wakenya wengi wanapenda kuongea kiswahili, hata radio yetu inatangaza kwa kiswahili, inatusaidia kujifunza zaidi kiswahili.

Kweli tunaona kiswahili ni chombo muhimu cha kufanya mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika, hata kati ya watu wa nchi mbalimbali za Afrika.

Ndiyo, kiswahili ni chombo muhimu, tunapenda lugha ya kiswahili.

Uliwahi kusikiliza matangazo ya idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa yaliyorushwa hewani kwa kupitia Radio KBC?

Ndiyo, niliwahi kusikiliza matangazo hayo, nilimjua mtangazaji wenu Fadhili Mpuji, na wewe Chen. Ulisoma wapi kiswahili?

Niliwahi kusoma nchini Tanzania, mara mbili kwa miaka mitatu. Unajua wenzako wanasikiliza matangazo yetu?

Ndiyo, wenzangu wengi wanasikiliza matangazo ya Radio China kimataifa, wanapenda kusikiliza.

Kwa nini wanapenda kusikiliza matangazo yetu?

Kwa kuwa matangazo ya Radio China kimataifa yanahusu mambo mengi ya China na nchi za Afrika, na mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika, hivyo wanapenda kusikiliza.

Umepata habari kuhusu Radio China kimataifa imeruhusiwa na serikali ya Kenya na kujenga kituo chake cha FM Nairobi Kenya?

Nimeabiwa, naona hii ni nzuri, kituo hiki kikijengwa, matangazo yenu yataongezwa muda.

Ndiyo, idhaa ya kiswahili hakika itaongeza muda wa matangazo yake, je, mnapenda zaidi kusikiliza vipindi gani?

Tunapenda kusikiliza vipindi kuhusu uchumi, utamaduni, sayansi na teknolojia au mambo mbalimbali kuhusu China.

Asante sana.