Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-28 21:27:29    
Mikopo yawawezesha wanafunzi maskini elfu 80 kusoma katika vyuo vikuu nchini China

cri

Mwezi Septemba mwaka huu, kijana Zhang Tianfu wa familia maskini katika wilaya ya makabila ya Watujia na Wamiao mkoani Guizhou alipopata taarifa ya kukubaliwa kujiunga na chuo kikuu iliyoambatanishwa na maelezo kuhusu mikopo ya serikali uso wake ulioonesha kutokuwa na furaha ulionesha ufuraha. Alipofika kwenye chuo kikuu alikamilisha taratibu za kupata mkopo wa yuan elfu 20 kwa muda wa saa moja tu, licha ya ada kila mwezi anapewa yuan 200 za posho.

Bi. Chen Jia, alihitimu masomo katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Guizhou mwezi Julai na alipata kazi anayoipenda ya ualimu katika sekondari moja. Kila mwezi kabla ya tarehe 19 lazima anakwenda kwenye benki ya kilimo kulipa deni la mkopo huo kwa yuan 300. Bi. Chen Jia akiwa mmoja wa wanafunzi waliobahatika kupata mikopo ya masomo kwa awamu ya kwanza alimaliza masomo yake bila tatizo. Bi. Chen Jia alisema, "Bila msaada wa mkopo wa serikali nisingeweza kuwa mwalimu wa sekondari."

Mkoa wa Guizhou ni moja ya mikoa kadhaa iliyotangulia kutoa mikopo kwa ajili ya wanafunzi maskini. Tokea mwaka 2000 hadi sasa wanafunzi wa familia maskini 80382 wamepata mikopo ya masomo yenye thamani ya yuan milioni 235. Tokea mwezi Septemba mwaka 2004 sera mpya ilipoanza kutekelezwa wanafunzi 37023 wamepata mikopo ya masomo yenye yuan milioni 108. Hivi sasa wanafunzi wanaopata mikopo ya masomo wanachukua asilimia 14.7 ya wanafunzi wote wa vyuo vikuu mkoani Guizhou.

Kutokana na kuwa mkoa wa Guizhou kuwa na wanafunzi wengi maskini, sera ya kutoa mikopo ya masomo huko huko wanafunzi walipo kutoka benki za kilimo, kwamba wanafunzi wanaofanikiwa kupokelewa na vyuo vikuu wanapata mikopo hiyo kwa ushahidi wa taarifa ya kupokelewa na vyuo vikuu kutoka benki za kilimo huko kwa kiasi ambacho juu kabisa ni yuan 6,000 ili kuwasaidia tatizo la usafiri na karo na gharama nyingine na kuhakikisha wanaweza kufika kwenye vyuo vyao. Mikopo ya masomo inayotolewa sehemu waliko wanafunzi ni nyongeza ya mikopo ya masomo ya kiserikali. Mwaka huu, mkoani Guizhou kuna wanafunzi 1795 waliopata mikopo inayotolewa na benki ya kilimo wanafunzi walipo, na jumla ya mikopo hiyo ni yuan milioni 7.719, kwa wastani kila mmoja anapata yuan 4,300.

Hivi sasa vyuo vikuu 34 vimeshiriki kwenye ushirikiano na benki, na licha ya kushirikiana katika mikopo, pia vinashirikiana katika mambo mengine.

Namna ya kuzuia mikopo mibaya na kurudisha mikopo kwa wakati ulioahidiwa ni jambo muhimu katika shughuli za mikopo. Vyuo vikuu licha ya kuwaelimisha wanafunzi waliopata mikopo wafuate mkataba wa kulipa mikopo, vinashirikiana na benki kufanya ukaguzi, usimamizi na kuhimiza.

Siku chache zilizopita, mkoa wa Guizhou ulifanya ukaguzi wa hali ya kulipa mikopo kwa wanafunzi waliopata mikopo ya masomo kwa awamu ya kwanza, kwamba kati ya wanafunzi 379 waliopata mikopo wanafunzi 367 wamekamilisha mikopo ambayo jumla ni yuan laki 9.6, hii ni asilimia 96.8 ya wanafunzi waliolipa mikopo na 97.4 ya mikopo iliyolipwa.