Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-27 16:15:50    
Mageuzi ya benki nchini China yapata maendeleo makubwa

cri

Baada ya Benki ya China na Benki ya Ujenzi, ambazo ni benki za biashara za serikali nchini China kufanyiwa mageuzi ya hisa katika mwaka 2003, mwaka huu Benki ya Biashara ya China pia imeanza kufanyiwa mageuzi ya hisa, na Benki ya Mawasiliano na Benki ya Ujenzi zimeingia katika soko la hisa. Baada ya kufanyiwa mageuzi, Benki ya China na Benki ya Ujenzi zimeimarika katika faida za biashara, hali ya raslimali na nguvu halisi ya raslimali. Tokea Benki ya Viwanda na Biashara ya China ifanyiwe mageuzi, kazi ya kuunda upya taratibu za mambo ya fedha ndani ya benki hiyo kimsingi imemalizika, hali ya mambo ya fedha imeboreshwa na nguvu halisi ya raslimali imeongezeka wazi na ubora wa raslimali umeinuka kwa kiwango kikubwa, mageuzi ya menejiment ya shughuli za benki yanaendelea kufanyika na yamepata maendeleo makubwa.

Tokea mwezi Juni mwaka 2003 mageuzi ya benki ya maendeleo ya kilimo yalipoanza, hivi sasa mageuzi hayo yameenea katika mikoa 30 na mageuzi yamepata mafanikio ya mwanzo. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka 2005 benki hiyo imefungua matawi 57 nchini China na kwenye ngazi ya wilaya idara zake za fedha 325 zimeanzishwa, shughuli za benki zinazoshughlikia kilimo zinaendelea haraka na biashara zimekuwa nzuri, mizigo ziliyokuwa nayo kwa muda mrefu imepungua, na kwa ujumla uwezo wa kupambana na hatari umeongezeka. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka 2005 raslimali za benki ya maendeleo ya kilimo zimekuwa na yuan trilioni 3.6, na mikopo mibaya imekuwa asilimia 15.9 ambayo imepungua kwa asilimia 21.4 ikilinganishwa na mwaka 2002, na akiba baada ya kutoa mikopo ni yuan trilioni moja, mikopo ya kilimo inachukua asilimia 47 ya mikopo yote ambayo ni asilimia 85 ya mikopo ya kilimo ya idara zote za fedha.

Imefahamika kuwa Kamati ya Usimamizi wa Benki ya China mwaka huu inahimiza mageuzi ya menejimenti ya mashirika ya kusimamia mambo ya fedha na imetoa "mwongozo wa kushughulikia raslimali zisizo halali", kuhimiza kuimarisha usimamizi wa kazi za mashirika ya mambo ya fedha, kuimarisha udhibiti wa shughuli mbaya na kusukuma kuboresha shughuli na kuhimiza mashirika ya kusimamia raslimali yapate maendeleo endelevu; Kutafiti uzoefu wa mageuzi ya benki ya maendeleo, benki ya maendeleo ya kilimo na benki ya kuagiza na kuingiza bidhaa ya China na kusukuma mbele utungaji sheria. Isitoshe, mageuzi ya benki ya posta pia yataanza.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka 2005 kwa jumla kuna benki na idara mbalimbali za fedha zaidi elfu 30 zenye thamani ya fedha yuan trilioni 36.2, hili ni ongezeko la asilimia 19.2 ikilinganishwa na mwaka jana, raslimali za benki na idara hizo zinachukua zaidi ya asilimia 90 ya raslimali za idara zote za fedha nchini China, shughuli za benki zimekuwa nguzo katika mambo ya fedha nchini China.

Idhaa ya kiswahili 2005-12-27