Hali ya wasiwasi kwenye peninsula ya Korea yapungua kwa ujumla na nafasi ya kuelekea kwenye utulivu inaonekana. Mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyukilia la peninsula la Korea yamerejeshwa na kupata maendeleo muhimu ya kipindi; Mazungumzo kati ya serikali za pande mbili za kaskazini na kusini za peninsula ya Korea yanafuata njia ya maendeleo, na maelewano na ushirikiano kati ya pande hizo mbili vimeendelezwa zaidi. Mambo yote hayo yanaonesha kuwa mchakato wa amani ya peninsula ya Korea umepiga hatua moja madhubuti katika mwaka 2005.
Suala la nyukilia la peninsula ya Korea ni suala linalofuatiliwa zaidi hivi sasa kuhusu hali ya peninsula hiyo. Kutokana na kuathiriwa na mambo mengi, mazungumzo ya pande 6 yalikwama baada ya mwezi Juni mwaka 2004. Kutokana na jitihada za pande mbalimbali husika, mazungumzo ya pande 6 ya duru la 4 yalifanyika katika vipindi viwili mwezi Julai na mwezi Septemba. Baada ya mazungumzo magumu, pande mbalimbali hizo zilipitisha waraka wa kwanza wenye maana, tangu mazungumzo ya pande 6 yaanze kufanyika. Baada ya kufanyika kwa duru la 5 la mazungumzo ya pande 6 azma ya pande hizo ya kutekeleza waraka huo ilionekana. Kiongozi wa ujumbe wa Korea ya kaskazini unaoshiriki kwenye mazungumzo ya pande 6 ambaye ni naibu waziri mkuu Bw. Kim Kye-gwan baada ya mazungumzo alisema,
"Mazungumzo yamekuwa na maoni ya namna moja ya kutekeleza 'Taarifa ya Pamoja' kwa kufuata 'ahadi kwa ahadi' na 'vitendo kwa vitendo'. Tumeamua kuanzisha mazungumzo ya kipindi cha pili ya duru la 5 la mazungumzo ya pande 6 mapema iwezekanavyo. Katika kipindi cha kwanza cha mazungumzo ujumbe wa Korea ya kaskazini ulieleza nia yake ya kutekeleza 'taarifa ya pamoja' na kufanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na silaha za nyukilia na ulitoa miswada kadhaa, ambayo mambo yaliyo muhimu ni pande mbalimbali zichukue msimamo wenye kanuni za 'vitendo kwa vitendo' na kuzitekeleza kwa vitendo kwa wakati mmoja.
"Taarifa ya Pamoja" imeandikwa ahadi za makini za kisiasa za pande mbalimbali kuthibitisha kanuni na lengo la kuifanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na silaha za nyukilia kwa njia ya amani. Korea ya kaskazini imeahidi kuacha mipango yote iliyopo hivi sasa ya kuhusu silaha za nyukilia, kurejea "mkataba ya kutoeneza silaha za nyukilia" na mfumo wa usimamizi wa shirika la nishati ya atomiki la kimataifa. Marekani inatakiwa kuhakikisha kwamba baada ya kuthibitishwa kutokuwepo na silaha za nyukilia kwenye peninsula ya Korea, haitaishambulia Korea ya Kaskazini kwa silaha za nyukilia au za kawaida.
Vyombo vya habari vinaona kuwa "taarifa ya pamoja" imeweka kanuni kwa utatuzi wa suala la nyukilia la peninsula ya Korea, na pia imeweka msingi wa kuimarisha hali ya kuaminiana kati ya Korea ya kaskazini na Marekani. Hivyo maendeleo hayo ni hatua moja muhimu kwa mchakato wa amani kwa peninsula ya Korea.
Kutokana na kuathiriwa na matukio kadha wa kadha, uhusiano kati ya Korea ya kaskazini na Korea ya kusini ulikuwa mbaya tokea nusu ya pili ya mwaka 2004. Kutokana na jitihada za pande mbili, mazungumzo na maingiliano ya serikali na watu wa Korea ya Kaskazini na Kusini yalifikia kiwango cha juu katika mwaka 2005. Shughuli kubwa za kusherehekea kufanyika kwa mazungumzo ya Korea za kaskazini na kusini na kutimia kwa miaka 5 tangu kupitishwa "Azimio la Kaskazini na Kusini" zilifanyika; Mazungumzo ya mawaziri ambayo ni ya ngazi ya juu kabisa kati ya serikali za nchi hizo mbili yalirejeshwa na kupata maendeleo halisi; katibu wa kamati kuu ya chama cha leba cha Korea ya Kaskazini Bw. Kim ki-Nam alishiriki kwenye sherehe kubwa ya muungano wa amani iliyojulikana kuwa ni sherehe kubwa ya taifa ya tarehe 15 Agosti, kutoa heshima kwenye makaburi ya taifa ya Korea ya Kusini na kutembelea kwa mara ya kwanza bunge la nchi hiyo.
Takwimu mpya zilizokusanywa na Korea ya Kusini zinaonesha kuwa thamani ya biashara kati ya Korea ya Kusini na Kaskazini ya mwaka huu imezidi bilioni 1 ya dola za kimarekani kwa mara ya kwanza, ambapo ushirikiano na maingiliano katika maeneo ya utamaduni, kilimo, utalii, michezo na kukabiliana na maafa ya kimaumbile pia yamepata maendeleo ya kufurahisha.
Idhaa ya Kiswahili 2005-12-23
|