Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-12-28 21:58:20    
Mchakato wa ujenzi mpya wa kisiasa nchini Iraq wapatwa shida nyingi

cri

Uchaguzi wa kwanza rasmi wa bunge la Iraq ulifanyika bila matatizo tarehe 15 mwezi Desemba. Hivi sasa kazi ya kuhesabu kura zilizopigwa bado inaendelea, na matokeo kamili yanatazamiwa kufahamika mwanzoni mwa mwezi Januari mwakani. Kuhusu umuhimu wa uchaguzi huo, rais Jalal Talabani wa serikali ya mpito ya Iraq siku hiyo alipopiga kura alisema,

"Leo ni siku ya furaha kwa nchi nzima, watu wa Iraq wamekuwa na haki ya kuchagua wenyewe wabunge wa taifa."

Ikilinganishwa na uchaguzi wa bunge la mpito mwanzoni mwa mwaka huu, katika uchaguzi huo wa bunge hali nchini Iraq kidogo ilikuwa shwari, wapigaji kura wa nchini na wale waliotoka nchi za nje, hususan watu wa madhehebu ya Sunni walishiriki kwa wingi, hata hivyo kuna baadhi ya makundi ya kisiasa yalieleza mashaka yao kuhusu haki kwenye uchaguzi huo. Huu ni umaalum wa ujenzi mpya wa kisiasa nchini Iraq katika mwaka zaidi ya mmoja uliopita: ingawa ujenzi mpya umepatwa shida nyingi, lakini bado unapiga.

Tarehe 30 mwezi Januari mwaka huu, Iraq ilifanya uchaguzi wa bunge la mpito, ambao ni hatua ya kwanza iliyopita Iraq ya kumaliza ukaliaji wa majeshi ya kigeni na kujenga Iraq mpya yenye demokrasia na uhuru. Lakini kususia uchaguzi huo kulikofanywa na madhehebu ya Sunni kumeleta mashaka kwa uhalali na matokeo ya uchaguzi huo, hali ambayo imekuwa chanzo cha migogoro ya makundi mbalimbali na msukosuko wa siasa katika siku za baadaye. Tarehe 3 mwezi May, wafuasi wa madhehebu ya Shiya na wa-Kurd ambao wana viti vingi katika bunge, waliunda umoja na kuanzisha rasmi serikali ya mpito, kwenye mchakato wa siasa madhehebu ya Sunni yametelekezwa, hatua ambayo ni matokeo ya kuvunjika kwa mazungumzo ya kuunda baraza la serikali katika muda wa miezi karibu mitatu iliyopita kwa makundi ya madhehebu ya Shiya, Kurd na Sunni. Migongano ya maslahi ya makundi hayo matatu, imeathiri mchakato wa ujenzi mpya wa kisiasa nchini Iraq na kuifanya Iraq ikabiliwe na hatari ya mfarakano na mapambano ya wenyewe kwa wenyewe. Profesa wa idara ya uhusiano wa kimataifa ya chuo kikuu cha Qatar Bw. Mohammad Saleh Al-Musfir amesema, hali ya namna hiyo ni matokeo ya kukosa msingi wa demokrasia nchini Iraq na kwamba demokrasia ya aina ya Marekani haiendani na hali halisi ya nchi hiyo. Alisema,

"Serikali mpya ilishindwa kuasisiwa katika siku zaidi ya 90 baada ya uchaguzi wa bunge, hali kama hii haikuonekana katika uchaguzi wa nchi yoyote duniani, hii siyo demokrasia ya kweli. Serikali ya mpito iliyoanzishwa kutokana na uungaji mkono wa wakaliaji wa Marekani na Uingereza ni dhaifu sana kutokana na kukosa uungaji mkono wa watu wa sekta mbalimbali wa nchi hiyo."

Moja ya changamoto kubwa kwa serikali ya mpito ya Iraq ni utungaji wa mswada wa katiba mpya ya nchi, na kuandaa upigaji kura za maoni kuhusu mswada huo. Baada ya kufanya majadiliano, madhehebu ya Shiya na watu wa Kurd waliafikiana na chama cha kiislamu cha Iraq ambacho ni cha kwanza kwa ukubwa cha madhehebu ya Sunni, kuhusu mswada wa katiba, ambao ulipigiwa kura za maoni ya rais tarehe 15 mwezi Oktoba. Hapo baadaye mswada huo wa katiba ulipitishwa kwa 78% ya kura. Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa masuala ya mashariki ya kati ya taasisi ya utafiti wa masuala ya kimataifa ya China Bw. Li Guofu alipofanya tathmini kuhusu katiba hiyo alisema, "Katiba hiyo ilipitishwa baada ya watu na makundi mbalimbali ya Iraq kufanya majadiliano marefu, hivyo ni msingi mzuri kwa ujenzi mpya wa kisiasa nchini humo.

Vyombo vya habari vinaona kuwa ingawa mchakato wa ujenzi mpya wa siasa wa Iraq umeingia kwenye njia sahihi, lakini utakabiliwa changamoto nyingi zisizojulikana, hivyo wachambuzi wanasema kuwa kwa upande mmoja makundi mbalimbali nchini Iraq yanatakiwa kujitahidi kwa pamoja ili kutimiza maelewano ya kitaifa; kwa upande mwingine majeshi ya kigeni yanatakiwa kuondoka hatua kwa hatua kutoka kwenye nchi hiyo. Aidha Umoja wa Mataifa unatakiwa kuelekeza mchakato wa ujenzi mpya wa kisiasa wa Iraq.