Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-26 15:06:35    
Mji mdogo wa kale Nanxun

cri

Katika mkoa wa Zhejiang, mashariki ya China kuna tambarare moja yenye ustawi inayoitwa Tambarare ya Ziwa Hangjia. Sehemu hiyo si kama tu ni sehemu inayozalisha mazao ya majini na mazao ya kilimo, bali pia inasifiwa kuwa ni sehemu inayozalisha hariri nzuri zaidi. Nanxun ni mji mdogo wa wilaya uliopo kwenye tambarare hiyo, mji huo mdogo uliwahi kuwa na ustawi mkubwa, mpaka sasa mabustani makubwa na madogo zaidi ya 20 yanahifadhiwa vizuri kwenye sehemu hiyo.

Mji mdogo wa kale Nanxun umekuwa na historia ya zaidi ya miaka 700, mji huo una utamaduni wa tangu enzi na dahari, mandhari ya mji huo ni nzuri. Mjini humo mito mbalimbali inapitana, njia zote mjini zilijengwa kando ya mito, na nyumba zote zilijengwa kwa kuegemea mito. Njia mbalimbali zilizopo mjini si pana, hata milango ya maduka madogo yaliyopo kando ya njia pia ni midogo, na milango yote ni ya mbao, juu yake zimening'inizwa taa za kichina, yote hayo yanaonesha hali ya zama za kale. Mwenyeji wa huko Bwana Zhang Xifu alituambia kuwa, katika sehemu hiyo yenye eneo la kilomita 3 za mraba, waliwahi kuwepo matajiri wengi. Alisema:

Katika mji wetu mdogo walijitokeza matajiri wengi, miongoni mwao, matajiri 12 ambao walikuwa ni mamilionea.

Wafanyabiashara wa mji huo mdogo walijihusisha na biashara ya hariri kuanzia karne ya 17, hivyo mji Nanxun ulijulikana nchini China kutokana na biashara yake ya hariri. Zaidi ya miaka 180 iliyopita, hariri kutokaa Nanxun ilisafirishwa kwenda nchini India, Misri, Syria na nchi nyingine. Mwaka 1915, hariri za Nanxun ziliwahi kupewa tuzo ya dhahabu kwenye Maonesho ya vitu ya kimataifa ya Panama. Biashara ya hariri ya Nanxun iliwaletea wafanyabiashara wa Nanxun mali nyingi, hivyo wafanyabiashara hao walijenga makazi ya anasa katika maskani yao.

Xiaolianzhuan ni makazi ya familia ya Liu Yong, tajiri mkubwa kabisa wa wakati huo, pia ni bustani kubwa kabisa iliyobaki mpaka sasa huko Nanxun. Familia Liu ilitumia zaidi ya miaka 40 kukamilisha ujenzi wa bustani hiyo yenye eneo la mita zaidi ya elfu 17. Upande wa kaskazini wa Xiaolianzhuan kuna kijito maarufu cha Partridge, kando ya kijito hicho kuna mti mmoja mkubwa sana wa cinnamomum camphora, kwenye kijito kuna daraja moja dogo la mawe, kama tukipita kwenye daraja hilo tunaweza kuingia kwenye bustani hiyo la kale. Majengo ya bustani hiyo yalijengwa kwa mtindo dhahiri wa sehemu ya kusini mwa mto Changjiang, ndani ya bustani kuna dimbwi moja la maua ya yungiyungi, nyumba, roshani na vibanda vyote vilijengwa kwa kuegemea dimbwi, kwenye bustani hilo, yalipandwa maua na miti mingi yenye thamani, kwenye kona ya kusini mashariki ya bustani hilo, kuna ua pekee mdogo ambao unasifiwa kuwa ni bustani ya ndani, na sehemu ya nje ya ua hilo inaitwa ni bustani ya nje. Katika bustani hilo dogo, kuna mlima mdogo, juu ya mlima kuna kibanda kimoja, kwenye kibanda hicho, watu wanaweza kuona mashamba makubwa ya mpunga nje ya kuta za bustani.

Mtalii Bi. Li Bei alituambia, anapenda sana bustani hilo dogo lililojengwa kwa maumbo yanayopendeza. Akisema:

Bustani za nje na ndani zinatofautiana pia zinaungana pamoja, naona maumbo ya bustani ni ya kupendeza, ndani ya bustani kuna mlima na mto, vibanda na roshani, ujenzi wake una mtindo dhahiri wa ujenzi wa mabustani ya sehemu ya kusini mwa mto Changjiang.

Sehemu ya Banjialou pia ni sehemu inayostahili kutembelewa. Sehemu hiyo kuna majengo mengi yaliyojengwa kando ya mto. Mwongoza wa utalii Bi.Zhang Qian alijulisha kuwa, Sehemu ya Banjialou ilijengwa zaidi ya miaka 400 iliyopita, vijakazi wanawake mia moja wa familia moja yenye utajiri huko Nanxun walikuwa wakazi wa kizazi cha kwanza katika sehemu ya Banjialou. Alisema:

Inasemekana kuwa, kabla ya miaka 400 na zaidi, mtoto wa familia Dong ya diwani mmoja wa Nanxun alitaka kumwoa binti wa familia ya Mao yenye utajiri. Lakini wakati walipokaribia kuoana, wazazi wa binti huyo walisema familia Dong hakuna nyumba kubwa, walituma mshenga kwenda familia Dong kuwa familia ya Mao itatuma vijakazi wanawake 100 kuambatana na binti huyo kuolewa, lakini familia yenu hakuna nyumba, lakini familia Dong ilisema, si kitu, tutajenga nyuma 100 mara moja, kila kijakazi atakaa kwenye nyumba moja, hivyo sehemu ya Banjialou imebaki mpaka hivi sasa.

Lakini nyumba walizowajengea vijakazi hakika ni tofauti na makazi ya watu matajiri kama vile Xiaolianzhuan, nyumba hizo walizokaa watumishi ni za kawaida, lakini kila nyumba ina mlango wake wa duara, na sehemu iliyo kati ya kila nyumba kuna ukuta. Baada ya mabadiliko ya miaka mingi, wakazi wa sehemu hiyo ya Banjianlou, sio vijakazi tena wa zama za kale, hata nyumba zao siyo mia moja tena, hakika hazina sura ile ya zama za kale, lakini nyumba hizo zimedumisha mtindo wao maalum wa makazi ya raia wa sehemu zilizo kusini mwa Mto Changjiang, kuta za nyumba zina rangi nyeupe, na paa ni za rangi nyeusi, nyumba hizo zilizoko kando ya mto zinaonekana katika hali yake ya asili na ya kupendeza.

Hali ya utulivu na ukimya ni umaalum katika mji mdogo Nanxun, kila siku unaweza kuona wakazi kadha wa kadha wa Nanxun wanaopita pita milango yenye umbo la duara, hawapigi kelele, hata baadhi ya wakati pikipiki moja ikipita huko, dereva wa pikipiki hiyo pia anaendesha pikipiki hiyo kwa mwendo polepole, kama anaogopa kusumbua utulivu wa mji huo mdogo, ambapo mjini humo unaweza kuwakuta wazee kadha wa kadha wanaopiga soga chini ya mwangaza wa jua wakati wa siku za baridi, lakini unaweza kuona, wazee hao wanaongea kwa sauti ya chini. Kila mmoja hataki kusumbua hali ya utulivu na ukimya wa mjini humo.

Ukipata nafasi karibuni kwenye mji wa Nanxun ushuhudie hali halisi ya huko.

Idhaa ya kiswahili 2005-12-26